Kidini Kajala ni mke wa mtu, Harmonize atamuoaje?

MimiNiMakini

Member
Jun 19, 2022
7
20
Baada ya Kajala Kuachana na Majani, aliamua akaolewe, bila kupoteza wakati alikamilisha hilo na akaolewa kwa Ndoa ya kanisani kabisa.

Bwana Faraji Agustino ndio Mume halali wa Kajala. Alipopata kesi na Kajala then Kajala akafanikiwa kutoka Jela, Mme wake aliendelea kusota Jela huku Kajala Aliendelea kudate na Wanaume mbalimbali mfano, Quick Rocka, Msami, Mutra. Hii ni dharau kubwa mno, Mme wake yupo jela then yeye akaendelea kudate na wanaume mbalimbali.

TURUDI NYUMA.
Mwaka 2013, Faraji Agustiono alishitakiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) akidaiwa kutakatisha pesa haramu na kuuza nyumba iliyo kwenye zuio la kuuzwa kutoka kwa taasisi hiyo.

Kuuzwa kwa nyumba hiyo iliyopo Mbezi Beach, kunadaiwa ndio kuliko muingiza Kajala kwenye kesi hiyo maana na Saini yake ilikuwepo (Alishiriki na mme wake kuuza nyumba ambayo ipo chini ya kizuizi)

Hukumu ya kesi hii ilitoka kwa Kajala kufungwa miaka 5 jela au faini ya shilingi milioni 13 ambapo alilipa faini hiyo baada ya kupewa nguvu na Wema Sepetu. Mumewe alihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela au faini ya shilingi milioni 200 ambazo alishindwa kuzilipa. Hivyo alitumikia Jela na Mwaka 2017 akaachiwa.

Baada ya Faraji kutoka Jela alipata Skendo zote za Kajala na hakuweza kuendelea kuwa pamoja na Kajala.

Lakini watu hawa hawajapeana Talaka, kwa mujibu wa ndoa za kikristo, mkioana ndio basi tena mpaka Mungu awatenganishe, Sasa Harmonize ataanza vipi kumuoa Kajala? Kwa wanaojua vizuri hizi sheria za kikristo, Je Kajala atafanikiwa kweli kuolewa na Konde, wakati tayari ameshaoelewa na mme wake yupo hai?
 
Back
Top Bottom