Kidato cha sita msichague kozi kwa mkumbo

Rosemary Stephen

New Member
Oct 22, 2019
3
5
Moja ya jambo ambalo vijana wengi wanafanya wakiwa katika kuchagua course za kusomea chuoni ni kufata mkumbo na kuiga kile ambacho wenzao wamechagua.

Wito wangu kwa form six wote waliomaliza sasa hivi, ni kuangalia kwa upana zaidi nini unataka katika maisha yako, usiende kusomea course ambayo huipendi wala hukuwa na malengo nayo. Nenda kasome kitu ambacho HATA UKIKOSA AJIRA UNA UWEZO WA KUJIONGEZA KUPITIA HIKO NA KUJITAFUTIA AJIRA.

Unakuta mtu kasoma PCM na alikuwa anataka kuwa engineeer ila kwa sababu amesikia ajira za engineering ni chache basi anaenda kusomea biashara.

Hii inasababisha
1. Kuzidi Kuwepo kwa wafanyakazi hewa katika sekta za huduma ya jamii

Mtu alikuwa na malengo ya kuwa daktari unaenda kumuweka benki, uhakika wa kuwa utendaji kazi wake utakuwa mdogo ni asilimia kubwa sana maana atafanya sio kwa kukusudia kuwahudumia watu ila apate kitu cha kupeleka kinywani.

2. Ongezeko La wafanyakazi chini ya kiwango

3. Ongezeko la ukosefu wa ajira. Sasa hivi watu wanaajiri ubora wa mtu na sio elimu ya mtu. Kwahiyo hata kama ukisomea kitu chenye soko la ajira kama haupo bora eneo hilo kupata kazi ni ngumu sana.

Wito wangu kwa wadogo zangu form six. NENDENI MKASOMEE VITU MNAVYOVIPENDA HUKO NDIO KWENYE MAFANIKIO YENU.

NECTA-ACSEE-Results.png
 
Wengi huchagua kozi zenye majina mazuri ila wakienda😂😂
Ukiona kozi inajina tamu na complicated yaani refu jua tu ushapoteana,utahangaika na hiyo cheti mpaka basi,unafika chumba cha interview watu wanashindwa kuitamka hiyo kozi yako jua tu ni chaka hilo
 
Ukiona kozi inajina tamu na complicated yaani refu jua tu ushapoteana,utahangaika na hiyo cheti mpaka basi,unafika chumba cha interview watu wanashindwa kuitamka hiyo kozi yako jua tu ni chaka hilo
, mimi nilifuata mkumbo eti ualimu unapata ajira moja kwa moja na boom ni uhakika, kwenye boom ikawa hvyo bt kwenye hicho kipengele cha pili sasa toka 2016 mpk leo holaaaaaa.
 
Shule ya darasani kibongo bongo inamuandaa mtu kuwa mtumwa na masikini maisha yote unless ajiongeze.
 
Hizo za watu wengi kama Account,Finance,Civil engineering,Medical Doctor sio Bsc in Agribusiness and finance investment hahahah huchomoki
Agribusiness? Hawachomoki? You're not serious. Finance investment nakubali...
 
Agribusiness? Hawachomoki? You're not serious. Finance investment nakubali...
Yaani hiyo ni kozi moja inaitwa Bachelor of Science in Agribusiness and finance investment,do you copy? Hahah yaani humo ndani unasoma mambo yote ya biashara ila ukienda interview room wanakuona kama sio chaguo lao yaani kozi kuitamka inakuwa ngumu sana...kozi mpya mpya ni vimeo sana bora usome kozi kongwe hata mkiwa wengi ila kozi inatambulika
 
Back
Top Bottom