Kidume wa Tanzania na anayefaa kuitwa wa kimataifa

proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,257
2,000
1. Simba ndiyo timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa, ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie.

2. Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.

3. Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.

4. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyewe na hili lilinuliwa mwaka1968.

5. Simba ndiyo timu ya kwanza kumiliki jengo lake lenyewe na hili lilizinduliwa 1971.

6. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa bingwa wa ligi kuu nchini1966.

7. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwakilisha nchi na hii ilikuwa 1967.

8. Simba klabu ya kwanza nchini kwenda Ulaya na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland

9. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa mabingwa wa Afrika Mashariki na kati na hii ilikuwa 1974.

10.Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa Afrika Mashariki na Kati, ndiyo timu iliyochukua ubingwa mara nyingi kuliko klabu yeyote Afrika Mashariki na Kati (Champs off all time.)

11.Simba ndiyo timu pekee nchini iliyowahi kufika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika na hii ilikuwa1974.

12.Simba ndiyo timu pekee nchini na Afrika Mashariki kufika fainali ya kombe la Caf na hii ilikuwa1993.

13.Simba ndio timu inayoshikilia rekodi Afrika kama si duniani kwa kufungwa na Mufurila Wonderers ya Zambia magoli 4-0 na kwenda kuibamiza 5-0 kwao, mbele ya Rais wao Kenneth Kaunda.

Hii haijafanywa na klabu yeyote Afrika na nina mashaka duniani, hii ilikuwa 1979.

14.Simba ilicheza katik hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika 2003 kwa mafanikio makubwa kulinganisha na timu yoyote nchini.

15.Simba ndiyo timu pekee kuivua ubingwa klabu bingwaAfrika nadi Zamalek hii ilikuwa pia 2003.

16.Simba ndiyo klabu pekee nchini kuzifunga timu zote za mataifa ya kiarabu kuanzia· Waliowatoa mwaka jana Etoile du Sahel (Tunisia)·
Widad Casablanca (Morocco)·
El Setif (Algeria)·
El Harach (Algeria)
halaf tumezifunga timu zote kubwa za Misri Zamelek,Al Ahly, Arab Contractors, Ismailia, Mehala, Al kubra na timunyingine mnajua huwa inafanywaje ikigusa kule.
Pia imeshaitoa El Merekh ya Sudan 1994 katak klabu bingwa ya Afrika.

Simba pia imeshazifunga miamba ya Afrika Magharibi kuanzia Asec, Asante Kotoko, Hafia ya Guinea hata mabingwa wa kihistoria wa Zambia Nkana Red Devils.

17. Tukirudi juu Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa suti na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland.

18.Simba ndiyo klabu pekee nchini kujenga jengo lake yenyewe kwa nguvu za wanachama na mashabiki, wenzetu ni mkopo na msaada toka kwa mzee Karume100%, Simba ilipewa kiasi flan na mzee karume baada ya jengo kukamilika na hii ilikuwa mwanzoni mwamiaka ya 70.

19.Angalia idadi ya wachezaji wa Simba walioenda Ulaya kucheza soka la kulipwa.· Nico Njohole· Deo Njohole· Kassim Matitu· George Kulagwa

Huku ikiwa na makumi ya nyota wake kadhaa waliowahI kutapakaa sehemu mbalimbali duniani.

Nikutajie wachache.· Khalid Abeid· Haidar Abeid· Martin Kikwa· Athman Mambosasa· Zamoyoni Mogella· Hamis Gaga· Lilla Shomari· Iddi Pazi· Kiwelu Mussa· George Masatu· Hussein masha na wengine wengi.bila kumsahau nguli wa sasa mbwana samata.mutoto ya msimbazi.

Na hapa kumbukumbu zikae vizuri wazee wangu mimi, Sunday na Kassim Manara wakati wanaenda kucheza Ulaya hawakuwa wachezaji wa Yanga, walikuwa wakicheza Pan African.

20. Nimalizie kwa kuwaambia FIFA ilizitaja timu bora za karne kwa kila nchi kwa Tanzania Simba ilitajwa ndio timu bora ya karne na wenye mpira wao FIFA.

Nenda kwenye rekodi za Caf ndio utajua nani wa kimataifa bainaya cc na wao.

Porojo za mjini ntakuwa nimezimaliza sasa na anayebisha abishe kwa data. Wakoloni wetu walitufundisha hivi…No reaserch no data no right to speak.
Tafsiri isiyo rasmi, hujafanya utafiti na huna takwimu funga bakuli lako.

Asanteni na nendeni mkawaambie.Haji S ManaraMsemaji wa klabu bora ya muda wote Tanzania (best club of all time)

Ukiona errors zipotezee jadili issues na nnaruhusu challenges kama zipoPorojo peleka kuleeeeeee.

Nimalizie Tu Kwa Kusema Msemaji Wa VYURA FC au Yanga Football Club Jerry Muro Anyamaze

Kwani Sasa Wanasimba Wameamua Kutembea Na Facts Hizi Ambapo Sasa Watakuwa Kama Wakimsikia Anaikashifu au Kuitukana Simba Sports Club Basi Na Wao Watamkabidhi Hizi Data Ili Kusudi Na Yeye Pia Atupatie Za Yanga Kama Zipo.

Shikamoo Msemaji Wa Simba Sports Club Haji Manara Hakika Leo Umemaliza Kila kitu

Ningeshauri Sana Ewe Mwana Yanga Football Club Yoyote Utakayeiona Hii Na Kuisoma Basi Si Vibaya Ukaisambaza Kwa Wana Yanga FC Wenzio Popote Pale Walipo au Watakapokuwepo Ili KUMBUKUMBU Hii Muhimu Isije Ikawatoka AKILINI Mwenu. Kila Mwana Yanga Apate Copy Ya Hii Tafadhal

Kusambaza tu tunasambaza
 
lil wayne

JF-Expert Member
Apr 15, 2016
994
1,000

Tambo za kijinga kama hizi haitoifanya klabu yetu Simba SC irudi kwenye ubora huu.

Wanachama tusipokuwa makini hatuwezi kurudi kwenye enzi hizi... Ogopa sana watoto zetu watakaokuja kushabikia Simba nao waje kujivunia mafanikio ya kale ambayo babu yao anajivunia sasa.

Ni muda muafaka sisi kama Mashabiki wa Simba tushiriki kujenga legacy mpya ya klabu. Nini maana ya kushabikia legacy za nyuma na kujivunia nazo? Kumbuka kiwa hata Aston Villa ya uingereza ishawahi kubeba ndoo ya UEFA... Je nao wanaweza kujiweka kwenye sahani moja na Arsenal,. Man City, Man Utd na akina Chelsea...?

Ninapoona eti msemaji wetu wa Klabu anahojiwa na chombo cha habari na ghafla anaanza kutaja hizi rekodi za miaka hiyo badala ya kutuambia na kutufafanulia mikakati ya Klabu kuelekea LigiKuu, inauma sana kwa kweli.

Tuwe makini sana wapenzi wa Simba SC.

Bado Aston Villa wanajivunia ushindi wao wa Uefa na vikombe vingine ,na hizo timu kubwa unazozitaja ziliwahi na zitaendelea kuchezea kichapo na timu ndogo tu,mpira hauna mwenyewe bro
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,101
2,000
Cha ajabu historia yenyewe ya kutunga na hata kama ingekuwa kweli ina umuhimu gani. Timu ya kwanza kuvaa suti. Kuna ushahidi gani?
Yanga tusijerogwa kujivunia upuuzi kama huo. Kila nchi ina bingwa wa kihistoria. Kila mwenye akili timamu ataelewa ni Yanga. Lakini haisaidii sana mbio za ubingwa mwakani
 
lil wayne

JF-Expert Member
Apr 15, 2016
994
1,000
Bado Aston Villa wanajivunia ushindi wao wa Uefa na vikombe vingine ,na hizo timu kubwa unazozitaja ziliwahi na zitaendelea kuchezea kichapo na timu ndogo tu,mpira hauna mwenyewe bro

Nakubaliana na wewe na ukisemacho. Ila hata kama timu kubwa zilizowahi na zinazoendelea kuchezea kichapo kutoka timu ndogo hazitobadilisha heshima ya timu hizo kubwa na nafasi zao. Wataendelea kuwa pale na heshima yao
 
proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,257
2,000

Nakubaliana na wewe na ukisemacho. Ila hata kama timu kubwa zilizowahi na zinazoendelea kuchezea kichapo kutoka timu ndogo hazitobadilisha heshima ya timu hizo kubwa na nafasi zao. Wataendelea kuwa pale na heshima yao
Nashukuru kwa kukubali kuwa Simba ni kidume kwa Yanga ya matopeni
 
Nanren

JF-Expert Member
May 11, 2009
1,898
2,000
Simba ni timu ya kwanza Tanzania KUGONGWA na Clube Recreativo Desportivo do LIBOLO ya Angola.
 
Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
13,488
2,000
Wa kimataifa kwa sababu ya historia ama kushiriki michuano ya kimataifa? Hebu acheni kuwa vibwengo mfunguke ufahamu
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,783
2,000
du, safi sana kwa kuweka historia na kumbukumbu sawa....ngoja usikie yeboyebo watakavyokuja kutoa mapovu yao hapa.
 
proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,257
2,000
Wa kimataifa kwa sababu ya historia ama kushiriki michuano ya kimataifa? Hebu acheni kuwa vibwengo mfunguke ufahamu
Mkuu soma point yangu kuanzia namba 8 na kuendelea,ukisha elewa ndipo ujiulize kama ulitakiwa kueleza ulichosema,povu hazifai .
 
proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,257
2,000
Wamchangani kazi mnayo,Endeleeni tu kushangilia ujinga wenzenu wanasonga mbele
Hata huyo msemaji wa timu yako hajui hata historia ya timu anayo isemea,hapana cheza na simba wewe ebo waulize kina Enyimba ,Zamalek Asek na wengine usikie walifanyiwa nini mwaka 2003 tena kwao ,Sio nyinyi mnaenda kurukaruka na kurudi,Timu inacheza dak 270 inafunga gori moja ,da wamatopeni bwana.
 
jm group

Senior Member
Jan 10, 2015
118
225
Historia ina matter kwenye kila kitu usibeze waliyofanya simba hata hayo mnayoyaita ya zamani wakati yange yange hamna ya zamani wala ya sasa kimataifa
 
Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,686
2,000
Hata huyo msemaji wa timu yako hajui hata historia ya timu anayo isemea,hapana cheza na simba wewe ebo waulize kina Enyimba ,Zamalek Asek na wengine usikie walifanyiwa nini mwaka 2003 tena kwao ,Sio nyinyi mnaenda kurukaruka na kurudi,Timu inacheza dak 270 inafunga gori moja ,da wamatopeni bwana.

Yanga ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi mara nyingi,Yanga pia imeshinda mechi nyingi za derby.Kwa hali mliyo nayo sasa hamna jinsi endeleeni kuzoea huko mchangani
 
proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,257
2,000
Yanga ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi mara nyingi,Yanga pia imeshinda mechi nyingi za derby.Kwa hali mliyo nayo sasa hamna jinsi endeleeni kuzoea huko mchangani
Simba ndio timu ya kwanza kupanda ndege hapa bongo na ni timu ya kwanza kupiga suti na yanga wakaiga.Wamchangani bwana kila kitu wanaiga tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom