Kidume Shituka: Ukijibiwa SMS yako hivi na Mwanamke, Acha haraka sana kuchat nae

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,515
2,000
Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaidatu kwa ajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.

KWA MFANO:

1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''

2. Ukimtumia sms ''Maishayanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maishamagumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui

3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''

4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa uposerious.

Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k

Lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako.

 

Daniel Myl

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
536
225
Teheheeeee...... Hawa wadudu nawaogopa sana, problem ni kwamba hawaelewi kwamba unaweza usiwe na pesa.....! Ee bwana sina kitu dear... Tayari umeshakuwa Mwanaume suruali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom