Kichwa cha habari gazeti la Mwananchi leo kimenihuzunisha

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Japo mie nshaacha kununua magazeti muda mrefu, ila hupenda kusikiliza kwenye radio kimhutasari magazeti yametoka na habari gani za siku husika.
Leo sikuamini kama gazeti linaloheshimika la Mwananchi linaweza kuwa na kichwa cha habari (kipuuzi) kama hiki. "Dk Mpango amshukia Makonda kama mwewe".

1.jpg
 
Sawa kabisa huyo Bashite aache uhuni,kila RC akiagiza msaada na kupata misamaha ya kodi itakuaje?
Halafu anaandika jina lake hembu imagine angetumbuliwa kabla makontena hayajafika bandarini ingekuaje?RC mpya angewezejae kuyatoa?
Pia baada ya kuambiwa kuhusu jina ange jaza form upya za TRA na kubadili jina kiwa ofisi ya mkuu wa mkoa dsm sasa kwa kiburi hajafanya hivyo.
 
Mkuu ulitaka aandikeje mkuu hebu ipe kichwa cha habari kwa mujibu wa akili yako..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa kabisa huyo Bashite aache uhuni,kila RC akiagiza msaada na kupata misamaha ya kodi itakuaje?
Halafu anaandika jina lake hembu imagine angetumbuliwa kabla makontena hayajafika bandarini ingekuaje?RC mpya angewezejae kuyatoa?
Pia baada ya kuambiwa kuhusu jina ange jaza form upya za TRA na kubadili jina kiwa ofisi ya mkuu wa mkoa dsm sasa kwa kiburi hajafanya hivyo.
Sawa mkuu, hayo yalishapata ufumbuzi nao ni kulipia kodi. Kinachonikere ni uamuzi wa mhariri wa gazeti hilo kumlinganisha Dr Mpango kama mwewe na mh Makonda kama kifaranga vile!
 
Kwa hiyo mkuu ulitaka amlinganishe makonda na nyumbu?, maana mwewe hawezi kumshukia nyumbu akiwa hai
 
Kwa maoni yangu Dr Mpango na mh Maponda wote ni viongozi hivo ni vema kuwaheshimu na si kuwapambanisha ili ionekane nani zaidi. Huu ndo uchochezi wenyewe.
Dr Mpango ni waziri mwenye dhamana, makonda ni mkuu wa mkoa hayuko Juu ya sheria
 
Japo mie nshaacha kununua magazeti muda mrefu, ila hupenda kusikiliza kwenye radio kimhutasari magazeti yametoka na habari gani za siku husika.
Leo sikuamini kama gazeti linaloheshimika la Mwananchi linaweza kuwa na kichwa cha habari (kipuuzi) kama hiki. "Dk Mpango amshukia Makonda kama mwewe".

1.jpg

Pole sana. Wewe umehuzunishwa na hujanunua gazeti kusoma na kuelewa kwa nini wametumia msemo huo na wengine wamenunua na kusoma na kuelewa kwa nini msemo kama huo umetumika. Ukumbuke kwamba kama wewe ungeambiwa uipe hiyo stori kichwa cha habari ungeandika kichwa cha habari ambacho baadhi ya wasomaji wangekuelewa na wengine wasingekuelewa. Hatuwezi wote kuwa na mawazo yaleyale. Kumbuka we are unity in diversity!
 
Back
Top Bottom