Kichunusi kama kijipu kimetokea kwenye kope za jicho nisaidieni dawa jamani

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,738
35,155
Kuna kichunusi kikubwakubwa kimeniota jichoni(kwenye kope za chini).

hakiumi ila kinanikosesha raha kweli!

Naskia kinaitwa kijpu mbuzi.

Naombeni mnaojua dawa yake mnisaidie.
 
pole sana! Sie kule kwetu unamchukua mtoto mdogo wa kiume halafu kale kadudu kake anakagusagusa hapo kwenye jicho kitaisha.
 
Sie Dar huku huwa tunasema hicho kinakuja ukimla chabo mkweo, sasa mama d, mnhhh. Anyway, nenda kwa daktari wana ki "remove" in 2 seconds, daktari mzzuri wa hivi vi minor surgery, jando na kadhalika, nimjuae mimi, ni Dokta Juma, clinic yake ipo pale club ya Pan Africa mtaa wa swahili, Dar.

Nakutakia kila la kheri.
 
Pole! Kichunusi hicho, dawa yake ni kupata karafuu, kile kichwa cha karafuu kiloweshe kikilainika sugua nacho polepole baada ya kubetua kope hizo pale kinapoonekana kichwa cha kijipu mbuzi hicho baada ya muda mfupi ama siku moja kitapotea.

Tahadhari: usitumie nguvu na kuchubua sehemu hiyo.
 
Pole! Kichunusi hicho, dawa yake ni kupata karafuu, kile kichwa cha karafuu kiloweshe kikilainika sugua nacho polepole baada ya kubetua kope hizo pale kinapoonekana kichwa cha kijipu mbuzi hicho baada ya muda mfupi ama siku moja kitapotea.

Tahadhari: usitumie nguvu na kuchubua sehemu hiyo.


asante sana Mwanamageuko!
Nitatumia dawa hiyo leo tu nifikapo nyumbani
 
This is serious!nenda kwenye choo ambacho hujawah hata kidogo kujisaidia,hasa choo cha shimo,chungulia/angalia kwa kutumia macho yako yote dakika 1-5,kat ya hzo,sio compulsory dakka 5, utapona!wenyej wa mbeya watakua wanaipata!practice.
 
Kuna kichunusi kikubwakubwa kimeniota jichoni(kwenye kope za chini ),
hakiumi ila kinanikosesha raha kweli!
Naskia kinaitwa kijpu mbuzi........
Naombeni mnaojua dawa yake mnisaidie.

Kitaalam kinaitwa CHARAZON matibabu yake ni incision and drainage(I&D)
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom