Kichina kufundishwa shuleni Tanzania

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
Tanzania inatarajia kuanza kufundisha lugha ya Kichina kama somo katika shule za sekondari hasa kidato cha tano na cha sita. Tayari Wataalamu wa lugha hiyo kutoka China wamekuja nchini Tanzania kusaidia katika kutengeneza na kuanzisha mtaala wa lugha hiyo.

Serikali imetenga shule zipatazo sita ambazo mradi wa majaribio ya ufundishwaji wa lugha hiyo utafanyika, ikiwa ni shule kutoka mkoa wa Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.

Chanzo: BBC Swahili
 
Faida yake ni nini?? kama ni kwa ajili ya biashara na sie walimu wa kiswahili kina Mhilu wataenda kufundisha kiswahili katika high school za Guanzhou, na shanghai?

nafikiria kwa sauti
 
Kichina iwe option tu ya mtu kujifunza au la na sio kuhalalisha. Kichina chenyewe hakina faida kihivooo!
 
Juzi napita hapo Udsm nkakuta wachina wamebandika Tangazo lao kwa kichina.. Yaani wamekuwa wengi mpaka wanabandika tu lugha zao kwenye nchi hii.
 
NEW COLONIALISM.

INABIDI LUGHA YA KISUKUMA AMBAYO INAONGELEWA NA WATZ KWANZA AIANZE KABLA YA KUFIKILIA KICHINA.

HAWA WATU NILIWAKUBALI SANA, ILA TANGU WAMEANZA KUFURIKA HUKU BILA KUFANYA INVESTMENTS ZA MAANA ZAIDI YA UJANJAUJANJA SITAKI KUWASIKIA KABISA. ILA KWAKUA CHAMA CHAO NI RAFIKI WA WATAWALA WANGU CCM SITHANI KAMA KUNA KUSIKILIZWA HAPO.
 
Back
Top Bottom