Kidole changu kimepona asanteni JamiiForums

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,351
Kuna kipindi hapo nyuma wiki iliyopita nliweka post hapa Kidole changu kimevimba na kinauma ,Nilienda hospitalini waliniambia nitumie dawa za ammoxylin na panadol lakini hazikusaidia, Nikabadilisha hospitali nikaenda nyingine wakaniambia nitoe kucha nikaona ngoja nitumie ushauri niliopewa na wana jf wa kutumia Ndula, Hio ndula niliichuma nikaikata juuu na chini na kuipachika sehemu iliyovimba kama vile pete. Nliivaa kwa siku mbili na kidole kimepona kabisaaaa...

SHUKRANI SANA WANAJAMII FORUMS
 
Naomba picha ya hiyo Ndula please
_IMG_000000_000000.jpg
 
Pole mkuu, naamini huo haukuwa ni ugonjwa wa kawaida. Ili kuwa ni harakati za Free mason kukuchukua msukule... Ishukuru hiyo ndumba kwa kukusaidia...
 
Ndula ni tunda LA mmea linalofanana na nyanya chungu katika namna nyingi. Hutumika kutibu meno pia.

Note: si kila Tiba ya kienyeji ni uchawi. Zingine ni tiba halali kabisa.

Hivi mnadhani kabla ya wakoloni kuleta vidonge babu zetu walitibiwaje?
 
Ndula ni tunda LA mmea linalofanana na nyanya chungu katika namna nyingi. Hutumika kutibu meno pia.

Note: si kila Tiba ya kienyeji ni uchawi. Zingine ni tiba halali kabisa.

Hivi mnadhani kabla ya wakoloni kuleta vidonge babu zetu walitibiwaje?
Kwa hapa mjini Dar tutazipata wapi ase ukizingatia hakuna mashamba huku
 
Kuna kipindi hapo nyuma wiki iliyopita nliweka post hapa kuhusu kidole changu kilichovimba ikidaiwa kina mdudu ndani, Nilienda hospitalini waliniambia nitumie dawa za ammoxylin na panadol lakini hazikusaidia, Nikabadilisha hospitali nikaenda nyingine wakaniambia nitoe kucha nikaona ngoja nitumie ushauri niliopewa na wana jf wa kutumia Ndula, Hio ndula niliichuma nikaikata juuu na chini na kuipachika sehemu iliyovimba kama vile pete. Nliivaa kwa siku mbili na kidole kimepona kabisaaaa...

SHUKRANI SANA WANAJAMII FORUMS
Hicho kinaitwa kipesani dawa ndo hiyo hiyo ndura
 

Similar Discussions

17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom