Kidata karibu tena TRA! Uungwana ni vitendo, usijaribu kuwa Kifutu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,343
217,370
Alphayo Kidata, Rais Samia Suluhu amekurudishia heshima yako iliyoondolewa kwa sababu ambazo hazikuelezwa, tunafahamu kwamba ulitukanwa sana hadi ukavuliwa ubalozi, yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

Nakuomba sana mkuu, tafadhali sana Mzee wangu fanya kazi yako kwa haki huku ukizingatia sheria za nchi. Si kila mtu aweza kubahatika kupata second chance.

Kwa leo ni hayo tu, lakini kesho nitakupigia simu kwa ile namba yangu inayoishia 72 ili nikueleze ambayo siwezi kuandika hapa.

Kila la heri .

Swahili_Times_on_Instagram:_“Rais_wa_Tanzania,_Samia_Suluhu_Hassan_amemteua_Alphayo_Kidata_kuw...jpg
 
Huyu Second chance amepata mara ngapi?

Alikuwa Katibu mkuu Wizara ya Ardhi, JPM akamteua kuwa Kamishina wa TRA, akalegea wapi sijui akampeleka Ikulu bado akalegeza wapi sijui akampa Ubalozi nchini Canada huko sijui aliharibu nini sijui akavuliwa mpaka na Ubalozi wenyewe..!! Ila Mama sijui kama atatuvusha naanza kuwa na Mashakha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kidatq ni mtu mwema sana,ndiyo maana meko alipata naye shida. Ile teua tengua ilikuwa kumtisha tu. Jamaa ameendelea kuwa mwema.

Pamoja na kupewa u RAS hajawa na huzuni wala mfadhaiko.

Daima alisisitiza kufanya kazi kwa uzalendo na sio kwa misheni za mtu..
 
Alphayo Kidata Rais Samia Suluhu amekurudishia heshima yako iliyoondolewa kwa sababu ambazo hazikuelezwa , tunafahamu kwamba ulitukanwa sana hadi ukavuliwa ubalozi , yaliyopita si ndwele tugange yajayo .

Nakuomba sana mkuu , tafadhali sana Mzee wangu fanya kazi yako kwa haki huku ukizingatia sheria za nchi , si kila mtu aweza kubahatika kupata second chance , kwa leo ni hayo tu , lakini kesho nitakupigia simu kwa ile namba yangu inayoishia 72 ili nikueleze ambayo siwezi kuandika hapa .

Kila la heri .

View attachment 1743565
Naona wafanyabiashara wakirudi tena.
 
Back
Top Bottom