Kichwani kwa Bondia Mwakinyo kupo sawa sawa? Amuombe Radhi upesi sana ' Legend ' Rashid Matumla kabla hajatuudhi zaidi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
Hivi atasemaje kuwa Rashid Matumla si Bondia chochote na lolote na kwamba hajawahi Kufanya Jambo Kubwa Tanzania wakati Kirekodi inajulikana kwamba Rashid Matumla ni Bondia mwenye Mafanikio Makubwa kuwahi Kutokea nchini Tanzania ambapo ameshacheza sana Ngumi za Ridhaa, amecheza Olympic na pia amecheza Michezo mingi ya Kulipwa ambayo nina uhakika kwa ' Upumbavu ' na ' Ushamba ' wa Bondia Mwakinyo hatoweza Kufikia na hana hata huo Ubavu.

Amuombe Radhi upesi sana. Na leo kwa Kujiamini kabisa nasisitiza na narudia tena Kusema kuwa Bondia Mwakinyo Juzi hakushinda ila ' alibebwa ' tu na hana Uwezo huo wa Kupigana isipokuwa tu anabebwa na ' Promo ' huku akitumika kwa Chama fulani Kujiimarisha Kisiasa na ' Kipopraganda ' mbele ya Mafanikio yake Kimichezo kwa Watanzania.

Na ' Management ' nzima na wale walio nyuma ya huyu Bondia wa ' hovyo hovyo ' Mwakinyo kutoka Mkoani Tanga kama wasipokuwa makini nae hasa katika Kumjenga Kinidhamu na Kimichezo kuna Siku atakuja Kuwagharimu na hawatowaamini macho na masikio yao. Bondia mwenye ' Maadili ' kamwe hawezi ' Kupayuka ' hovyo na Kuendeleza ' Uswahili ' kama alionao na alivyofanya Yeye Mwakinyo.
 
Bila kupepesa macho naombea pambano lake lijalo mwakinyo apigwe vibaya sana.. hajui kwanini watu tulimwita snake boy huyu! Hajui kuwa snake man alisimamisha nchi pale diamond jubilee ktk pambano lake na yule msouth Africa. Hata cheka mwenyewe ambaye aliwahi kumshinda matumla mara kadhaa pamoja na bangi zake zote hajawahi kumkosea adabu snake man!! .. hawa wasanii kina msangi washamharibu huyu msambaa
 
Mkuu bila ushahidi hizi ni porojo tu kama za Haji Manara Au Bi Hindu.

Pumbavu ametoa Kauli hiyo akiwa anahojiwa na Wasafi fm, Clouds fm na mapema tu wakati Kipindi cha Sports Headquarters cha Efm leo asubuhi amezungumza tena na nina uhakika Watu wote waliosikiliza hizo Redio jana Usiku na hadi leo Asubuhi wamamsikia huyo Bondia ' Mpuuzi ' Mwenzio Mwakinyo.
 
Mkuu, kukamilisha Uzi wako weka na Rekodi za Rashid Matumla Snake Boy

Ungekuwa na Akili Timamu sawa sawa Kichwani mwako usingeniuliza Mimi hili Swali lako la ' Kipumbavu / Kipopoma ' hivi. Hivi kuna Bondia nchini Tanzania ambaye alipata Mafaniko makubwa kama Rashid Matumla ' Snake Boy ' japo Kaka zake akina Stanley Mabesi, Joseph Marwa na Iraq Hudu walijaribu lakini hawakufikia Mafanikio yake?
 
Pumbavu ametoa Kauli hiyo akiwa anahojiwa na Wasafi fm, Clouds fm na mapema tu wakati Kipindi cha Sports Headquarters cha Efm leo asubuhi amezungumza tena na nina uhakika Watu wote waliosikiliza hizo Redio jana Usiku na hadi leo Asubuhi wamamsikia huyo Bondia ' Mpuuzi ' Mwenzio Mwakinyo.
Tutashindwa kama tulivyoshindwa kwenye soka,tumetanguliza siasa badala ya miiko ya mchezo husika!
 
Mnamwongelea bondia yupi? Huyuhuyu ambaye alidundwa juzikati pale shamba la bibi na kupewa ushindi wa mezani km serikali za mitaa? Huyu ambaye haujui hata wimbo wake wa Taifa? My God nisamehe kwa hili tusi nililomezea kwa gongo mchachuo hapa...
 
Bondia Hassan Mwakinyo ambae amekua gumzo nchini na nje ya nchi kwa ushindi wa kijecha jecha kazua tena tafrani baada ya kumtusi na kumtole maneno machafu legendary wa masumbwi nchini Rashid Matumla.

Matumla alikosoa mbinu za kocha wa Mwakinyo kama watu wengine wa kawaida na mwanamichezo wa kawaida, lakini kitendo hicho kimemkasirisha Mwakinyo na kuanza kufoka na kutupa matusi mazito mazito kwa Matumla kua yeye hajui lolote kuhusu ndondi ndio maana hajafika popote na hata watoto wake hawajafika popote kindondi. Mwakinyo kaenda mbali zaidi na kusema lazima Matumla akamuangukie kocha wake amuombe msamaha mara moja la sivyo bifu itakua kubwa na hakuna wakuizima. Mwakinyo amemkejeli Matumla kua alikua anapigwa kama mtoto na kupoteza mapambano mfululizo.

Hakika pata pesa na umaarufu tujue tabia zako, kijana huyu naona kawasahau watanzania kwanza katuita wapumbavu.

Ni muda sasa wakutupa kwenye dustbin huyu dogo asiekua na heshima kwa waliomtangulia, kama alikua hataki kukosolewa angeenda kupigania chumbani kwake
 
Back
Top Bottom