Elections 2010 Kidonge Kichungu- tema au meza

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
1.Ni kweli demokrasia ya Tz kama ilivyo nchi nyingi hususani za Afrika bado inahitaji kukua. Kutahitajika kuwepo mabadiliko ya katiba, sheria na hata muundo wa Tume yetu ya Uchaguzi na wasimamizi wake huko majimboni na utoaji wa matokeo ya uchaguzi mapema.

2.Vyombo vya habari bado vina safari ndefu katika kuimarisha wajibu wao na hususan wakati wa uchaguzi mkuu na kuajibika vyema kwa ufanisi pasi ushabiki wa kisiasa.

3.Vyama vya Upinzani vina changamoto nyingi. Mara nyingi wanaongelea nguvu za nje zinazowaathiri bila kugusa kwa kina madhaifu waliyonayo ndani mwao mfano:

i. Ukweli ni kuwa Wananchi wengi wanaweza kuwa wameona mbadala wa aliyekuwa Mbunge au Diwani wao lakini bado hawajaona Chama kingine mbadala wa CCM katika kutawala nchi. Utaratibu wa CCM kuwa na kura za maoni toka kwa wanachama wote ni jambo linaloendelea kuwapiga deni sana Wapinzani. Chama hakiwezi kuwa kinasubiri watu wanaokataliwa toka chama kingine. Hili lina madhara makubwa sana katika afya ya Chama hata kama aliyehamia atashinda katika uchaguzi!

ii. Ukweli ni kuwa Upinzani mnatakiwa kusambaa nchi nzima na muwe hai wakati wote si kusubiri wakati wa uchaguzi.

iii. Ukweli ni kuwa Upinzani hamko pamoja na hivyo kutia mashaka sana wananchi kile mnachokitafuta mkipewa madaraka. Angalia hata wakati wa midaharo, Lipumba anawaeleza Watz ‘u- Kilimanjaro’ wake na ‘u-Kichuguu’ wa Silaa.

iv. Ukweli ni kwamba kiwango cha uelewa kimeongezeka sana katika kuchambua nini Mgombea anasema na kuahidi. Ingawa ni kweli kuwa Serikali yetu inaweza kuboresha huduma za afya, elimu, maji n.k na hasa kwa kuongeza uwajibikaji, ni vyema upinzani kuwa wakweli kwa kuzipitia tena sera zao na ahadi za huduma za bure kwa wote na kuondoa kodi nyingi baada ya kufanya tafiti za kisayansi, hapa nilimkubali Lipumba. Kupambana na mafisadi ni agenda inayotakiwa kuendelea kuzungumzwa na kushughulikiwa, hata hivyo lazima pia tuongee kwa nguvu zote juu ya kuwa na sera za kuhakikisha uwajibikaji na kuongeza uzalishaji na matumizi ya sayansi na teknolojia nchini kama tunataka kupunguza umaskini na kuwa na maisha bora.

4. Ingawa Mh. Silaa kwa namna moja ameamsha hamasa za upinzani katika nchi, bado ukweli unabaki kuwa kura zake katika nchi yote ( Bara & Visiwani) hata zingerudiwa kuhesabiwa upya hazitatosha kumzidi Mh. Kikwete. Na siamini kuwa ni kwa sababu ya uchakachuaji (vinginevyo Mnyika, Tindu Lissu, Mdee hata Mr. Sugu, n.k wasingekatiza!) bali ni upinzani kutodhibiti au kushughulikia madhaifu ya ndani niliyoyataja hapo juu (na. i – iv).

Wito kwa CCM: kaeni chini na kujiuliza pale ambapo mmepoteza viti pasi kutegemea nini kimetokea ili mrekebishe. Mjitahidi kuleta maboresho yanayopaswa kiutendaji katika Serikali kama mnataka kuendelea kupata kibali machoni pa Wananchi miaka mitano ijayo.

Wito kwa Upinzani: Shughulikieni madhaifu yenu ya ndani pamoja na umoja wenu wa kweli (usio wa ubinafsi) ili mpate kibali cha ama kutawala au kuwa wenza katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa miaka ijayo.
 
Fair analysis. Labda niangalie point (i) hapo juu. Si kweli kwamba watu hawajaona mbadala wa kuongoza zaidi ya CCM, mimi nadhani ni uelewa tu wa watz wengi more than anything else.

Nasema hivyo kwa sababu trend inaonyesha kuwa sehemu za miji mikubwa ambazo watu ni waelewa wamekuwa na imani zaidi na upinzani na hasa CHADEMA kuliko CCM. Sasa mathalan kama TZ yote ingekuwa na watu wa uelewa wa say Mwanza, Arusha, Mbeya leo tungekuwa tunaongea lugha nyingine.

Hebu tazama ni picha gani unayoipata kwa jimbo kama la Kawe ambalo ndio wanakaa vigogo wa nchi hii wanapoamua kuwapa upinzani. Hicho ni kielelezo tosha tu kuwa wana imani kubwa kwa CHADEMA kuongoza nchi kuliko CCM.

Kwa hiyo kule kijijini ambako CCM wameshinda sana ni kwa kukosa elimu na uelewa ndio wamewapa CCM kuliko utayari wa CHADEMA/upinzani kuongoza nchi.

Swala la kwamba CCM watarecover from here i choose to disagree. Kwa mfumo huu waliokuwa nao hakuna jipya nnalotegemea. Pia (samahani) uwezo wa Kikwete kuongoza nchi na chama kikubwa kama cha mapinduzi pia ni mdogo sana, huo ni ukweli ambao kila mtu aliyeenda shule analijua hilo.

Sasa kiongozi huyo ambaye ametuonyesha kabisa hata katika kampeni zake kuwa hana vision yoyote badala yake anataja mipango ya serikali sidhani kama nnategemea jipya kutoka kwake, he is to me a crisis manager, anashughulika na jambo linapotokea.

Pia sidhani kama anaelewa hata concept ya policy ni nini, kwa sababu utakumbuka kuwa Kikwete ana degree moja tu ambapo policy discussions katika level hii sio very elaborate kama wale wanaosoma Master na PhD. Hili pia linamfanya Kikwete asiweze kuwa ni mtu ambaye nategemea atafanya anything different from what he did in the last 5 years of his administration.
 
Back
Top Bottom