kichaa na mwehu..

NG'ADA

Senior Member
Sep 2, 2011
152
15
wadau kama kuna mtu anaweza kunipa tofauti halisi ya hawa watu watu wawili...kichaa na mwehu.
 
Kuku mgeni wewe naona unakamba mguuni......nenda jukwaa la lugha bana
 
Tofauti kati y kichaa na Mwehu ni hivi Mwehu ni nusu ya kichaa,na kichaa kipo cha aina 2 kichaa cha kwanza ni kile cha kufanya fujo, mimi huwa nakiita Kichaa cha joto la mwili, na kuna kichaa cha kutulia kichaa cha tabia ya baridi yaani kwa jina hilo la Mwehu kichaa hicho ni kizuri hicho kichaa unakuwa huwasumbuwi Watu. Ninafikiri umenielewa Mkuu.
 
Kaka asante kidogo naanza kupata mwangaza...

Je na mwendawazimu?
 
kichaa wangu....rafiki yangu!hii lugha ya siku hizi!kichaa mtu anamaanisha rafiki!mwehu mtu akili zimefyatuka
 
Sijui ila nadhani mwenda wazimu ni jina ambalo limemeza kichaa na wehu. kwa hivo mwendawazimu anaweza kua kichaa (cha kwanza au cha pili) kama vile anaweza kua mwehu. Nimejisemea tu, sina uhakika
 
Nimekusamehe binti
 
wadau kama kuna mtu anaweza kunipa tofauti halisi ya hawa watu watu wawili...kichaa na mwehu.
Kichaa ni wale wa kawaida tunaowaona majalalani n.k Mwehu unaweza kumkuta
kavaa suti n.k lakini hana uwezo wa kuamua mambo, mfano Watanzania wote
wanaoipigia kura CCM ni wehu!
 
duh! na wanaopigia chahema watakuwa wendawazimu eti enh!
 
  • Thanks
Reactions: tz1

Ha ha haaa Washabiki wa Arsenal Vichaa, Man U wenda....., Chelsea Wehu Liverpool ndo wazima
yaani inategemea tu na mtazamo wako sina maana ya nilivyoandika.
 
Kichaa, Mwehu na Mwenawazimu wote ni wagonjwa.

Tafsiri yangu:
1.Kichaa- linatumika zaidi kwa wanyama mfano mbwa likimaanisha ugonjwa unaovuruga akili.
2.Mwehu- linatumika kwa binadamu likimaanisha mtu ambaye hawezi kujiongoza mwenyewe.
3.Mwendawazimu -ni mtu aliyerukwa na akili ambaye naweza kurudia hali yake ya kawaida.
 
Hao wote ni wagonjwa wa akili. Tofauti iliyopo ni ndogo sana, Mwehu kwa lugha ya kiingereza ni Lunacy (Lunatic), kwa Kiswahili haswa ni Mbulukwa au Majununi, (majinuni).

Ambaye ugonjwa wake wa akili ina aminiwa kuwa unaathiriwa na mwezi (believed to be affected by the phases of the moon). Wakati mwingine ufanya mambo kama mtu mwenye akili zake na wakati mwingine ufanya mambo tofauti na mtu mwenye akili za kawaida. Kwa ufupi upata maradhi ya akili kwa msimu.

Kichaa ni ugonjwa wa akili, na mara nyingi uendana na ufanyaji wa fujo kama vile kupiga watu, sawasawa na wazimu (Mwendawazimu).
 
Je na mwendawazimu?
Mwendawazimu ni yule mtu ambaye ni mgonjwa haswa wa kichaa anayeokota okota vitu majalalani na kula vitu hivyo vya majalalani anayevaa nguo mbovu mbovu anaweza kufanya fujo wakati wowote ule na kupiga makelele kila wakati.

Last edited by a moderator:

Nashukuru kwa ufafanuzi huu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom