Kifafa ukubwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifafa ukubwani

Discussion in 'JF Doctor' started by sajosojo, Aug 1, 2011.

 1. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Nina mdogo wangu ana miaka 20. Alianza kuweweseka na kukakamaa pamoja una kujingata ulimi usiku akiwa amelala bila yeye kujijua, asubuhi anajikuta ameumia mdomoni...bila kuchukua hatua akijua hali hiyo labda ni ya mda mfupi lakini hali inazidi kuwa mbaya kwani sasa anaanguka mchana... Je dawa ya tatizo hili ni nini kwani hakuwahi kuwa na kifafa before
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Kifafa unaweza ukawa ugonjwa...mara nyingi huu uanzia tangu ukiwa na umri mdogo. Lakini pia kifafa kinaweza kikawa dalili ya tatizo kubwa la ubongo, especially kinapoanzia ukubwani, na haijawahi kutokea mgonjwa akawa na ugonjwa huo tangu utoto, na hasa kama inatokea mara mara...mfano mara kadhaa katika wiki moja.

  NB: Mpelekeni haraka hospitali akaonwe na neurologist na/au neurosurgeon. Hii itakuwa level ya hospitali ya rufaa, kama mpo Dar es salaam nashauri Muhimbili. Najua katika hospitali ndogo watamtibu kama mgonjwa wa kifafa na kumpa dawa za kifafa bila kuchunguza nini kimesababisha apate kifafa ukubwani.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Je, kuna tiba ya kifafa? Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali zingine kama vile uvimbe kwenye ubongo ,ugonjwa wa figo au ugonjwa wa ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

  Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa mda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Dalili na ishara za kifafa Nitajuaje ikiwa niimeathiriwa na kifafa?
  Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika

  kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

  Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya mda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa mda baada ya kuzirai.

  Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa zingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.

  Katika aina zingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.

  Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.


  Je, kuna tiba ya kifafa? Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali zingine kama vile uvimbe kwenye ubongo ,ugonjwa wa figo au ugonjwa wa ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

  Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa mda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.


  Jinsi nyingine za kudhibiti kifafa Kando na madawa, ni nini kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?

  Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata amedhibitiwa na matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8 ilhali mtoto anahitaji angalau masaa 9) kunaweza kusababisha mshtuko wa

  kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia kusababisha shambulizi. Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya kutokea kwa mshtuko wa kifafa. Taa zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa

  katika watu wengine. Kupumua kwa nguvu wakati unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara katika watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa unaweza kuepuka haya, unaweza kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.

  Kwa nini haupaswi kumwekea mtu kitu mdomoni anaposhikwa na mshtuko wa kifafa?
  Kwa mda mrefu iliaminika ya kwamba wakati mtu ameshikwa na kifafa, mgonjwa anaweza kumeza ama hata kunyongwa na ulimi wake na kwa hivyo kusababisha kifo. Hivi sasa hali imebadilika na inaeleweka ya kwamba hakuna haja ya kuweka kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na kifafa. Hili linaweza kusababisha madhara zaidi.

  Wakati wa kifafa kuna mshtuko wa ghafla wa misuli.Mikono, miguu na sehemu zingine za mwili huwa na mwendo wa kujirudia rudia ambao ni vigumu kuukabili kwa kutumia nguvu haswa ikiwa mgonjwa ni mkubwa kwa umbo. Kama sehemu ya tendo la misuli, mgonjwa husaga meno yake kwa sababu ya tendo la nguuvu katika taya. Jaribio lolote la kuweka kitu kwenye mdomo linaweza kusababisha kuvunjika kwa meno ya mgonjwa, kunyongwa na kile kilichowekwa mdomoni ama mgonjwa kumuuma vibaya mhudumu wake.

  Kwa hivyo fahamu: USIWEKE kitu katika mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na mshtuko wa kifafa.
   
 5. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  thanks so much and God bless you all
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wagonjwa wa kifafa hawawezi kugawana madawa yao? Madawa ya kifafa hufanya kazi ya kukomesha shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo. Kuna aina nyingi za kuzirai katika kifafa na hizi zote huitikia kwa njia tofauti kwa madawa tofauti. Hii ndio sababu ya kwanza kwa nini haufai kugawa dawa za kifafa. Dawa ambazo hudhibiti aina moja ya kifafa zinaweza kukosa athari kwa aina nyingine ya kifafa.

  Pili, watu tofauti wanahitaji vipimo tofauti vya dawa iliyotolewa kudhibiti kifafa. Ugonjwa wa kifafa unamaanisha ya kwamba ubongo wa mtu unaweza kufyatuka kwa njia isiyo ya kawaida. Watu tofauti hupata kifafa katika viwango tofauti vya mchangamsho wa ubongo. Watu wengine huchangamshwa kwa urahisi na kuzirai ilhali wengine hawachangamshwi kwa urahisi. Kipimo cha dawa kinachotumiwa kumdhibiti mtu ambaye huzirai kwa urahisi ni tofauti na kile cha yule ambaye hazirai kwa urahisi.

  Tatu, sio vizuri kugawana madawa ambayo yametolewa kufuatia maagizo ya dakitari. Maagizo ya dakitari hutoa dawa kwa mtu mmoja kwa kipindi maalumu cha wakati. Kwa kugawana madawa, mtu ambaye alipewa maagizo ya dakitari ataishiwa na dawa kabla ya ahadi ya kuonana na dakitari inayofuatia. Wanweza kuzirai kwa urahisi kwa sababu hawako kwenye matibabu. Sio salama kwa mtu mwenye kifafa kugawa dawa zake

  Matatizo yaweza tokezea wakati wa matibabu? Je kuna jambo ambalo linaweza kuenda mrama nikiwa bado kwenye matibabu?

  Athari ya matibabu ni hisia ya kusinzia na kutokuwa mwepesi ambako hutoweka baada ya mda. Baadhi ya madawa yanaweza kumfanya mgonjwa aongeze uzito. Athari mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea ni kwenye ini. Hili ni jambo la kawaida wakati mgonjwa anatumia madawa kadhaa ili adhibiti kifafa.

  Unapoanza matibabu, athari yake kwa kifafa huwa siio ya papo kwa hapo. Inachukua angalau mwezi mmoja kuona athari yoyote ya kudumu na mtu anahitajiwa kuwa mvumilivu. Katika visa vichache, visa vya kuzirai vinaweza kuongezeka unapowekwa kwenye matibabu kabla kuzirai hakujapungua.

  Ni kipi kipimo cha dawa za kutibu kifafa? Kipimo cha dawa ni kile ambacho kitatibu kitadhibiti ama kitatibu hali hii bila ya kusababisha mathara mabaya ya kando. Hii hutofautiana kutoka kwa matibabu hadi matibabu na hali hadi hali. Dawa zingine kama Panadol zina kiwango chake rasmi; watu wazima humeza vidonge 2 kila masaa 6-8. Hali zingine kama malaria isiyo kali zina kiwango cha dawa kinachopeanwa katika kiwango cha kipimo cha dawa kama watu wazima humeza vidonge 2 vya Camoquine mara moja kwa siku 3.

  Hesabu ya kiwango cha kipimo cha dawa hutegemea uzani wa mgonjwa ama umri wake. Kila aina ya dawa ina kipimo kwa uzani ama umri wa mgonjwa uliopeanwa.

  Katika visa vingine vya kifafa, kiwango cha dawa hakiwezi kuhesabika kwa urahisi. Matibabu yanayotolewa ili kudhibiti kifafa huathiriwa kwa urahisi na vipimo vya dawa na hufanya kazi katika kadiri ndogo. Dawa kidogo kwenye damu ama dawa nyingi kwenye damu na udhibiti wa kifafa hupotezwa. Kwa hivyo kila dawa inaweza tu kutumiwa katika kadiri iliyotolewa ya kipimo cha dawa. Ikiwa kuzirai hakuwezi kudhibitiwa katika kadiri hii,dawa ya pili na saa zingine dawa ya tatu inaweza kuongezwa. Hii nyongeza ya madawa hujiathiri na kipimo cha kila dawa kinahitaji kuhesabiwa mara tena ili kila dawa ikuwe katika kiwango kinachofaa katika damu.

  Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, kutokea kwa kifafa hakuwezi kutabirika katika watu tofauti. Kuna wale ambao ugonjwa wao wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ilhali wengine wanahitaji matibabu 2-3 ili kupunguza visa vya kuzirai bila ya kuvimaliza kabisa. Kwa wagonjwa 2 wenye umri sawa na uzani sawa, matibabu ya kipekee yanaweza kutolewa katika vipimo tofauti ili kudhibiti kuzirai kwao.
   
Loading...