Kichomi ni nini? Husababishwa na nini? Na tiba yake ni ipi?

Mdogo wangu wa kiume anasumbuliwa na vitu kama vichomi upande wa kushoto wa tumbo lake na alifika hospital mara tatu kupimwa anaambiwa ni amoeba lakini tatizo linajirudia after some months hasa wakati wa asubuh tatizo litakuwa nn wataalam?
 
TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO…​

VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo.

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.

Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.
  1. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
  2. Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
Jambo la kuangalia ni je?
  1. Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
  2. Umeinama au umelala
  3. Ukishakula chakula

Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.

Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka.

Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.
Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.
Hasa kama hunywi maji.

Kitunguu swaumu
Chukua kitunguu swaumu punje tano menya kisha viweke ndani ya nusu lita ya maji safi na salama, changanya na maji ya limao moja chemsha mpaka maji yapungue, usisahau kuweka chumvi kidogo kwa ajili ya kupata ladha.
Ukishatengeneza kinywaji hicho unaweza kunywa kila siku glasi moja.
Ni tiba nzuri isiyo na madhara kwa mgonjwa. tumia siku 7 au siku 15 kisha lete mrejesho wako hapa.
 
Mdogo wangu wa kiume anasumbuliwa na vitu kama vichomi upande wa kushoto wa tumbo lake na alifika hospital mara tatu kupimwa anaambiwa ni amoeba lakini tatizo linajirudia after some months hasa wakati wa asubuh tatizo litakuwa nn wataalam?
Acid reflux?

0678096545
 
Mimi ilinisunbuaga nakumbuka nilikuwa nasikia vichomi tumboni... Siku ingine kifua kinawaka moto..nikienda hospital wakipima hamna kitu...nagewa dawa tu...kuna siku tumbo liliniuma mno nilivyofika chooni kujisaidia haja kubwa ilitoka damu...hapo ndo nikaelekea hospital kubwa sasa majibu yakatoka nina vidonda vya tumbo...nikarudi na rundo la madawa ya mwezi mzima...na mpaka sasaivi vinanitesa hivi vidonda
 
Mdogo wangu wa kiume anasumbuliwa na vitu kama vichomi upande wa kushoto wa tumbo lake na alifika hospital mara tatu kupimwa anaambiwa ni amoeba lakini tatizo linajirudia after some months hasa wakati wa asubuh tatizo litakuwa nn wataalam?
Je anatoa choo chenye mtelezo ? Na Kuna vitu kama makamasi hv ? Kama ndio ni amoeba fika duka la dawa nunua dawa metronidazole
 
Habarini Wana jf

Naomba msaada kuhusu management ya kichomi,

Na pia jina lake halisi kitaalamu

Ahsanten! Karibuni
 
Habarini Wana jf

Naomba msaada kuhusu management ya kichomi,

Na pia jina lake halisi kitaalamu

Ahsanten! Karibuni

Pole kwa kuumwa,
Kwa mawazo yangu ni vyema ungesema mambo yafuatayo, yatasaidia waungwana kuelewa tatizo la msingi:

1: Una maumivu sehemu gani ya mwili?

2: Yana muda gani tangu uanze kuumwa?

3: Unapokuwa na maumivu huweza kukaa/kuwepo/kudumu kwa muda gani?

4: Kitu gani huweza kuanzisha/kuleta maumivu husika?

5: Kitu gani ukifanya, hupunguza au huondoa kiasi cha maumivu husika?

6: Maumivu haya huwa ni ya sehemu moja husika au huwa yanaelekea sehemu nyingine ya mwili?
 
Ahsante
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom