Kidato Cha Nne Waanza Mitihani na Janga la Kitaifa

Nungunungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2007
311
13
Wanafunzi 499,274 asubuhi hii wanaanza mtihani ya kumaliza elimu ya kidato cha nne wakianza na somo la Hisabati ambalo kwa sasa ni kama janga la Kitaifa.

Matokeo ya mwaka jana kitaifa kwa somo hilo yalikuwa: F- 77% na 23% zilizobaki ndio walipata A, B, C na D.

Mwaka huu mambo yatakuwaje, ni jambo la kusubiri.

Tunawatakia kila la heri vijana wetu katika mitihani yao.
 
Hivi practical zilisharudishwa?
imean chemistry, biology and physics - practicals?
na Chemistry na physics vilishatenganishwa tena? au bado vipo kwenye muungano?

kila la heri form IV
 
Nungunungu, Heshima yako!

Haya matokeo kwa anayefuatilia trend nzima ya Elimu Bongo hawezi kushangaa matokeo ya Mwaka jana kuwa vile ikumbukwe hii ni ile Form iliyopata bahati maana hata Uongozi wa Baraza la Mitihani umeingia mpya sasa hata ule upumbavu na njaa za watumishi za kuvujisha Mitihani haukuwepo.

Mkubwa Kasana! Practical zimerudi kama kawaida na isitoshe kila somo lina nafasi yake kikamilifu ile ndoa imevunjwa zamani hakuna ule mseto ulioletwa na Blaza Mungai. Kwahiyo vijana Kazi kwao. KILA LA KHERI FORM 4.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom