Kichwa cha mwendawazimu kijifunze kupata kinyozi bora kwa maslahi mapana ya kichwa chenyewe

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Lipo kubwa la kujifunza Tanzania kutokana na uchaguzi wa Kenya,kisiasa,kimaadili na kijamii.

Siasa za Kenya zimejengwa na ushindani mkubwa wa kisera na utoaji wa haki sawa kwa vyama vyote vya siasa. Siasa zetu zimejaa ghiliba,chuki,utumwa,utwana na ubwenyenye unao tengeneza mfumo wa watu wachache wazandiki,wenye roho mbaya ku support maovu yanayo jengwa na msingi mkuu wa dhuluma.

Kenya yeyote anaweza kuwa rais kutegemeana na Imani na utashi wa wananchi,lakini Tanzania imetengeneza mfumo unamtaka anayetakiwa na mfumo kuwa rais ataye utumikia mfumo huo.

Ni suala la muda tu,yaliyo fanyika kule Kenya chini ya waangalizi walitokea Tanzania waliojengwa kwenye mfumo nilioutaja hapo juu,ndo watakuwa wa Kwanza kupinga yale ya Kenya kwa kusema Tanzania Ina democracy yake na mambo yake😱😱😱

Tunaposema tume huru bila katiba huru ni kujidanganya mchana kweupe. Hivi Leo kama Kenya wasingekuwa na katiba nzuri,hiyo tume huru iliyokataa kuingiliwa majukumu yake ingetoka wapi!!!

Uadilifu wa kimamlaka unajengwa na msingi mkuu wa Sheria mama kwa maana ya katiba ya wananchi. Tupopigia chapuo kutaka tume huru kwa katiba ya zamani ni sawa na kuziba tundu la panya kwa kipande Cha mkate.

Uchaguzi huu unajengwa na dhana nzito ya umuhimu wa katiba Bora ya wananchi, ndiyo msingi mkuu wa maridhiano ya wananchi wa Kenya,serikali na vyombo vya maamuzi.

Tanzania tunaipinga katiba mpya kwa kuwa inavunja mianya ya ,watu wachache wanaopuuza maamuzi ya wengi kwa maslahi ya wachache.

Si kwamba uchaguzi wa Kenya hauna kasoro,laa hasha,mazuri ni mengi na ya wazi kuliko machache ya kizani yenye lengo chafu.

Uchaguzi usitufanye kuvunja umoja wetu wa kitaifa kwa tamaa ya madaraka,nchi hii ni ya Watanzania wote,tusiifanye mfano mweusi wa kukimbiwa na mataifa yanayo tufanya mentor wao.

Kenya imejijengea heshima kijamii kwa jamii nzima inayokwenda kuangalia maslahi ya Wakenya kwanza kama taifa moja bila kujali vyama vyao. Imejiheshimisha kwa kuheshimu maamuzi ya wapiga kura ambao kwetu the one who casts vote doesn't determine the victory of the election.

Tumeona ushindani wa sera na mwitikio wa wananchi kupiga kura tofauti na ushindani wa kijinga unaopelekea kupunguza idadi ya wapiga kura.

Tumeona uadilifu toka hatua ya kwanza kinyume na tabia mbaya inayojengwa kuhujumu hata daftari la wapiga kura kwa kutengeneza wapiga kura mazombie kwenye uchaguzi. Huu ni mmomonyoko wa maadili kwa jamii nzima,inayopelekea kiongozi aliyechaguliwa kwa kura za kutengeneza lazima awatengeneze wananchi kujikita madarakani kwa nguvu kubwa.

Tumeona uadilifu wa jeshi la polisi pasi na matamko kama ya kina Sirro,kutishia vyama vya upinzani.

Tumeona nguvu ya mamlaka ya wananchi dhidi ya matakwa ya serikali. Hili ni fundisho tosha kwa sisi tunaojifunza toka kwa wenzetu.

Mwisho,demokrasia na maendeleo ni mapacha,tujifunze kuheshimu misingi ya demokrasia ili tuweze kujiletea maendeleo ya kweli.
 
Back
Top Bottom