Kichwa kinauma, eti kibuku imelipa kodi kubwa zaidi ya Barrick!!!

chidide

Member
Nov 11, 2010
91
9

Tafakari:Ni ajabu Chibuku kuizidi dhahabu katika ulipaji kodi Tanzania!


Saturday, 03 September 2011 18:54

Na Julius Samwel Magodi

WASWAHILI wanasema zubaa uliwe. Hilo ndilo linalotokea katika nchi yetu Tanzania kwa sasa.

Sikushangaa baada ya msomaji wangu mmoja wiki hii kuniandikia meseji (sms) kupitia simu yangu ya mkononi akisema anashangazwa na Serikali ya Tanzania kulia kuwa haina fedha za kuhudumia wananchi wake wakati Afrika Kusini wanachuma mamilioni ya fedha kupitia madini ya Tanzanite yanayochimbwa katika ardhi yetu.


Msomaji huyu anasema katika Mtaa wa Aderlay na Long kwenye Mji wa Cape Town nchini humo (Afrika Kusini )kuna jengo refu la ghorofa ambalo linaitwa Tanzanite House ambako madini ya Tanzanite ndipo yanapigwa bei.


Meseji hii ya msomaji huyo imenikumbusha takwimu ambazo zilitolewa hivi majuzi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akiahirisha Bunge mjini Dodoma kuwa, kampuni kubwa za madini nchini ikiwamo Barrick inayomiliki migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi, mkoani Shinyanga, North Mara kule Tarime na Tulawaka mkoani Kagera haimo katika orodha ya walipa kodi wakubwa nchini.


Badala yake katika orodha hiyo iliyosomwa na Pinda, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ndiyo inayoongoza ikiwa imelipa kodi ya Sh165.4 bilioni, ikifuatiwa na Benki ya NMB (Sh108.6 bilioni), Kampuni ya Sigara (TCC) (Sh92.1 bilioni), Benki ya NBC (Sh89.9 bilioni) na Kampuni ya Saruji ya Tanzania Portland (Sh73.4).


Hata hivyo, katika orodha hiyo kunakosekana kampuni kama Vodacom na Tigo (simu) huku Kampuni ya Airtel ikiwa imelipa Sh63.6 bilioni kwa mwaka.


Hali hii inazua maswali mengi kwa nini kampuni za madini siyo miongoni mwa walipakodi wakubwa nchini, wakati wanasafirisha tani nyingi za mchanga wa dhahabu na madini hayo kila mwaka kwenda kuuza katika soko la dunia?


Nadhani kuna tatizo hapa ama huenda kuna mikopo ya watu wazito nchini ambao wamekubali baadhi ya wawekezaji wakubwa wasichangie katika pato la nchi.


Kinachosikitisha zaidi ni kwamba kampuni hizi za madini na simu zinazidiwa kwa kulipa kodi na kampuni ya kutegeneza pombe ya Chibuku iliyoko Dar es Salaam ambayo ililipa kiasi cha Sh13.4 bilioni.


Hivi kweli pombe ya kienyeji ya Chibuku ambayo haiuzwi hata nje ya nchi, inaweza kushinda ulipaji kodi kampuni za madini?


Hapa nadhani kuna haja sasa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuangalia upya utaratibu wa ulipaji kodi kwa kampuni kubwa za madini. Haiwezekani kuona kampuni kubwa ambazo ndizo zinatakiwa kuongoza kwa kulipa kodi ndizo ambazo sasa zinalipa kodi kidogo.


Kinachoshangaza zaidi ni kwamba baadhi ya kampuni hizo za madini zimekuwa kila mwaka zikieleza kuwa zimeshindwa kufikia malengo na baadhi yake zikisema kuwa zimepata hasara na badala ya kuondoka zinaomba kuongezewa muda wa kuchimba madini.


Hivi mtu anaye anapata hasara anaweza kukubali kuendelea kuchimba madini wakati fedha zake zinateketea?


Ni wazi hapa kuna kitu kitu, lazima Watanzania tufumbue macho na hasa viongozi wetu wakiongozwa na Wizara za Nishati na Madini, Fedha, lazima waelewe kuwa hawa ni wawekezaji ambao kama hatutaweza kuwabana wataendelea kutolipa kodi inayotakiwa.


Katika orodha hiyo ya Pinda, kampuni ya madini ya Tanzanite haimo wakati kule Afrika Kusini ni moja ya kampuni ambazo zinatengeneza mabilioni ya fedha kila mwaka kutokana na kuuza madini hayo katika soko la dunia.




Ni wazi kuwa kama Serikali haitaweza kuwabana wawekezaji kulipa kodi inavyotakiwa Tanzania itaendelea kubaki kuwa nchi inayosifiwa kuwa fursa nzuri ya uwekezaji, lakini ambayo hainufaiki na badala yake wageni ndio wanaoneemeka.


Mbali ya kampuni hizo za madini kushindwa kulipa kodi kubwa, fedha ambazo wanalipwa wananchi wanaozunguka migodi bado ni ndogo ambayo hainufaishi.


Kwa mfano, leo nenda katika migodi mikubwa nchini angalia maisha ya wananchi wale wanaoishi karibu na migodi hiyo, wanaishi kwenye nyumba za tope, huku usiku wakitumia vibatari na vijinga vya moto, lakini jirani yao mwanga wa taa za umeme za mgodi ukiwaka.


Fedha zinazotolewa kama mrabaha na kampuni hizi kwa mwaka ni ndogo mno sawa na mtu kumlambisha asali mdomoni huku wewe ukibaki na kibuyu kizima.


Kwa kufika mahali hapa, inafaa Watanzania tuamke, tutafakari na tusikubali kuendelea kugeuzwa shamba la bibi, wawekezaji watulipe kodi zetu kama inavyotakiwa.


Vinginevyo, TRA na Hazina watuambie kulikoni kodi zetu kutoka katika kampuni hio hazilipwi ipasavyo?


0754 304336



juliusmagodi@yahoo.com This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it



 
inashangaza sana tra au wamelala au wanatumika....hivi karibuni walitumwa kufuatilia kodi za chama cha chadema..wakapiga kelele sana huku wakiacha mamilion ya pesa yakipotea kny makampuni ya madini na simu....,wananchi tunatakiwa kufanya maamuzi otherwise vizazi vijavyo vitachoma maoto makaburi yetu..
 
Duhh kweli aibu yaani pombe ngumu inaizidi dhahabu?

Kuna maana gani kung'ang'ania hii migodi?
 
Haki ya mungu tumelogwa nawashangaa wahubiri kwa nini wasiombee nchi jamani itakufa siku si zake
 
Very simple: Watanzania wanunua pombe zaidi kuliko dhahabu!!! Kama hutaki basi wewe mbishi tu!!

Unataka kuniambia dhahabu yetu inayochimbwa na hao waporaji hainunuliwi huko wanakoipeleka??? Hivi kweli unajua bei ya dhahabu katika soko la dunia??? You are "very simple" indeed!!
 
Am not suprised, kama mawaziri wananunuliwa suti na "wawekezaji" nani anajua vitu vingine wanavyopewa? We have a long way to go.
 
Haki ya mungu tumelogwa nawashangaa wahubiri kwa nini wasiombee nchi jamani itakufa siku si zake

Nchi hii imeshakufa mkubwa!!! Maana kuna vifo vya aina nyingi. Kimaadili na kiuwajibikaji nchi hii ni marehemu siku nyingi!!!
 
na ule mtandao unaojitangaza kwamba unaongoza tanzania! vipi kwenye mambo ya kulipa kodi? ila sishangai sana maana yule 'spika' mtaalamu wa kuuza mbuga za wanyama aliwahi kuwa mwenyekiti wa board wa mtandao huo!
 
CCM kuendelea kukaa madarakani ni janga la kitaifa. Ndiyo maana bei ya pombe inapanda kila mwaka,
 
Nitakuja baadae wacha nifanye kazi kwanza siku utakija sikia soko la samaki linalipa kodi zaidi ya barrick
 
inashangaza sana tra au wamelala au wanatumika....hivi karibuni walitumwa kufuatilia kodi za chama cha chadema..wakapiga kelele sana huku wakiacha mamilion ya pesa yakipotea kny makampuni ya madini na simu....,wananchi tunatakiwa kufanya maamuzi otherwise vizazi vijavyo vitachoma maoto makaburi yetu..
 
Yaah, ndio maana ni rahisi sana Tanzania kupata pombe kuliko maji, ndio maana mambo yanaenda ndivyo sivyo sababu uchumi waendeshwa kwa pombe, hivi ni mataifa mangapi duniani ambako pombe ndio inachukua namba kwa kulipa kodi??

Hii lazima kichwa kiume au kipasuke!
 
Mimi naona ni heri tufunge migodi kwa sababu hatuna akili ya kukusanya kodi za migodini hadi tupate akili ya kutosha. Na serikali ijikite zaid kwenye kuwekeza kwenye chibuku mana inalipa kuliko migodi.
 
Mimi naona ni heri tufunge migodi kwa sababu hatuna akili ya kukusanya kodi za migodini hadi tupate akili ya kutosha. Na serikali ijikite zaid kwenye kuwekeza kwenye chibuku mana inalipa kuliko migodi.

Ni kheri serikali iwekeze zaidi kwenye Pombe maana ndo mkombozi na inaisaidia serikali kwa kiasi kikubwa katika swala la kodi
 
SAFI SANA HIYO...SASA NIMEAMINI "TANZANIA BILA WAWEKEZAJI WA MIGODI NA SIMU INAWEZEKANA"...tuingie barabarani kuandamana watoke maeneo yetu ya migodi tufungue viwanda vya CHIBUKU.
 
Niliwahi kuongea na auditor mmoja wa TRA kuhusu hili la baadhi ya makampuni makubwa kutolipa kodi na kwanini. Alinijibu kwamba kuna kampuni ambazo ''hazitakiwi kukaguliwa na TRA''. Jamaai anasema yeye kama auditor aliandika taarifa kwa kampuni moja ya kampuni hizo ya kupanga tarehe ya ukaguzi, akashangaa baada ya masaa mawili anaitwa ofisini kwa bosi wake. Akaulizwa nani kakwambia uwaandikie hao kwamba unataka kwenda kuwakagua? Jamaa anasema akajibu kwamba wako ndani ya Wilaya yangu na ninachofanya ni kuzikagua kampuni zote kama lilivyo jukumu la kazi yangu. Akajiwa, ''ok nenda kakague''.

Jamaa akaenda kukagua na kukuta jamaa ni wakwepa kodi wakubwa na wadaiwa mabilioni ya pesa. Ripoti hiyo ikaikabidhi kwa bosi wake. Bosi akaitupia kwenye droo na hakuna kilichofanyika wala hakuna hatua zozoe zilichokuliwa. Sana sana akawa na wasiwasi wa kuhamishiwa Ngara au Ukerewe. Jamaa anasema tangu siku hiyo ikabidi ajifunze toka kwa wenzake kuhusu kampuni zipi hazitakiwi kukaguliwa wala kubughudhiwa.

Hivi kwenye hiyo listi hapo juu mbona kampuni kubwa za wahindi hazimo? Ni kwa kuwa wahindi ni mabingwa wa kutoa rushwa. Kampuni zote zilizo mstari wa mbele kwenye kulipa kodi ni zile zenye wazungu kwa kuwa wanaheshimu sheria za kodi toka utotoni. Kampuni kama Barrick walipewa tax relief kubwa sana na serikali yetu wenyewe, kwa sheria zetu wenyewe kwa hiyo mstarajie watawajibishwa kwa kutolipa kodi.
 
Back
Top Bottom