Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
1628658894680.png

Kifafa ni nini?
Kifafa ni ugonjwa wa ubongo.

Ubongo wa binadamu una mabilioni ya seli za neva. Zinashirikiana na kila moja kupitia chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima.Wakati baadhi ya ama hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na husababisha kifafa ama kuzirai.

Kuzirai kwa ghafla huathiri vile ubongo hufanya kazi.Kunaweza kumsababisha mtu kupata mabadiliko ya ghafla katika fahamu, mwendo ama hisia.

Mshtuko wa moyo mmoja haumanishi ya kwamba mtoto ana kifafa.Kuzirai mara moja kunaweza kutokea kwa sababu tofauti k.m homa, jeraha la kichwa, kiwango cha chini cha sukari katika damu na kadhalika.

Kifafa ni jina la kuzirai kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu ya kutibiwa inayojulikana.

Katika sehemu hii jifundishe zaidi kuhusu huu ugonjwa.

Dalili na ishara za kifafa

Nitajuaje ikiwa niimeathiriwa na kifafa?

Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya muda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa muda baada ya kuzirai.

Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa nyingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.

Katika aina nyingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.

Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.

Je, kila mtu anayeathiriwa na kifafa anapaswa kupelekwa hospitalini?
La, Sio kila mtu anayeathirika na kifafa anapaswa kupatiwa huduma ya matibabu. Mtu mwenye kifafa ambaye yuko chini ya matibabu labda hahitaji kupelekwa hospitalini mara moja. Kuna visa vingine ambavyo ni muhimu kumpeleka mtu hospitalini kama dharura.
  • Kuzirai mara ya kwanza. Ikiwa mtu anafahamika ya kwamba huwa hana kifafa na kishe azirai, mtu huyu anahitaji kumuona dakitari mara moja.
  • Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa hospitalini.Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili kuokoa maisha yake.
  • Ikiwa kupumua hakurudii hali ya kawaida baada ya kuzirai.
  • Ikiwa kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo Kabla ya mgonjwa kupata nafuu.
Je, kuna tiba ya kifafa?
Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali nyingine kama vile uvimbe kwenye ubongo, ugonjwa wa figo au ugonjwa wa Ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa muda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.

Namna nyingine za kudhibiti kifafa
Kando na madawa, ni nini kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?
Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata amedhibitiwa na matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8 ilhali mtoto anahitaji angalau masaa 9) kunaweza kusababisha mshtuko wa kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia kusababisha shambulizi. Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya kutokea kwa mshtuko wa kifafa. Taa zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa katika watu wengine. Kupumua kwa nguvu wakati unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara katika watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa unaweza kuepuka haya, unaweza kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.

Kwanini haupaswi kumwekea mtu kitu mdomoni anaposhikwa na mshtuko wa kifafa?
Kwa muda mrefu iliaminika ya kwamba wakati mtu ameshikwa na kifafa, mgonjwa anaweza kumeza ama hata kunyongwa na ulimi wake na kwa hivyo kusababisha kifo. Hivi sasa hali imebadilika na inaeleweka ya kwamba hakuna haja ya kuweka kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na kifafa. Hili linaweza kusababisha madhara zaidi.

Wakati wa kifafa kuna mshtuko wa ghafla wa misuli.Mikono, miguu na sehemu nyingine za mwili huwa na mwendo wa kujirudia rudia ambao ni vigumu kuukabili kwa kutumia nguvu haswa ikiwa mgonjwa ni mkubwa kwa umbo. Kama sehemu ya tendo la misuli, mgonjwa husaga meno yake kwa sababu ya tendo la nguuvu katika taya. Jaribio lolote la kuweka kitu kwenye mdomo linaweza kusababisha kuvunjika kwa meno ya mgonjwa, kunyongwa na kile kilichowekwa mdomoni ama mgonjwa kumuuma vibaya mhudumu wake.

Kwa hivyo fahamu: USIWEKE kitu katika mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na mshtuko wa kifafa.

Kwanini wagonjwa wa kifafa hawawezi kugawana madawa yao?
Madawa ya kifafa hufanya kazi ya kukomesha shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo. Kuna aina nyingi za kuzirai katika kifafa na hizi zote huitikia kwa njia tofauti kwa madawa tofauti. Hii ndio sababu ya kwanza kwa nini haufai kugawa dawa za kifafa. Dawa ambazo hudhibiti aina moja ya kifafa zinaweza kukosa athari kwa aina nyingine ya kifafa.

Pili, watu tofauti wanahitaji vipimo tofauti vya dawa iliyotolewa kudhibiti kifafa. Ugonjwa wa kifafa unamaanisha ya kwamba ubongo wa mtu unaweza kufyatuka kwa njia isiyo ya kawaida. Watu tofauti hupata kifafa katika viwango tofauti vya mchangamsho wa ubongo. Watu wengine huchangamshwa kwa urahisi na kuzirai ilhali wengine hawachangamshwi kwa urahisi. Kipimo cha dawa kinachotumiwa kumdhibiti mtu ambaye huzirai kwa urahisi ni tofauti na kile cha yule ambaye hazirai kwa urahisi.

Tatu, sio vizuri kugawana madawa ambayo yametolewa kufuatia maagizo ya dakitari. Maagizo ya dakitari hutoa dawa kwa mtu mmoja kwa kipindi maalumu cha wakati. Kwa kugawana madawa, mtu ambaye alipewa maagizo ya dakitari ataishiwa na dawa kabla ya ahadi ya kuonana na dakitari inayofuatia. Wanweza kuzirai kwa urahisi kwa sababu hawako kwenye matibabu. Sio salama kwa mtu mwenye kifafa kugawa dawa zake.

Matatizo yaweza tokezea wakati wa matibabu

Je, kuna jambo ambalo linaweza kuenda mrama nikiwa bado kwenye matibabu?

Athari ya matibabu ni hisia ya kusinzia na kutokuwa mwepesi ambako hutoweka baada ya muda. Baadhi ya madawa yanaweza kumfanya mgonjwa aongeze uzito. Athari mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea ni kwenye ini. Hili ni jambo la kawaida wakati mgonjwa anatumia madawa kadhaa ili adhibiti kifafa.

Unapoanza matibabu, athari yake kwa kifafa huwa siio ya papo kwa hapo. Inachukua angalau mwezi mmoja kuona athari yoyote ya kudumu na mtu anahitajiwa kuwa mvumilivu. Katika visa vichache, visa vya kuzirai vinaweza kuongezeka unapowekwa kwenye matibabu kabla kuzirai hakujapungua.

Ni kipi kipimo cha dawa za kutibu kifafa?
Kipimo cha dawa ni kile ambacho kitatibu kitadhibiti ama kitatibu hali hii bila ya kusababisha mathara mabaya ya kando. Hii hutofautiana kutoka kwa matibabu hadi matibabu na hali hadi hali. Dawa nyingine kama Panadol zina kiwango chake rasmi; watu wazima humeza vidonge 2 kila masaa 6-8. Hali nyingine kama malaria isiyo kali zina kiwango cha dawa kinachopeanwa katika kiwango cha kipimo cha dawa kama watu wazima humeza vidonge 2 vya Camoquine mara moja kwa siku 3.

Hesabu ya kiwango cha kipimo cha dawa hutegemea uzani wa mgonjwa ama umri wake. Kila aina ya dawa ina kipimo kwa uzani ama umri wa mgonjwa uliopeanwa.

Katika visa vingine vya kifafa, kiwango cha dawa hakiwezi kuhesabika kwa urahisi. Matibabu yanayotolewa ili kudhibiti kifafa huathiriwa kwa urahisi na vipimo vya dawa na hufanya kazi katika kadiri ndogo. Dawa kidogo kwenye damu ama dawa nyingi kwenye damu na udhibiti wa kifafa hupotezwa. Kwa hivyo kila dawa inaweza tu kutumiwa katika kadiri iliyotolewa ya kipimo cha dawa. Ikiwa kuzirai hakuwezi kudhibitiwa katika kadiri hii, dawa ya pili na wakati mwingine dawa ya tatu inaweza kuongezwa. Hii nyongeza ya madawa hujiathiri na kipimo cha kila dawa kinahitaji kuhesabiwa mara tena ili kila dawa ikuwe katika kiwango kinachofaa katika damu.

Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, kutokea kwa kifafa hakuwezi kutabirika katika watu tofauti. Kuna wale ambao ugonjwa wao wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ilhali wengine wanahitaji matibabu 2-3 ili kupunguza visa vya kuzirai bila ya kuvimaliza kabisa. Kwa wagonjwa 2 wenye umri sawa na uzani sawa, matibabu ya kipekee yanaweza kutolewa katika vipimo tofauti ili kudhibiti kuzirai kwao.

Ni kwa muda upi ambao mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia dawa?
Mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia madawa aliyopewa hadi ashauriwe vingine. Kwa kutegemea wingi wa kutokea kwa visa vya kifafa, wagonjwa wanaweza kutumia dawa kwa maisha yao yote. Katika watoto, hata hivyo mambo yanabadilika. Kitambo, ilichukuliwa ya kwamba mtoto mwenye kifafa ngehitajika kutumia madawa kwa miaka mingi ya maisha yake. Lakini hali sio hivyo tena. Ikiwa mtoto anatumia madawa kwa njia inayofaa na kwa wakati bila ya kukosa hata kipimo.cha dawa na anabakia bila kifafa kwa angalau miaka 2, basi daktari anaweza kufikiria kusimamisha utumizi wa madawa. Ni dakitari pekee yake anayeweza kutoa ushauri kuhusu kusimamaisha matumizi ya madawa ya kifafa baada ya kumfuatilia mgonjwa kwa kipindi fulani cha muda. Ni muhimu maamuzi haya yafanywe na dakitari, kwa sababu mwanzo utumizi wa madawa umeanza haufai kukatizwa kwa ghafla. Badala yake dakitari atapunguza kipimo cha dawa pole pole hadi matumizi ya dawa umesitishwa. Ukisitisha dawa kwa ghafla, kuna madhara ya kando kama kumwa na tumbo, kutapika na kutomakinika na kuzirai kunaweza kujirudia.

Ni muda gani unaochukuliwa ili kudhibiti kifafa?
Wagonjwa tofauti wana aina tofauti za kifafa na aina tofauti za kifafa hudhibitiwa kwa njia tofauti.Baada ya kubainika kumehakikishwa, mgonjwa huwekwa kwenye kipimo kimoja cha dawa hapo mwanzoni. Hushauriwa kurudi baada ya mwezi ama zaidi dakitari atathmini ikiwa dawa inadhibiti kifafa kwa njia inayofaa.Ikiwa sivyo, basi kipimo cha dawa huongezwa pole pole. Na ikiwa hii haina mafanikio, basi dawa ya pili huongezwa na ikiwa inahitajika, dawa ya tatu itaongezwa.

Muda unaochukuliwa kwa ugonjwa wa kifafa kudhibitiwa hutofautiana kutoka kwa mgonjwa hadi kwa mwingine.Ugonjwa wa kifafa wa mgonjwa mmoja unaweza kudhibitiwa kwa dawa moja tu.Katika visa vingine, mgonjwa anaweza kuwa akitumia madawa 3 na bado anaathirika na kifafa, ingawaje idadi ya kuzirai kunakosababishwa na kifafa kutapungua ukilinganisha na hapo awali. Wagonjwa wengine hutibika haraka kuliko wengine na aina nyingine za kifafa huwa rahisi kudhibiti kuliko nyingine.

Hakuna mbinu iliyobainika katika kudhibiti kifafa.Lengo la matibabu ni kupunguza idadi ya kuzirai kunakoathiri mgonjwa na ikiwa inawezekana kusimamisha kuzirai kabisa kwa muda mrefu.

Ni nani yuko kwenye hatari ya kupata kifafa?
Ugonjwa wa kifafa unaweza kuathiri mtu yeyote katika umri wowote. Madhara ya ubongo ndio hali ya kawaida ambayo inaweza kusababisha kifafa baadaye. Matatizo wakati wa kujifungua,homa ya nyonga ya manjano katika mwezi wa kwanza wa maisha, magonjwa ya utotoni kama homa ya uti wa mgongo ni sababu za kawaida za kifafa katika watoto. Homa kali pia husababisha kuzirai kwa watoto wadogo. Katika visa vingine kuzirai huku hufanyika kila wakati kuna homa. Mtoto ambaye amezirai mara tatu ama zaidi ambako kuna uhusiano na homa anafaa kuwekwa chini ya matibabu dhidi ya kifafa.

Watu wazima ambao huathiriwa na madhara ya ubongo kwa sababu ya jeraha, ambukizo ama kwa sababu ya ugonjwa mwingine kama maradhi ya ini, maradhi ya figo wanaweza pia kuathiriwa na ugonjwa wa kifafa.

Ni muhimu kukumbuka ya kwamba ugonjwa wa kifafa unaweza kuwaathiri watu ambao hawana madhara yoyote ya ubongo ama ugonjwa wa hapo awali. Katika visa vingine hutokea katika familia, lakini wakati mwingi hutokea bila ya sababu yoyote inayojulikana.

Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa mtu atashikwa na mshtuko wa kifafa?
Wakati mwingi, huduma ya kwanza ina maana ya kumfanya mtu awe salama wakati mshtuko wa kifafa unapotokea. Kwa bahati nzuri, mshtuko huwa mfupi na huisha baada ya dakika kadhaa.

Hatua ya kwanza katika kujitayarisha kwa ajili ya kifafa ni kufahamu kitu cha kufanya wakati ugonjwa huu unapotokea. Hii ni muhimu ikiwa unamchunga mgonjwa wa kifafa lakini pia kwa kila mtu. Ugonjwa wa kifafa unaweza kuanza katika umri wowote na kila mtu anahitaji kufahamu nini cha kufanya wakati mtu karibu nao anaathiriwa na kifafa.

Huduma ya Kwanza
  • Kuwa mtulivu na usiogope. Kifafa humuogopesha mtazamaji. Huchukua dakika chache na kwa kawaida huhitaji matibabu.Kumbuka ya kwamba mtu aliyeshikwa na kifafa huwa hafamu vitendo vyake na anaweza au asiweze kukusikia.
  • Walinde dhidi ya majeraha wakati wanaposhikwa na kifafa.Ikiwa inahitajika mweke chini kwa njia iliyo taratibu.
  • Sogeza vitu vigumu, vitu vyenye ncha kali na vilivyo moto na linda kichwa na mwili wa mgonjwa dhidi ya jeraha.
  • Usiweke chochote mdomoni ama ujaribu kubanua meno.
  • Mtu hayuko katika hatari ya kumeza ulimi wake
  • Usijaribu kuzuia mwendo wao kwa kutumia nguvu.Hili linaweza kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia yule anayejaribu kuwasaidia.
  • Popote inapowezekana, jaribu kumlaza mtoto katika sehemu iliyo laini na wageuze upande mmoja.
  • Weka kitu tambarare na laini chini ya kichwa chake ili asijiumize.
  • Fungua nguo zilizombana haswa kwenye shingo kama tai, skafu na kadhalika
  • Usiweke chochote mdomoni.
  • Nakili muda ambao mshtuko umechukua.
  • Jaribu kutazama mwondoko ambao mtu hufanya wakati ameshikwa na kifafa.
  • Wakati mkutuo unaanza kupungua, hakikisha ya kwamba kupumua kumerudia hali yake ya kawaida.
  • Baada ya kifafa, mvingirishe mtu ili alalie upande mmoja.Hili hufanya mate kutoka mdomoni na kuhakikisha ya kwamba hanyongwi. Ikiwa kuna matapishi, mweke mtu kwa upande mmoja na safisha mdomo wake kwa kidole.
  • Usijaribu kumpatia dawa ama uoevu hadi aamke
  • Waondolee hofu, zungumza nao kwa upole na wasaidie kupata nafuu pole pole.
  • Usimwache mtu pekee yake hadi apate nafuu.
Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa nadhani nimeathiriwa na kifafa?
Ni muhimu kukumbuka ya kwamba kifafa ni hali ambayo inaweza kudhibitiwa. Sio kitu cha kuona haya. Sio laana ama ulemavu. Ni hali inayohitaji matibabu na kufuatiliwa kama hali nyingine kama shinikizo la juu la damu, kisukari, pumu na kadhalika

Ikiwa unadhani ya kwamba umeathiriwa na ugonjwa wa kifafa ama ikiwa umewahi kuanguka chini na kuzimia ni muhimu kutafuta usaidizi wa dakitari aliye karibu. Ikiwa inawezekana andamana na mtu aliyekuwa nawe wakati ikifanyika ili waeleze kile walichokiona. Hili litasaidia dakitari kufanya

Ni sehemu gani ya ubongo huathiriwa na kifafa?
Ubongo ni ogani iliyo na sehemu nyingi (sehemu ya mwili) ambazo hudhibiti mwili wote. Sehemu tofauti za ubongo hudhibiti sehemu tofauti za mwili na kazi tofauti kwenye mwili. Kuna sehemu ya ubongo ambayo hudhibiti misuli ya mkono; sehemu tofauti itadhibiti kuhisi uchungu wa mkono huo huo na sehemu tofauti ya ubongo itaratibu sauti ya kupiga mayowe wakati mkono huo unahisi uchungiu ama uko kwenye hatari. Hizi sehemu zimeunganishwa na seli za ubongo (nyuroni). Muungano huu ndio ule unaoturuhusu kufanya kazi kama mtu mmoja kwa njia ya kupatana kwa misuli.

Kifafa ni shughuli isiyo ya kawaida kwenye ubongo. Sehemu yoyote ya ubongo inaweza kupatwa na jambo hili lisilo la kawaida. Kwa sababu sehemu tofauti za ubongo hudhibiti sehemu tofauti za mwili, hii ndiiyo sababu mtukutiko wa maungo katika kifafa ni tofauti kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ama pia kutoka kwa kuzirai huku na kule. Ikiwa kuna shughuli isiyo ya kawaida kwenye ubongo katika sehemu ya ubongo inayoathiri misuli ya mikono na miguu, kutakuweko msukumano mwingi katika hizo sehemu za mwili.

Shughuli hii isiyo ya kawaida kwenye ubongo inaweza kufanyika tu katika sehemu moja ya ubongo ama inaweza kusambaa katika muungano ili kuhusisha ubongo wote.Kuzimia ambako husababishwa na shughuli ya sehemu moja ya ubongo ndio kule tunakokuita kuzirai kusio kamili. Kuzirai kunakosababishwa na shughuli ya ubongo wote ndio kule tunakokuita ugonjwa wa kifafa ulio mbaya ama kuzimia kamili.

Kwa jumla tunaweza kusema ya kwamba ikiwa sehemu ndogo ya ubongo itaathirika basi mtukutiko wa maungo utakao onekana utakuwa mdogo. Ikiwa sehemu kubwa ya ubongo itaathirika basi mtukutiko wa maungo utakao onekana utakuwa mkubwa. Kuzirahi kusio kamili kutaathiri sehemu ndogo ya ubongo kuliko kuzimia kuliko kamili.

Ni vipi naweza kujilinda mimi mwenyewe na familia yangu dhidi ya kifafa?
Njia moja muhimu ya kuwalinda watoto dhidi ya hatari ya kifafa ni kuhakikisha ya kwamba wanapata chanjo zao kwa wakati unaofaa. BCG kwa mfano humlinda dhidi ya kifua kikuu. Ugonjwa wa kifua kikuu umekuwa ugonjwa wa kawaida hivi leo na unapoathiri mtoto mdogo ambaye hajapata chanjo, hatari ya kupata ugonjwa homa ya uti wa mgongo (meningitis) huongezeka. Homa ya uti wa mgongo itamweka mtoto kwenye hatari kubwa ya kupata kifafa. Chanjo nyingine maalumu kwa aina tofauti za homa ya uti wa mgongo zinapatikana hospitalini lakini kwa ada.

Homa ni kitu kinachoongezea hatari ya kupatwa na mshtuko ilhali inaweza kudhibitiwa vyema. Mtoto ambaye homa yake inaruhusiwa kupanda juu yuko katika hatari ya kupatwa na mshtuko. Ni muhimu kwa homa kudhibitiwa vizuri pindi tu inapoanza. Udhibiiti wa homa unajumuisha; kutumia dawa kama Panado (paracetamol) ama Brufen (Ibuprofen), mtoe mtoto nguo kisha umpanguze na kitambaa kilicholoweshwa ndani ya maji yenye joto la kadri na la muhimu zaidi ni kutafuta msaada wa matibabu.

Ulinzi dhidi ya jeraha, haswa jeraha kwenye kichwa ambayo ndiyo sababu nyingine ya kifafa. Ulinzi hutokana na kuhakikisha ya kwamba watoto hawezi kuanguka kwa urahisi kutoka katika sehemu iliyo juu, usimamizi unaofaa wanapocheza na kuweka mbali vitu ambavyo vinaweza kuwaletea madhara wanapocheza. Unaposafiri kwenye gari, ni muhimu kutumia mishipi ya usalama ili kupunguza hatari ya kujeruhiwa ikiwa kutatokea ajali. Jeraha la kichwa ndilo jeraha ambalo hutokea mara kwa mara kukitokea ajali.

Ni wapi naweza kuenda ikiwa sitapata usaidizi?
Kuzirai ambako hakuwezi kudhibitiwa kunaweza kuwa hatari kwa mgonjwa.Huwa hakuwezi kubashiriwa na unaweza kufanyika wakati mgonjwa yuko karibu na moto, anaendesha gari ana jaribu kuvuka barabara, anaogelea ama anafanya kazi akiwa juu (k.m juu ya paa la nyumba). Katika hali hii, kuzirai kutamweka mtu katika hatari kubwa kwani anaweza kuchomeka, kupatwa na ajali, kuzama ama kuanguka na kuumia. Hii ni sababu moja muhimu ambayo inahitaji kifafa kudhibitiwa.

Pili, ugonjwa wa kifafa unaweza kutokea mara kwa mara ukiwa hautadhibitiwa. Kuzimia kunaweza kutokea mara kwa mara na kuonekana ni kama unaendelea. Hii ni dharura ya kimatibabu ambayo inaweza kusababisha kifo katika muda mfupi. Kwa hivyo ikiwa mgonjwa ataathiriwa na kifafa kwa zaidi ya dakika 5, mpeleke katika hospitali iliyo karibu haraka iwezekanavyo kwa sababu kuzimia hakuwezi kuisha bila ya dawa.

Nitapata usaidizi wapi?
Hospitali iliyo karibu nawe itakutolea usaidizi. Watakuwa na dakitari ambaye atakuchunguza na atakushauri kuhusu uchunguzi wowote ama matibabu ambayo unaweza kuhitaji kutumia.

Uongo unaozungumziwa kuhusu Kifafa

"Kifafa ni aina ya ulemavu kwani huathiri utenda kazi wa ubongo"
Ulemavu ulielezewa vizuri na Shirika la Afya Duniani mnamo mwaka wa 1976. Unatofautisha dhana tatu ambazo hutumiwa sana na unadhihirisha baina ya kudhoofika, ulemavu na upungufu.

Kudhoofika ni upungufu wowote ama hali ya akili isiyo ya kawaida (saikolojia), utenda kazi wa mwili (fiziolojia) ama muundo wa mwili wa binadamu (anatomia) ama utenda kazi; Ulemavu ni kikwazo ama kukosa uwezo (unaotokana na upungufu) wa kufanya shughuli kwa njia inayochukuliwa kuwa ya kawaida kwa binadamu; Upungufu ni kasoro inayotokea kwa mtu kwa sababu ya kudhoofika ama ulemavu ambao huzuia kutimilika kwa wajibu unaochukuliwa kuwa wa kawaida (kwa kutegemea umri, jinsia na mambo ya ushirikiano wa jamii na utamaduni) kwa mtu huyo.

Kifafa ni matokeo ya utenda kazi wa ubongo usio wa kawaida ama kudhoofika kwa utenda kazi wa ubongo.Huathiri utenda kazi wa ubongo kwa kuendelea na kuwacha. Kuna hali nyingine ambazo huwa na athari inayoendelea na ya muda mrefu. Hizi hali hutokea kama kutoona vizuri, kutowiiana vizuri,kuongea pole pole,kutoweza kumakinika na kusahausahau. Hali hizi huitwa ulemavu ama taahira ya akili.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kumshika mtu mwenye hali/ulemavu mwingine. Unaweza pia kutokea tu wenyewe. Mgonjwa wa kifafa ambaye yuko chini ya matibabu na anafuatiliwa mara kwa mara anaweza kutimiza majukumu yake kama mtu yeyote mwingine. Katika hali hii hadhaniwi kuwa na ulemavu wowote. Ikiwa kuzirai kunakosababishwa na kifafa kumeongezeka na kunamzuia mtu kufanya kazi yake ya kawaida, basi hili huchukuliwa kuwa ulemavu.

"Kifafa hutokea kwa sababu ya kupagawa na mapepo"
 
Kifafa.jpg

Ndugu zangu katika JF kabla sijaanza kueleza swahibu lililo nisibu ningependa kukumbushia utani nilio uandika katika jukwaa la joke/utani ndani ya post ile nilisema natafu mfanya kazi wandani wa kike (house girl) ile ilikuwa ni utani lakini mpaka ukawa utani kulikuwa na ukweli fulani ndani yake.

Mke wangu alikuwa ananisumbua sana kuhusu kutafuta msaidizi wa kazi za ndani.

Yeye anataka lakini mimi niluwa napinga kutokana na ukweli kwamba familia yetu ni ndogo huku nikijaribu kuangalia majukumu ya huyo msaidizi.

Binafsi nikaona mke wangu anajitengenezea mazingira ya kuja kuonekana hana maana tenda kama msaidizi atafua, kupika,kuosha watoto, kutandika kitanda nk.ndiyo maana nikaandika utani kwamba natafuta msaidizi wa ndani awe mzuri kuliko mke wangu mpole mcheshi na mwenye kujituma awe tayari kufanya kazi yeyote nitakayo mwambia .

Huo ulikuwa utani. Sasa tuje kwenye mada

Baada ya kutafuta mfanyakazi wa ndani hatimae tulifanikiwa kumpata hivi sasa ana wiki. Lakini tangu aanze kazi kufanya amekuwa akisumbuliwa na kichwa.

Lakini leo hii kaanguka na kuanza kutoka mapovu mdomoni nimeshindwa kutambua kama ni majini au kifafa. Lengo la mada hii ni kupata ushauri wenu je?

Nitumie dawa gani au nifanye nini, au nimfukuze kama anavyotaka wife?

Msaada.

BAADHI YA MASWALI YA WADAU
Jana katika safari za huku na kule, nikiwa kwenye daladala kuna mmama mmoja alipatwa na mshtuko na kuanza kutoa mapovu mdomoni, kitu nilichoambiwa na abiria wengine ni kwamba ni mgonjwa wa kifafa, kulikuwa kuna kijana aliyekuwa na huyo mgonjwa alijaribu kumpepea na kumtuliza mgonjwa wake.watu wakawa wanasema akimfuta yale mapovu anaweza kufariki, na yale mapovu yakikupata unaweza ukapata ule ugonjwa.nina maswali kuhusu huu ugonjwa.

1. Je, nini ni source ya huu ugonjwa?
2. Je, unarithika?
3. Kwanini yale mapovu yakifutwa yanaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa?
4. Mtu akipatwa na kifafa anatakiwa apewe first aid gani?
5. Je, ugonjwa huu unatibika?

Naombeni majibu ili nipate ufahamu zaidi.

Ahsanteni
Baada ya miaka 3 ya ndoa, imegundulika kuwa mke wangu ana KIFAFA, nasikia kifafa ni hatari sana kwa wanawake, naomba kujua kuna tiba ya kifafa? kama hakuna natakiwa kufanya nini kuhusu ndoa yangu changa? Ushauri plzeeeeee
Habari wanaJF,

Nina rafiki yangu wa karibu anaumwa ugonjwa wa kuanguka, yaani kifafa kwa muda mrefu sasa ameangaika hospitalini mpaka kwa wanganga wa kienyeji na kutumia dawa mbalimbali bila mafanikio.

Tafadhali mwenye kujua lolote kuhisiana na tiba naomba anijuze ili tumsaidie ndugu yetu huyu jamani. Maoni, mawazo, ushauri na lolote ujualo unakaribishwa.

Asante sana
Habari zenu wadau, huduma ya kwanza kwa mtu mwenye Ugonjwa wa Kifafa ni nini? pia Ugonjwa wa Kifafa unaambukizwa kwa njia zipi?
Wanajamvi naomba msaada wenu kwa mtu yeyote anayefahamu dawa ya mtu mwenye kifafa, maana hali hii imenitokea ghafla kwa mara ya kwanza mwaka jana kwa kupoteza fahamu kwa muda usiozidi nusu saa. Nimejaribu kwenda hospitali na kufanya vipimo mbalimbali kama MRI na CT-Scan lakini vyote vinaonyesha nipo sawa.

Nilipewa dawa na Prof. Matuje, neurologist nikatumia kwa muda wa mwezi mzima lakini ile hali imeendelea kunitokea na mpaka hivi sasa ninavyoandika hali hiyo imenitokea jumamosi. Kwa sasa nipo above 29years old.

NINAOMBA SANA MSAADA WENU WA USHAURI AU ANAYEJUA TIBA YA HIKI KIFAFA CHA UKUBWANI.NAPATA SHIDA SHANA NDUGU ZANGU.

BAADHI YA MICHANGO YA WADAU
UGONJWA WA KIFAFA NI NINI?

Huu ni ugonjwa amabao unasabababishwa na seli za mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara.

Ifahamike kuwa, aina ya kifafa inayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakakamaa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakakamai wala kupoteza fahamu, kama tutakavyoona hapo baadae.

Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika.

Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu…

Chanzo cha ugonjwa huu ni nini?

chanzo kikuu cha ugonjwa huukwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ni moja ya sababu za kuugia kifafa.

Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu.

Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa.

Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis.

Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo kama kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa.

Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa baadae.

Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mototo huzaliwa kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia utotoni.

Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa akizaliwa.

Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.

Kuna aina mbili kubwa za kifafa…

1) Primary generalized seizures

Hii ndio aina ya kifafa ambayo inafahamika sana mitaani; na inahusisha mgonjwa kukamaa, na kupoteza fahamu, pamoja na dalili zingine kama vile kutoa povu mdomoni, na kujisaidia haja kubwa na/au ndogo bila kujitambua akishikwa na hali hiyo.

Pia wengine hupatwa kama na wazimu au kuchanganyikiwa kwa muda kabla au baada ya kushikwa na hali hiyo.

2) Partial seizures

Aina hii ya kifafa ni ile ambayo haihusishi muhusika kupoteza fahamu na kukakamaa!! Bali hushikwa na hali fulani kama ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa; Wengine huwa na dalili zisizoeleweka za mara kwa mara kama vile kusihiwa nguvu, kizungu zungu, kichwa kuuma sana (bila sababu ya kiafya inayojulikana), na kadhalika. Aina hizi za kifafa ziko nyingi, na dalili hutofautiana kwa kadri ya aina ya kifafa!!

Vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa

Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa daktari kuchukua historia ya dalili zinazomkabili muhusika tu(hakuna kipimo ambacho kinaweza kutambua kifafa kwa asilimia 100); Kuna kipimo kinachopima jinsi ubongo unavyotoa taarifa za umeme (ELECTROENCEPHALOGRAM-EEG), ambacho kinaweza kutambua kifafa, lakini kipimo hiki kinaweza kikaonekana kuwa hakina shida, na bado mtu akawa na tatizo hilo la kifafa. Hivyo basi, kifafa ni moja kati ya magonjwa machache ambayo kutambulika kwake kunategemea sana ujuzi na utaalamu wa daktari katika kuunganisha dalili za mgonjwa kuliko vipimo!!

Hata hivyo, mara nyingi nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa, mfano:
  • Uwezo wa kufanya kazi figo
  • Uwezo wa kufanya kazi maini
  • Kupima maji ya uti wa mgongo
  • Kupima Kaswende
  • Picha ya ubongo mfano CT SCAN..
Matibabu

Kama kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa huanzishiwa matibabu lakini kama mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa.

Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa, USIMALIZE FEDHA ZAKO KWA WAGANGA WA KIENYEJI naomba nisisitize hili, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa fuata utaratibu wa matibabu yaani kumeza dawa siku zote za maisha yako na kufuata baadhi ya masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.

Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amekamatwa na kifafa:{non pharmacological treatment}
  • Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake kama kisu, sindano au vyuma.
  • Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa.
  • Usimshike kuzuia mizunguko yake
  • Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni.
  • Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe
  • Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa kama dawa au chakula mpaka apate fahamu zake.
Mtu mwenye kifafa hali hii ya kukamatwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona dalili hizi mkimbize hospitali.
  • Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi
  • Kutapika sana
  • Kushindwa kuona vizuri
  • Kupoteza fahamu
  • Kichwa kuuma sana.
Matibabu ya dawa

Mgonjwa akishagundulika na kifafa ataanzishiwa dawa kama carbamizapine, phenorbabitone au zingine za kifafa na atakua anameza kila siku ili kuzuia hali hiyo ya kuanguka na kuoteza fahamu na akifuata masharti ataishi maisha ya kawaida kabisa.

Mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara..
  • Kukosa usingizi kwa muda mrefu
  • Mianga na miale ya disco
  • Unywaji wa pombe
  • Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali.
  • Kutomeza dawa kama ilivyoelekezwa.
KIFAFA SI UGONJWA WA KUAMBUKIZA

Kifafa (Epilepsy) kinatokea kunapokuwa na mapungufu katika seli za ubongo. Ubongo unafanya kazi katika mfumo wa umeme au kama umeme hivi, sasa kunapokuwa na hitilafu katika huu mfumo ndio kifafa kinaweza kutokea ambacho dalili zake ni kuona maluwe luwe (aura), kiasha kupoteza fahamu, kuanguka na kutupa miguu na/au mikono, kukaza mdomo, kutoa povu na huwa inamalizia na kutoa haja ndogo au kubwa wakati mwingine.

Kifafa sio ugonjwa wa kuambukiza, mara nyingi unakuwa kwenye familia kwa kurithi toka kwa mzazi/wazazi, lakini pia wakati mwingine inaweza tokea baada ya kuumia ubongo kutokana na ajali, kiharusi (stroke), kuumia wakati wa kuzaliwa (birth injuries) etc...Kifafa hiki ni tofauti na 'dege dege' kwa watoto au kifafa cha mimba (Eclampsia).

Kifafa hakitibiki, nikiwa na maana hakitibiwi kikapona kabisa, ila kuna dawa za kupunguza au kuzuia kifafa kutokea mara kwa mara. dawa hizi zinapatikana hospitali, na mgonjwa atakunywa kwa maisha yake yote dozi inategemea na hali ya mgonjwa anapoonwa mara kwa mara kwenye kliniki zao maalum. Kwa sababu kifafa hutokea ghafla, ni muhimu sana mgonjwa anapoanguka utoe vitu vyote vya hatari vyenye kuumiza (watu wengi hukimbilia kumtoa mgonjwa au kumshika na pengine hata kumfunga kamba, hii si sahihi, inatakiwa utoe vitu vitakavyohatarisha mgonjwa kuumia au hata kufa) mfano moto, jiko, vifaa vyenye ncha kali etc. Kuna wagonjwa wengine huwa wanashtukia kifafa kinapoanza (aura) hivyo kujiepusha na sehemu za hatari.

Baada ya kuanguka kifafa, mgonjwa anaweza akawa kama hana fahamu sawa sawa, amechanganyikiwa au hata kama kichaa...mara nyingi anahitaji msaada badala ya kumnyanyapaa. Siwezi kukushauri umtimue au usimtimue housegirl wako sababu sijui kwa nini wataka kufanya hivyo, kama unaogopa kuwa atawaambukiza, si kweli...kifafa hakiambukizi, kama unaogopa majukumu ya kumlea mgonjwa wa kifafa, lakini kama una moyo wa kumsadia, mpeleke Muhimbili pale Idara ya magonjwa ya akili kuna wataalamu waliobobea, na kuna kliniki maalum kwa ajili ya wagonjwa wa kifafa atapata msaada unaostahiki na maisha yake yataboreka kadri amabavyo zile attacks za kifafa zinapungua.
EPILEPSY IS A BRAIN DISORDER

Epilepsy (kifafa) is a brain disorder that causes people to have recurring seizures (ile mitetemeko yake). The seizures happen when clusters of nerve cells, or neurons, in the brain send out the wrong signals. People may have strange sensations and emotions or behave strangely. They may have violent muscle spasms or lose consciousness. yale mate/ute unaotoka ni kwa sababu koo pamoja na organs zingine zimepata the wrong signals, hakuna cha issue ya kuukata unakufa,ni imani tu.

Epilepsy has many possible causes, including illness, brain injury and abnormal brain development. In many cases, the cause is unknown.

Doctors use brain scans and other tests to diagnose epilepsy. It is important to start treatment right away. There is no cure for epilepsy, but medicines can control seizures for most people. When medicines are not working well, surgery or implanted devices such as vagus nerve stimulators may help. Special diets can help some children with epilepsy.
KIFAFA NI UGONJWA WA UBONGO

Ubongo wa binadamu una mabilioni ya seli za neva.Zinashirikiana na kila moja kupitia chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima.Wakati baadhi ya ama hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na husababisha kifafa ama kuzirai.

Kuzirai kwa ghafla huathiri vile ubongo hufanya kazi.Kunaweza kumsababisha mtu kupata mabadiliko ya ghafla katika fahamu, mwendo ama hisia.

Mshtuko wa moyo mmoja haumanishi ya kwamba mtoto ana kifafa.Kuzirai mara moja kunaweza kutokea kwa sababu tofauti k.m homa, jeraha la kichwa, kiwango cha chini cha sukari katika damu na kadhalika.

Kifafa ni jina la kuzirai kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu ya kutibiwa inayojulikana.

Katika sehemu hii jifundishe zaidi kuhusu huu ugonjwa.

Dalili na ishara za kifafa

Nitajuaje ikiwa niimeathiriwa na kifafa?
Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya mda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa mda baada ya kuzirai.

Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa zingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.

Katika aina zingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.

Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.

Je, kila mtu anayeathiriwa na kifafa anapaswa kupelekwa hospitalini?

La. Sio kila mtu anayeathirika na kifafa anapaswa kupatiwa huduma ya matibabu. Mtu mwenye kifafa ambaye yuko chini ya matibabu labda hahitaji kupelekwa hospitalini mara moja. Kuna visa vingine ambavyo ni muhimu kumpeleka mtu hospitalini kama dharura.
  • Kuzirai mara ya kwanza. Ikiwa mtu anafahamika ya kwamba huwa hana kifafa na kishe azirai, mtu huyu anahitaji kumuona dakitari mara moja.
  • Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa hospitalini.Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili kuokoa maisha yake.
  • Ikiwa kupumua hakurudii hali ya kawaida baada ya kuzirai.
  • Ikiwa kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo Kabla ya mgonjwa kupata nafuu. Nitaendelea hii Topic
JE, KUNA TIBA YA KIFAFA?

Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali zingine kama vile uvimbe kwenye ubongo ,ugonjwa wa figo au ugonjwa wa ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa mda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.

Jinsi nyingine za kudhibiti kifafa

Kando na madawa, ni nini kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?

Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata amedhibitiwa na matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8 ilhali mtoto anahitaji angalau masaa 9) kunaweza kusababisha mshtuko wa kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia kusababisha shambulizi. Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya

kutokea kwa mshtuko wa kifafa. Taa zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa katika watu wengine. Kupumua kwa nguvu wakati unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara katika watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa unaweza kuepuka haya, unaweza kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.

Kwa nini haupaswi kumwekea mtu kitu mdomoni anaposhikwa na mshtuko wa kifafa?

Kwa mda mrefu iliaminika ya kwamba wakati mtu ameshikwa na kifafa, mgonjwa anaweza kumeza ama hata kunyongwa na ulimi wake na kwa hivyo kusababisha kifo. Hivi sasa hali imebadilika na inaeleweka ya kwamba hakuna haja ya kuweka kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na kifafa. Hili linaweza kusababisha madhara zaidi.

Wakati wa kifafa kuna mshtuko wa ghafla wa misuli.Mikono, miguu na sehemu zingine za mwili huwa na mwendo wa kujirudia rudia ambao ni vigumu kuukabili kwa kutumia nguvu haswa ikiwa mgonjwa ni mkubwa kwa umbo. Kama sehemu ya tendo la misuli, mgonjwa husaga meno yake kwa sababu ya tendo la nguuvu katika taya. Jaribio lolote la kuweka kitu kwenye mdomo linaweza kusababisha kuvunjika kwa meno ya mgonjwa, kunyongwa na kile kilichowekwa mdomoni ama mgonjwa kumuuma vibaya mhudumu wake.

Kwa hivyo fahamu: USIWEKE kitu katika mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na mshtuko wa kifafa.

Kwa nini wagonjwa wa kifafa hawawezi kugawana madawa yao?

Madawa ya kifafa hufanya kazi ya kukomesha shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo. Kuna aina nyingi za kuzirai katika kifafa na hizi zote huitikia kwa njia tofauti kwa madawa tofauti. Hii ndio sababu ya kwanza kwa nini haufai kugawa dawa za kifafa. Dawa ambazo hudhibiti aina moja ya kifafa zinaweza kukosa athari kwa aina nyingine ya kifafa.

Pili, watu tofauti wanahitaji vipimo tofauti vya dawa iliyotolewa kudhibiti kifafa. Ugonjwa wa kifafa unamaanisha ya kwamba ubongo wa mtu unaweza kufyatuka kwa njia isiyo ya kawaida. Watu tofauti hupata kifafa katika viwango tofauti vya mchangamsho wa ubongo. Watu wengine huchangamshwa kwa urahisi na kuzirai ilhali wengine hawachangamshwi kwa urahisi. Kipimo cha dawa kinachotumiwa kumdhibiti mtu ambaye huzirai kwa urahisi ni tofauti na kile cha yule ambaye hazirai kwa urahisi.

Tatu, sio vizuri kugawana madawa ambayo yametolewa kufuatia maagizo ya dakitari. Maagizo ya dakitari hutoa dawa kwa mtu mmoja kwa kipindi maalumu cha wakati. Kwa kugawana madawa, mtu ambaye alipewa maagizo ya dakitari ataishiwa na dawa kabla ya ahadi ya kuonana na dakitari inayofuatia. Wanweza kuzirai kwa urahisi kwa sababu hawako kwenye matibabu. Sio salama kwa mtu mwenye kifafa kugawa dawa zake.
KUNA MATATIZO YANAYOWEZA KUTOKEA WAKATI WA MATIBABU?

Je, kuna jambo ambalo linaweza kuenda mrama nikiwa bado kwenye matibabu?

Athari ya matibabu ni hisia ya kusinzia na kutokuwa mwepesi ambako hutoweka baada ya mda. Baadhi ya madawa yanaweza kumfanya mgonjwa aongeze uzito. Athari mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea ni kwenye ini. Hili ni jambo la kawaida wakati mgonjwa anatumia madawa kadhaa ili adhibiti kifafa.

Unapoanza matibabu, athari yake kwa kifafa huwa siio ya papo kwa hapo. Inachukua angalau mwezi mmoja kuona athari yoyote ya kudumu na mtu anahitajiwa kuwa mvumilivu. Katika visa vichache, visa vya kuzirai vinaweza kuongezeka unapowekwa kwenye matibabu kabla kuzirai hakujapungua.

Ni kipi kipimo cha dawa za kutibu kifafa?

Kipimo cha dawa ni kile ambacho kitatibu kitadhibiti ama kitatibu hali hii bila ya kusababisha mathara mabaya ya kando. Hii hutofautiana kutoka kwa matibabu hadi matibabu na hali hadi hali. Dawa zingine kama Panadol zina kiwango chake rasmi; watu wazima humeza vidonge 2 kila masaa 6-8. Hali zingine kama malaria isiyo kali zina kiwango cha dawa kinachopeanwa katika kiwango cha kipimo cha dawa kama watu wazima humeza vidonge 2 vya Camoquine mara moja kwa siku 3.

Hesabu ya kiwango cha kipimo cha dawa hutegemea uzani wa mgonjwa ama umri wake. Kila aina ya dawa ina kipimo kwa uzani ama umri wa mgonjwa uliopeanwa.

Katika visa vingine vya kifafa, kiwango cha dawa hakiwezi kuhesabika kwa urahisi. Matibabu yanayotolewa ili kudhibiti kifafa huathiriwa kwa urahisi na vipimo vya dawa na hufanya kazi katika kadiri ndogo. Dawa kidogo kwenye damu ama dawa nyingi kwenye damu na udhibiti wa kifafa hupotezwa. Kwa hivyo kila dawa inaweza tu kutumiwa katika kadiri iliyotolewa ya kipimo cha dawa. Ikiwa kuzirai hakuwezi kudhibitiwa katika kadiri hii,dawa ya pili na saa zingine dawa ya tatu inaweza kuongezwa. Hii nyongeza ya madawa hujiathiri na kipimo cha kila dawa kinahitaji kuhesabiwa mara tena ili kila dawa ikuwe katika kiwango kinachofaa katika damu.

Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, kutokea kwa kifafa hakuwezi kutabirika katika watu tofauti. Kuna wale ambao ugonjwa wao wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ilhali wengine wanahitaji matibabu 2-3 ili kupunguza visa vya kuzirai bila ya kuvimaliza kabisa. Kwa wagonjwa 2 wenye umri sawa na uzani sawa, matibabu ya kipekee yanaweza kutolewa katika vipimo tofauti ili kudhibiti kuzirai kwao.

Ni kwa mda upi ambao mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia dawa?

Mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia madawa aliyopewa hadi ashauriwe vingine. Kwa kutegemea wingi wa kutokea kwa visa vya kifafa, wagonjwa wanaweza kutumia dawa kwa maisha yao yote.Katika watoto,hata hivyo mambo yanabadilika. Kitambo, ilichukuliwa ya kwamba mtoto mwenye kifafa angehitajika kutumia

madawa kwa miaka mingi ya maisha yake. Lakini hali sio hivyo tena. Ikiwa mtoto anatumia madawa kwa njia inayofaa na kwa wakati bila ya kukosa hata kipimo.cha dawa na anabakia bila kifafa kwa angalau miaka 2, basi dakitari anaweza kufikiria kusimamisha utumizi wa madawa. Ni dakitari pekee yake anayeweza kutoa ushauri kuhusu kusimamaisha matumizi ya madawa ya kifafa baada ya kumfuatilia mgonjwa kwa

kipindi fulani cha mda. Ni muhimu maamuzi haya yafanywe na dakitari, kwa sababu mwanzo utumizi wa madawa umeanza haufai kukatizwa kwa ghafla. Badala yake dakitari atapunguza kipimo cha dawa pole pole hadi matumizi ya dawa umesitishwa. Ukisitisha dawa kwa ghafla, kuna madhara ya kando kama kumwa na tumbo, kutapika na kutomakinika na kuzirai kunaweza kujirudia.

Kwa hivyo, jambo muhimu ni kuzungumza na dakitari wako kuhusu kusimamisha matibabu. Ikiwa mtoto hajafuzu kwa ajili ya kusitishwa matibabu kwa sasa, na kisha aendele kutokana na ushauri wa dakitari. Ikiwa mtoto atafuzu, basi hili linafaa kufanywa kwa utaratibu. Wakati kipimo cha dawa kinapunguzwa, ni muhimu kukumbuka ya kwamba mtoto anaweza kushikwa na kifafa. Waweke wakiwa salama na waangalie kwa karibu hadi dawa zote zimesitishwa kabisa na kila kitu kiko salama.
JE, KUNA TIBA YA KIFAFA?

Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali zingine kama vile uvimbe kwenye ubongo ,ugonjwa wa figo au ugonjwa wa ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa mda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.
DALILI ZA KIFAFA

Nitajuaje ikiwa niimeathiriwa na kifafa?
Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika

kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya mda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa mda baada ya kuzirai.

Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa zingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.

Katika aina zingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.

Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.

Je, kuna tiba ya kifafa?

Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali zingine kama vile uvimbe kwenye ubongo ,ugonjwa wa figo au ugonjwa wa ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa mda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.

Jinsi nyingine za kudhibiti kifafa

Kando na madawa, ni nini kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?

Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata amedhibitiwa na matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8 ilhali mtoto anahitaji angalau masaa 9) kunaweza kusababisha mshtuko wa

kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia kusababisha shambulizi. Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya kutokea kwa mshtuko wa kifafa. Taa zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa

katika watu wengine. Kupumua kwa nguvu wakati unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara katika watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa unaweza kuepuka haya, unaweza kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.

Kwa nini haupaswi kumwekea mtu kitu mdomoni anaposhikwa na mshtuko wa kifafa?

Kwa mda mrefu iliaminika ya kwamba wakati mtu ameshikwa na kifafa, mgonjwa anaweza kumeza ama hata kunyongwa na ulimi wake na kwa hivyo kusababisha kifo. Hivi sasa hali imebadilika na inaeleweka ya kwamba hakuna haja ya kuweka kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na kifafa. Hili linaweza kusababisha madhara zaidi.

Wakati wa kifafa kuna mshtuko wa ghafla wa misuli.Mikono, miguu na sehemu zingine za mwili huwa na mwendo wa kujirudia rudia ambao ni vigumu kuukabili kwa kutumia nguvu haswa ikiwa mgonjwa ni mkubwa kwa umbo. Kama sehemu ya tendo la misuli, mgonjwa husaga meno yake kwa sababu ya tendo la nguuvu katika taya. Jaribio lolote la kuweka kitu kwenye mdomo linaweza kusababisha kuvunjika kwa meno ya mgonjwa, kunyongwa na kile kilichowekwa mdomoni ama mgonjwa kumuuma vibaya mhudumu wake.

Kwa hivyo fahamu: USIWEKE kitu katika mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na mshtuko wa kifafa.
UFAHAMU UGONJWA WA KIFAFA NA TIBA YAKE

Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara.

Ifahamike kuwa, aina ya kifafainayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakakamaa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakakamai wala kupoteza fahamu, kama tutakavyoona hapo baadae.

Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika.

Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu.

Chanzo cha ugonjwa wa kifafa ni nini?
Chanzo kikuu cha ugonjwa huu kwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ya hiz ni moja ya sababu za kuugua kifafa.

Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu.

Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa.

Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis.

Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo kama kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa.

Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa baadae.

Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mtoto huzaliwa kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia utotoni.

Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa akizaliwa.

Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.

Kuna aina mbili kubwa za kifafa

1) Primarymary generalized seizures
Hii ndio aina ya kifafa ambayo inafahamika sana mitaani; na inahusisha mgonjwa kukamaa, na kupoteza fahamu, pamoja na dalili zingine kama vile kutoa povu mdomoni, na kujisaidia haja kubwa na/au ndogo bila kujitambua akishikwa na hali hiyo.

Pia wengine hupatwa kama na wazimu au kuchanganyikiwa kwa muda kabla au baada ya kushikwa na hali hiyo.

2) Partial seizures
Aina hii ya kifafa ni ile ambayo haihusishi muhusika kupoteza fahamu na kukakamaa!! Bali hushikwa na hali fulani kama ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa; Wengine huwa na dalili zisizoeleweka za mara kwa mara kama vile kusihiwa nguvu, kizungu zungu, kichwa kuuma sana (bila sababu ya kiafya inayojulikana), na kadhalika. Aina hizi za kifafa ziko nyingi, na dalili hutofautiana kwa kadri ya aina ya kifafa!!

Vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa.

Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa daktari kuchukua historia ya dalili zinazomkabili muhusika tu(hakuna kipimo ambacho kinaweza kutambua kifafa kwa asilimia 100); Kuna kipimo kinachopima jinsi ubongo unavyotoa taarifa za umeme (ELECTROENCEPHALOGRAM-EEG), ambacho kinaweza kutambua kifafa, lakini kipimo hiki kinaweza kikaonekana kuwa hakina shida, na bado mtu akawa na tatizo hilo la kifafa. Hivyo basi, kifafa ni moja kati ya magonjwa machache ambayo kutambulika kwake kunategemea sana ujuzi na utaalamu wa daktari katika kuunganisha dalili za mgonjwa kuliko vipimo!!

Hata hivyo, mara nyingi nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa… mfano

• Uwezo wa kufanya kazi figo
• Uwezo wa kufanya kazi maini
• Kupima maji ya uti wa mgongo
• Kupima Kaswende
• Picha ya ubongo mfano CT SCAN.

Mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara.
• Kukosa usingizi kwa muda mrefu
• Mianga na miale ya disko
• Unywaji wa pombe
• Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali.
• Kutomeza dawa kama ilivyoelekezwa

Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amekamatwa na kifafa:{non pharmacological treatment}yaani HUDUMA YA KWANZA
• Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake kama kisu, sindano au vyuma.
• Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa.
• Usimshike kuzuia mizunguko yake
• Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni.
• Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe
• Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa kama dawa au chakula mpaka apate fahamu zake.

Mtu mwenye kifafa hali hii ya kukamatwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona dalili hizi mkimbize hospitali..
• Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi
• Kutapika sana
• Kushindwa kuona vizuri
• Kupoteza fahamu
• Kichwa kuuma sana.

MATIBABU YA UGONJWA
Kama kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa huanzishiwa matibabu lakini kama mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa.

Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa kwa 100% hospitali, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa basi utapewa utaratibu wa matibabu yaani kumeza dawa sik u zote za maisha yako na kufuata baadhi ya masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.
UFAHAMU UGONJWA WA KIFAFA NA TIBA YAKE

Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara.

Ifahamike kuwa, aina ya kifafainayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakakamaa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakakamai wala kupoteza fahamu, kama tutakavyoona hapo baadae.

Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika.

Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu…

Chanzo cha ugonjwa wa kifafa ni nini?

chanzo kikuu cha ugonjwa huu kwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ya hiz ni moja ya sababu za kuugua kifafa.

Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu.

Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa.

Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis.

Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo kama kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa.

Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa baadae.

Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mtoto huzaliwa kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia utotoni.

Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa akizaliwa.

Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.

Kuna aina mbili kubwa za kifafa…

1)Primarymarygeneralized seizures

Hii ndio aina ya kifafa ambayo inafahamika sana mitaani; na inahusisha mgonjwa kukamaa, na kupoteza fahamu, pamoja na dalili zingine kama vile kutoa povu mdomoni, na kujisaidia haja kubwa na/au ndogo bila kujitambua akishikwa na hali hiyo.

Pia wengine hupatwa kama na wazimu au kuchanganyikiwa kwa muda kabla au baada ya kushikwa na hali hiyo.

2)Partial seizures

Aina hii ya kifafa ni ile ambayo haihusishi muhusika kupoteza fahamu na kukakamaa!! Bali hushikwa na hali fulani kama ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa; Wengine huwa na dalili zisizoeleweka za mara kwa mara kama vile kusihiwa nguvu, kizungu zungu, kichwa kuuma sana (bila sababu ya kiafya inayojulikana), na kadhalika. Aina hizi za kifafa ziko nyingi, na dalili hutofautiana kwa kadri ya aina ya kifafa!!

Vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa

Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa daktari kuchukua historia ya dalili zinazomkabili muhusika tu(hakuna kipimo ambacho kinaweza kutambua kifafa kwa asilimia 100); Kuna kipimo kinachopima jinsi ubongo unavyotoa taarifa za umeme (ELECTROENCEPHALOGRAM-EEG), ambacho kinaweza kutambua kifafa, lakini kipimo hiki kinaweza kikaonekana kuwa hakina shida, na bado mtu akawa na tatizo hilo la kifafa. Hivyo basi, kifafa ni moja kati ya magonjwa machache ambayo kutambulika kwake kunategemea sana ujuzi na utaalamu wa daktari katika kuunganisha dalili za mgonjwa kuliko vipimo!!

Hata hivyo, mara nyingi nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa… mfano

• Uwezo wa kufanya kazi figo

• Uwezo wa kufanya kazi maini

• Kupima maji ya uti wa mgongo

• Kupima Kaswende

• Picha ya ubongo mfano CT SCAN.

mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara..

• Kukosa usingizi kwa muda mrefu

• Mianga na miale ya disko

• Unywaji wa pombe

• Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali.

• Kutomeza dawa kama ilivyoelekezwa

Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amekamatwa na kifafa:{non pharmacological treatment}yaani HUDUMA YA KWANZA

• Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake kama kisu, sindano au vyuma.

• Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa.

• Usimshike kuzuia mizunguko yake

• Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni.

• Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe

• Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa kama dawa au chakula mpaka apate fahamu zake.

Mtu mwenye kifafa hali hii ya kukamatwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona dalili hizi mkimbize hospitali..

• Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi

• Kutapika sana

• Kushindwa kuona vizuri

• Kupoteza fahamu

• Kichwa kuuma sana.

MATIBABU YA UGONJWA
Kama kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa huanzishiwa matibabu lakini kama mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa.

Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa kwa 100% hospitali, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa basi utapewa utaratibu wa matibabu yaani kumeza dawa siku zote za maisha yako na kufuata baadhi ya masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.

ukitaka dawa asili ya kupona kabisa kifafa wasiliana nami

Kifafa (Epilepsy) kinatokea kunapokuwa na mapungufu katika seli za ubongo. Ubongo unafanya kazi katika mfumo wa umeme au kama umeme hivi, sasa kunapokuwa na hitilafu katika huu mfumo ndio kifafa kinaweza kutokea ambacho dalili zake ni kuona maluwe luwe (aura), kiasha kupoteza fahamu, kuanguka na kutupa miguu na/au mikono, kukaza mdomo, kutoa povu na huwa inamalizia na kutoa haja ndogo au kubwa wakati mwingine.

Kifafa sio ugonjwa wa kuambukiza, mara nyingi unakuwa kwenye familia kwa kurithi toka kwa mzazi/wazazi, lakini pia wakati mwingine inaweza tokea baada ya kuumia ubongo kutokana na ajali, kiharusi (stroke), kuumia wakati wa kuzaliwa (birth injuries) etc. Kifafa hiki ni tofauti na 'dege dege' kwa watoto au kifafa cha mimba (Eclampsia).

Kifafa hakitibiki, nikiwa na maana hakitibiwi kikapona kabisa, ila kuna dawa za kupunguza au kuzuia kifafa kutokea mara kwa mara. dawa hizi zinapatikana hospitali, na mgonjwa atakunywa kwa maisha yake yote dozi inategemea na hali ya mgonjwa anapoonwa mara kwa mara kwenye kliniki zao maalum. Kwa sababu kifafa hutokea ghafla, ni muhimu sana mgonjwa anapoanguka utoe vitu vyote vya hatari vyenye kuumiza (watu wengi hukimbilia kumtoa mgonjwa au kumshika na pengine hata kumfunga kamba, hii si sahihi, inatakiwa utoe vitu vitakavyohatarisha mgonjwa kuumia au hata kufa) mfano moto, jiko, vifaa vyenye ncha kali etc. Kuna wagonjwa wengine huwa wanashtukia kifafa kinapoanza (aura) hivyo kujiepusha na sehemu za hatari.

Baada ya kuanguka kifafa, mgonjwa anaweza akawa kama hana fahamu sawa sawa, amechanganyikiwa au hata kama kichaa. Mara nyingi anahitaji msaada badala ya kumnyanyapaa. Siwezi kukushauri umtimue au usimtimue housegirl wako sababu sijui kwa nini wataka kufanya hivyo, kama unaogopa kuwa atawaambukiza, si kweli. Kifafa hakiambukizi, kama unaogopa majukumu ya kumlea mgonjwa wa kifafa, lakini kama una moyo wa kumsadia, mpeleke Muhimbili pale Idara ya magonjwa ya akili kuna wataalamu waliobobea, na kuna kliniki maalum kwa ajili ya wagonjwa wa kifafa atapata msaada unaostahiki na maisha yake yataboreka kadri amabavyo zile attacks za kifafa zinapungua.
 
Kama unaogopa kuwa atawaambukiza, si kweli kifafa hakiambukizi, kama unaogopa majukumu ya kumlea mgonjwa wa kifafa. Binafsi siogopi chochote ndio maana nimeomba msaada.najua namna gani mgonjwa ambavyo hujisikia vibaya anapo hisi kutengwa na jamii kuhusiana na ugonjwa wake, ila baada kukaanae kanambia aliwahi kupewa mawani japo nimeshindwa kuoanisha tatizo lake na kuvaa miwani.
 
Kama unaogopa kuwa atawaambukiza, si kweli. Kifafa hakiambukizi, kama unaogopa majukumu ya kumlea mgonjwa wa kifafa. Binafsi siogopi chochote ndio maana nimeomba msaada.najua namna gani mgonjwa ambavyo hujisikia vibaya anapo hisi kutengwa na jamii kuhusiana na ugonjwa wake.ila baada kukaanae kanambia aliwahi kupewa mawani japo nimeshindwa kuoanisha tatizo lake na kuvaa miwani.

Miwani haijawahi kuhusika na tiba ya kifafa, wala kifafa hakiharibu macho kiasi cha kuhitaji miwani. Nadhani nia matatizo ma2 tofauti. Ila ni vizuri pia ukamuuliza kama alishawahi kuwa na tatizo hilo la kuanguka anguaka kifafa huko nyuma (kama hajawahi na imeanza ghafla sasa basi atahitaji uchunguzi zaidi), na kama alishawahi kupata matibabu na kuhudhuria kliniki za kifafa.
 
Miwani haijawahi kuhusika na tiba ya kifafa, wala kifafa hakiharibu macho kiasi cha kuhitaji miwani...nadhani nia matatizo ma2 tofauti. Ila ni vizuri pia ukamuuliza kama alishawahi kuwa na tatizo hilo la kuanguka anguaka kifafa huko nyuma (kama hajawahi na imeanza ghafla sasa basi atahitaji uchunguzi zaidi), na kama alishawahi kupata matibabu na kuhudhuria kliniki za kifafa.

Riwa, huyu dada anaamini yaye tangu zamani ni kuugua kichwa na hiyo mawani anadai ma dr wa mwananyamala walimpa ila alipoenda muhimbili walimkataza kuvaa.
 
Miwani haijawahi kuhusika na tiba ya kifafa, wala kifafa hakiharibu macho kiasi cha kuhitaji miwani...nadhani nia matatizo ma2 tofauti. Ila ni vizuri pia ukamuuliza kama alishawahi kuwa na tatizo hilo la kuanguka anguaka kifafa huko nyuma (kama hajawahi na imeanza ghafla sasa basi atahitaji uchunguzi zaidi), na kama alishawahi kupata matibabu na kuhudhuria kliniki za kifafa.

Mkuu maelezo yako ni sahihi ila tu labda niongeze. Kuna baadhi ya wagonjwa wa kifafa hupata tabu sana na mwanga mkali (Photo sensitive epilepsy), hasa kama flash za camera, au mionzi ya jua inapokua reflected; hawa wakitumia miwani inayo block polarised light inaweza punguza incidences za epileptic fits!
 
Mkuu maelezo yako ni sahihi ila tu labda niongeze. Kuna baadhi ya wagonjwa wa kifafa hupata tabu sana na mwanga mkali (Photo sensitive epilepsy), hasa kama flash za camera, au mionzi ya jua inapokua reflected; hawa wakitumia miwani inayo block polarised light inaweza punguza incidences za epileptic fits!!

Naanza kupata picha.
 
Ahasante sana Riwa. Lakini umeelezea GRAND MAL peke yake. Elezea na PETIT MAL pia maana zote mbili ni kifafa.
 
Nakubaliana na maelezo yaliyotolewa na Riwa. mimi mtoto wangu ana kifafa kilichosababishwa na ubongo kujaa maji kulikotokana na kutotibiwa kwa wakati homa ya uti wa mgongo (meningitis).

Kichwa kilianza kuwa kikubwa kwa sababu ya maji ambayo huzalishwa na ubongo wenyewe ili kujisafisha. Katika hali ya kawaida maji hayo hutoka kwa kupitia njia ya uti wa mgongo; lakini kwa mtoto wangu mirija ya uti wa mgongo ya kupitishia maji hayo iliziba ikiwa ni katika harakati za mwili kuzuia wadudu wa homa ya uti wa mgongo kuingia kwenye ubongo.

Alikaa muhimbili kwa miezi saba na kwakuwa ni vigumu kufanya operation ya uti wa mgongo waliamua kumuwekea shunt. Hii ni tube ndogo iliyoshonewa karibu kabisa na ubongo na inateremka hadi tumboni ambako maji yanayozidi kwenye ubongo hupelekwa kupitia tube hiyo (iko ndani kwa ndani).

Alipata tatizo hilo akiwa na umri wa miezi 8, sasa ana miaka 6. Amekuwa akipata kifafa kwa sababu hiyo. Ni kweli basi kuwa kifafa hakiambukizi na si vizuri kumnyanyapaa mgonjwa. Ugonjwa hauna dawa za kitaalamu, zilizopo ni za kutuliza tu.

Lakini kuna dawa za kienyeji ambazo zinasaidia zadi kuliko za hospitali. Nakushauri kwa sasa mpeleke kwa babu wa Loliondo; mimi wangu nimeshampeleka, nimetoka huko wiki iliyopita hivyo ni mapema kujua kama amepona au la. Baada ya miezi miwili nitakuwa na la kusema; ila nina imani atakuwa amepona!
 
Nakubaliana na maelezo yaliyotolewa na Riwa. mimi mtoto wangu ana kifafa kilichosababishwa na ubongo kujaa maji kulikotokana na kutotibiwa kwa wakati homa ya uti wa mgongo (meningitis). Kichwa kilianza kuwa kikubwa kwa sababu ya maji ambayo huzalishwa na ubongo wenyewe ili kujisafisha.

Katika hali ya kawaida maji hayo hutoka kwa kupitia njia ya uti wa mgongo; lakini kwa mtoto wangu mirija ya uti wa mgongo ya kupitishia maji hayo iliziba ikiwa ni katika harakati za mwili kuzuia wadudu wa homa ya uti wa mgongo kuingia kwenye ubongo. Alikaa muhimbili kwa miezi saba na kwakuwa ni vigumu kufanya operation ya uti wa mgongo waliamua kumuwekea shunt. Hii ni tube ndogo iliyoshonewa karibu kabisa na ubongo na inateremka hadi tumboni ambako maji yanayozidi kwenye ubongo hupelekwa kupitia tube hiyo (iko ndani kwa ndani). Alipata tatizo hilo akiwa na umri wa miezi 8, sasa ana miaka 6. Amekuwa akipata kifafa kwa sababu hiyo.

Ni kweli basi kuwa kifafa hakiambukizi na si vizuri kumnyanyapaa mgonjwa. Ugonjwa hauna dawa za kitaalamu, zilizopo ni za kutuliza tu. Lakini kuna dawa za kienyeji ambazo zinasaidia zadi kuliko za hospitali.

Nakushauri kwa sasa mpeleke kwa babu wa Loliondo; mimi wangu nimeshampeleka, nimetoka huko wiki iliyopita hivyo ni mapema kujua kama amepona au la. Baada ya miezi miwili nitakuwa na la kusema; ila nina imani atakuwa amepona!

Dah! Pole sana mkubwa. Vilevile nashukuru kwa ushauri.
 
Naomba msaada jamani, hivi ugonjwa wa kifafa a.k.a mwezi mchanga unatibika?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom