KICHEKESHO: Mgombea Urais Zanzibar CCM apigia kura Oysterbay DSM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KICHEKESHO: Mgombea Urais Zanzibar CCM apigia kura Oysterbay DSM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Endeleaaa, Oct 31, 2010.

 1. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,223
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Inawezekanaje Mgombea urais wa Nchi moja kupiga kura kwenye Nchi Nyingine? (joke)

  Najiuliza hivi Shain hakujua azma yake kuwa siku moja atakuwa mgombea urais wa Zanzibar? kama hakuandikishwa kuwa mpiga kura zanzibar Ukaazi je? au kwa vile ni CCM?

  Hakika kaweka historia duniani kwa mgombea urais kutopiga kura kwenye Nchi yake mwenyewe anapogombea. Mgombea urais tokuwa na haki ya kupiga kura.

  Likewise Historia kwa Mbatia kuwa mgombea alieshindwa kupiga kura.
   
 2. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,550
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Zanzibar kweli mwaka huu mambo shwari!!! najaribu kufikiria kwa miaka hiyo issue kama hii ingekuwa labda kwa Seif Sharrif hivi ingekuwaje?
   
 3. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kakimbia nchi huyo!
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Iyo issue iliibuka toka mwanzo CCM wakaipoza kiaina
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Shein si mkaazi?

  ukiwa upo nje ya jimbo lako kwa zaidi ya miaka 5 huruhusiwi kupiga kura ama?
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  kwani ilikuwaje wakati wa kwenda kuhamisha majina, sasa itakuwaje kama kura yake moja ndio itamuwezesha kuwa rais huko zenj...au hakujua atateuliwa kuwa mgombea wa urais....CCM bana.....vululuvululu
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Dah ina maana hta yeye hakujipigia kura Zenji? Kaaazi kwelikweli!
   
 8. N

  NTANGUYE Member

  #8
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HUYO hata haeleweki
   
 9. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mimi pia nimeshangaa sana. Labda mwenzetu kajiandikisha mara mbili, akitoka hapo anapanda helikopta anakwenda Pemba kujipigia kura? Au pengine nimesahau, labda uchaguzi wa Zanzibar sio leo ni wiki ijayo?
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kapiga kuwa kituo cha Oyster Bay

  inaonyesha anajiamini, hahitaji kura yake :nono:
   
 11. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2010
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakukidhi matakwa ya sheria ya kujiandikisha kuwa mpiga kura. dkt. shein hajakaa znz miaka 10 mfululizo!!! Sheria ndio inasema hivyo,kabla haijapitishwa wapinzani waliikataa but ccm walikubaliana nayo na hayo ndio matokeo unagombea urais lakini hupigi kura ya kujichagua!!!
   
 12. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Huh! Siamini! Kwa hiyo mgombea urais Zanzibar si mpiga kura wa Zanzibar? Hivi sheria inaruhusu mgombea ambaye hana sifa za kupiga kura? Maana naelewa sifa mojawapo ni kuwemo kwenye daftari husika, au nakosea jama?
   
 13. M

  Mashi Member

  #13
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  SIFA KUBWA YA DR. SHEIN hakuwa king'anizi cha uongozi. Ila watu ndo wamuona anafaa.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ilitakiwa CUF (chama kikuu cha upinzani Zanzibar) imwekee pingamizi la kutokuwa na sifa za kugombea. Lakini haikufanya hivyo kwa sababu ya ndoa iliyofungwa baina ya CCM na CUF!

  Cha ajabu ni kwamba hata vyama vingine havikuweka pingamizi!!!
   
 15. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Na ndugu yetu Mbatia yamemsibu yepi hadi asipige kura?
   
 16. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hilo la mbatia ni ccm tu walikuwa wanajaribu kumtumia ujumbe kwamba hawamhitaji tena pindi Uchaguzi ukipita. Hata hivo hakufanya kazi aliyopewa vema Kama mrema
   
 17. W

  We know next JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hayo ndio matatizo ya Katiba ambayo wagombea wengine wanasema mchakato wake utaanza ndani ya siku 100 White House. Lakini sounds very interesting, unagombea nafasi halafu huna haki ya kupiga kura? something wrong somewhere.
   
 18. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Eeeh sasa ndio mnaliona hilo. siku zote tunawaambia CCM ni cham cha Masanii. Mnaona sasa. Hiyo kura yake moja ndio itamcost leo
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hakujiandikisha huyo, halafu mimi naona hoyo inafaa kwake, make alikuwa anawapigia debe sana CCM.
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  wasi wasi wang hakutaka tu kujiandikisha zanzibar kwa sababu ukiwa upo 'nje ya nchi' kikazi, na ukarudi jimboni kwako unaruhusiwa kuandikishwa na kupiga kura.
   
Loading...