KICHEKESHO CHA DOWANS, Kikwete, majaji na watumishi wa Tanesco si WAZALENDO. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KICHEKESHO CHA DOWANS, Kikwete, majaji na watumishi wa Tanesco si WAZALENDO.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by drangimoto, Oct 17, 2011.

 1. drangimoto

  drangimoto New Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa upeo wangu UZALENDO ni hali ya mtu kuwa tayari kufanya lolote kwa maslahi ya nchi yake, haijalishi kwa kufanya hivyo atakuwa anafuata sheria au anaivunja. Yaani kwa mtazamo wangu UZALENDO uko juu ya sheria!

  Mf. Kwa mzalendo hawez kutii sheria au mamlaka ambayo ipo kwaajili ya maslahi ya kikundi kidogo cha watu na si kwaajili ya umma.

  Hivi ni vema kutii serikal katili, onevu, yenye viongoz wabinafsi, wachoyo, wanaotunga sheria za kuwaweka milele madarakani na wezi wa kura?
  Ktk mazingira kama haya mzalendo hawez kusubiria muujiza wa sanduku la kura ktk kubadilisha hali ya mambo! Sheria mbovu za uchaguz na tume iso huru kwa mzalendo ni sawa na kitanda chenye nge, ambacho hakivumilik hata kwa kukaa macho, sembuse kulala?
  Karume mwaka 63 alivaa sura ya mbuz ili kupambana na ghilba za serikal, hata mwaka 64 january umma ukaingia madarakani ZANZIBAR. Picha ilianza kama MHAINI lkn alikufa akiwa mzalendo na mwanamapinduzi wa kweli, alaa! Kumbe uhaini ukipata nakshi hugeuka na kuwa MAPINDUZI?

  Tunahitaj mapinduz ktk fikra ze2 ili tuwe wazalendo!

  Kikwete si mzalendo coz yuko ikulu kwa maslah yake ndo aliyeleta richmond. Kwani rais wetu si ndo mwenyekiti wa baraza la mawaziri? je, anatoka ktk maamuzi ya baraza hilo hata kama hakuwepo wakati upuuzi huu wanaupitisha?

  Watendaj wa Tanesco hawakuwa wazalendo, kwann wasingejiuzulu nafasi zao kuliko kufanya kaz kwa kushnikzwa tena kwa kupindsha sheria ya manunuz ya umma!

  Majaji waliotupilia mbali pingamizi la wanaharakat na Tanesco dhidi ya dowans nao pia si wazalendo! Kwani hawajui kupita kwa tuzo hii ni mzigo kwa maskini wa kitanzania?
  Mzalendo yko juu ya sheria, anaweza kufanya mambo yake kwa kufuata au kuvunja sheria!
  Hivi majaji wetu wamekosa namna ya kuzuia ile tuzo isipite? Hata kama sheria ilitunyima haki, lkn majaji walitakiwa waoneshe uzalendo ktk hili.
  Kwani mara ngapi majaji w2 wanapndsha sheria kwa maslahi yao binafsi? Yumkini kwa maslahi ya umma?
  Lazma ifike mahala mtz aseme ktk nafsi yake,"sheria imenipa mamlaka ya kufanya hili, lkn sifanyi kwa kuwa si uzalendo, au sheria imenizuia kufanya hili, lkn nafanya kwakuwa kutokufanya si uzalendo"
  haya, ukitaka kujua wale majaji si wazalendo, wanachi wamewaweka ktk kapu la mafisad, yaan walihongwa!
  Asanteni
   
 2. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  nimesoma habari ya Dr. Lingo Tenga jana kwenye gazeti na ndio nikaona kuwa Watanzania kuna haja ya kuamka maana tumelala.
  Ukisubiria hizi sheria zilizopo na mfumo huu kuleta mageuzi, itabidi kusubiria miaka mingine kama 75 (sabini na tano) kuona hata hizo dalili za mapinduzi!
  Tatizo kubwan wale watu tunaodhani wanaelewa ndio hawana kitu kabisa kutokana na kutokuwa na nia ya moyoni kusema ukweli.
  Angalia hapo kwenye red, tatizo si kutokuelewa bali nia ya mtu. Dr. tenga anajua kilichosemwa na BRELA na JK mwenyewe kuwa hakujawahi kuwa na MWEKEZAJI Tanzania aitwaye RICHMOND bali ilikuwa mbinu ya kupata pesa!

  .....
  ...
  Kauli ya Dk Tenga (Mwananchi Oktoba 16)
  Wakili wa kujitegemea kutoka Kampuni ya Law Associates, Dk Ringo Tenga ambaye alitia saini mkataba huo Juni 23, 2006 kama shahidi wa Kampuni ya Richmond, aliliambia Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalumu kuwa wawekezaji wanapenda migogoro yao kusuluhishwa na mahakama hiyo kwa sababu ina uzoefu wa masuala ya biashara za kimataifa.

  "Kuhusu Tanesco kuingia mkataba na Richmond na kuwepo kipengele cha mgogoro kupelekwa ICC, mikataba mingi ya kimataifa inakuwa na kipengele hicho," alisema Dk Tenga.

  Katika kesi iliyofunguliwa na Dowans mwaka 2009 kupinga kuvunjwa kwa mkataba wake iliorithi kutoka Richmond kwenye Mahakama ya kimataifa, kampuni hiyo ilishinda na Tanesco kuamriwa kulipa Sh111 bilioni.

  Baada ya hapo Januari 25 mwaka huu Kampuni ya Dowans iliiomba Mahakama Kuu isaijili tuzo hiyo. Hata hivyo, Tanesco ilipinga. Mahakama Kuu ya Tanzania katika hukumu yake Septemba 28 mwaka huu, iliyosomwa na Jaji Emilian Mushi, ilikubali kuisajili tuzo ya ICC na Tanesco kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.

  Jaji Mushi, alisema mahakama hiyo haina uwezo wa kuingilia maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya kibiashara iliyotoa tuzo hiyo, Novemba 15, mwaka jana.

  Kwa mujibu wa mkataba huo, waliotia saini kwa upande wa Kampuni ya Richmond ni Mkurugenzi wake, Mohammed Gire na Tanesco iliwakilishwa na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji, Johannes G. Loterring (Net Group Solution).

  Dk Tenga, alisema wawekezaji wengi wanahofia kama mkataba usipokuwa na kipengele cha matatizo yao kumalizwa na ICC, wanaweza kupoteza haki yao kutokana na uhaba wa wataalamu wa sheria katika mahakama za kawaida.

  Alisema ugeni katika sekta ambayo mwekezaji anawekeza pia unaweza kuwa moja ya sababu ya kuamua migogoro itakayoibuka na mtu aliyeingia naye mkataba, iende ICC.

  .....
  ...
   
Loading...