Kichaa kumsomea Mashitaka ni WEHU wa Hakimu

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Ama kweli sasa yanatimia yale ya "Abunuwasi"

Hadithi: Siku moja jamaa alikuwa anaoga mtoni, wakati akiwa kwenye kina kirefu alikuja kichaa akazichukua nguo zote na kukimbia nazo. Jamaa kuona vile akatoka na kuanza kumkimbiza hadi wakafika mjini. Muda wote wakati akimkimbiza alikuwa akipiga mayowe ya ........Kichaa huyo!!!! kichaa huyoooo!!!!

Watu walitoa ili kumkamata kichaa. Hakika huwezi kuamini walimkamata yule aliye kuwa uchi wakidhani ni kichaa. JADILI
 
Mahakimu wetu saa nyingine hawatumii common sense. Eti kwa vile sheria inataka mtuhumiwa afikishwe mahakamani na kusomewa mashitaka ndani ya saa 24 tangia alipokamatwa basi hakimu akaitekeleza sheria kichwa kichwa bila kujali huyu mtuhumiwa ni kichaa au la. Ndio maana wakampeleka mahakamani akiwa na ukichaa wake 100%. Ingekuwa ni mimi nisingefanya hivyo sababu haina maana kumsomea mashitaka mtu katika hali ya ukichaa tena akiwa uchi wa mnyama. That was too mechanical!!!!
 
Utawala wa SHERIA unapokuwa kazini kwa asilimia 100 ukiondoa ile ya MAFISADI wa EPA, RICHMOND,.....
 
Unamshangaa hakimu!

Waziri yeye kamuundia kabisa Tume huyo kichaa. Tume ya watu wenye professions zao!
 
Nadhani huko waliko hawajiamini kabisa. Hakimu mzima uliye na mamlaka kisheria unapoteza muda na kuacha kazi muhimu unasimama na kumsome mashitaka mtu aliye uchi. Unaongea naye kwamba "Hutakiwi kujibu chochote kwani mahakama hii haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji" Wakati huo huyo Mtuhumiwa anaongea kivyake haijulikani nani ni kichaa hapo. Shame on you Hakimu.
USHAURI WANGU KWA HAKIMU: Kesi hii ikiitwa tena kuwa jasiri, sema hivi Mahakama hii kwa kwa uwezo ilionao na kwasababu mtuhumiwa alikuwa wodi ya wagonjwa wa akili, tunaona bado hana akili timamu kuendelea kusikiliza mashitaka yanayo mkabili. Mahakama inamuamuru arudishwe WODINI. Hakimu ukisema hivyo huyo mgonjwa atarudishwa Muhimbili kuendelea na matibabu. Vinginevyo unachofanya wewe hakimu utaingizwa kwenye vitabu vya GUINESS. Zaidi wewe ndiye KICHAA.
 
Nilisikia kuwa alileta vurugu pale mahakamani ikiwa ni pamoja na kuvua mavazi aliyovaa na kukataa kuyavaa.Hvyo ikalazimu asome mashtaka kwenye KARANDINGA(cjui ni utani au?)nway,TUUUUME hiyoooo.......
 
kwanini wasiwashitaki wale madaktari walompa nusu dozi ... i really wonder how this law works ... guy is just a victim of drug abuse caused by those people vested with power to treat others ... they are instead left out .. to continue administering their nusu doses, chop off other peoples legs and heads and also to kill pregnant women with their babies???? ... funny .. i had one time they switched even bodies .. watu wakazika miili tofauti na ndugu yao .... SICKENING .. NOT ????
 
Nilisikia kuwa alileta vurugu pale mahakamani ikiwa ni pamoja na kuvua mavazi aliyovaa na kukataa kuyavaa.Hvyo ikalazimu asome mashtaka kwenye KARANDINGA(cjui ni utani au?)nway,TUUUUME hiyoooo.......
'
Ni kweli maana wanamuonea ... angewapaka kinyesi kabisa
 
Kwenye kesi nyingi mahakimu hawa wakimuona mtu hajielezi vizuri au kuna walakini fulani huwa wanataka mtuhumiwa akapimwe akili ili kuona kama kuna umuhimu wa kuendelea na kesi.Sasa huyu ambaye tayari alilazwa baada ya daktari kuthibitisha anahitaji matibabu inakuwaje? Au ni kutaka ku-divert attention kwa uzembe ulofanyika wodini?
 
Mahakimu wetu saa nyingine hawatumii common sense. Eti kwa vile sheria inataka mtuhumiwa afikishwe mahakamani na kusomewa mashitaka ndani ya saa 24 tangia alipokamatwa basi hakimu akaitekeleza sheria kichwa kichwa bila kujali huyu mtuhumiwa ni kichaa au la. Ndio maana wakampeleka mahakamani akiwa na ukichaa wake 100%. Ingekuwa ni mimi nisingefanya hivyo sababu haina maana kumsomea mashitaka mtu katika hali ya ukichaa tena akiwa uchi wa mnyama. That was too mechanical!!!!

Mmmhhhh kweli Bongo tambarare bwana...sasa huku si kupoteza muda tu wajameni
 
Mahakimu wetu saa nyingine hawatumii common sense. Eti kwa vile sheria inataka mtuhumiwa afikishwe mahakamani na kusomewa mashitaka ndani ya saa 24 tangia alipokamatwa basi hakimu akaitekeleza sheria kichwa kichwa bila kujali huyu mtuhumiwa ni kichaa au la. Ndio maana wakampeleka mahakamani akiwa na ukichaa wake 100%. Ingekuwa ni mimi nisingefanya hivyo sababu haina maana kumsomea mashitaka mtu katika hali ya ukichaa tena akiwa uchi wa mnyama. That was too mechanical!!!!

Ujuzi wangu wa sheria ni mdogo ama hakuna kabisa. Lakini sidhani kama kuna sheria inasema kama mtu alikuwa katika wodi ya wagonjwa wa akili basi hatakiwi apelekwe mahakamani akifanya kosa la jinai.

Inabidi taratibu za kisheria zichukuliwe. Wakili wake ataitaarifu mahakama kwamba mteja wake ni mgonjwa na kuleta vielelezo. Baada ya kusikiliza na upande wa mashitaka na Mahakama ikiridhika ndipo itaamuru huyu mtu apelekwe kunakostaili. Ndio taratibu. Huwa tunapenda sana shortcut, lakini walioweka taratibu si wajinge.

Tunajuaje kama huyu mtu alitumwa kuua kule ndani na kupose kama mgonjwa?
 
That was my first reaction, lakini nikajiuliza, ukisema tutajuaje kama jamaa ni kichaa au anajifanya kichaa? Si madakatari ndo wana-prove!? Sasa huyu mtuhumiwa katokea wapi? Hospitali ambapo alishabainika kuwa na matatizo ya akili. So why the charade?
It's a coverup! Hawataki kuwashtaki madakatari, but we are getting there bcoz hakuna njia ya kuficha uzembe like in this case.
 
Naamini Pundit the fishmonger ops Law monger will deapear with conclusive mind on this saga.
In my livinghood I never seen such a high degree ya ukilaza na uvunjifu wa haki za binadamu. Najua inawezekana hayo mashtaka ni agizo kutoka juu kwani ki-haki Mgonjwa wa akili ana relif ktk sheria kushtakiwa endapo alifanya kosa akiwa ktk state au degree ya unsound-mind. I think inabidi hizi mahakama zetu ziwe makini kwa kila shauri linalokuja mbele yake au la itakuwa inashusha hadhi ya mahakama zetu.

Pia suala la mgonjwa wa kili kuwashambulia wengine ni dalili ya kutopewa huduma yakinifu zaidi ya dawa za usingizi tu. Nafahamu hilo sana kwani tulikuwa na ndugu yetu ambaye alipopagawa tulimpeleka pale hakupata tiba mpaka tulipomhamishia mwananyamala akapona kabisa.... najiuliza inakuwaje hiii????

Na hii tume ya kumchunguza mgonjwa wa akili ni sawa na kumfukuza chizi aliyenyakua nguo zako ukiwa unaoga mtoni.... Inabidi iundwe tume kuchunguza uwezo wa kufikiria wa waziri wa afya na wasaidizi wake pia....
 
Hii kweli siasa inaharibu kila fani sasa hivi sio michezo,habari,sheria na fani nyingine zimeharibiwa na siasa
Wanaachwa wauaji wazima na mafisadi kisha eti unamshitaki chizi
 
Mbona hamzungumziii na Mwakyusa kuunda tume eti kuchunguza hivyo vifo vya wagonjwa wa akili walio uawa na mwendawazimu?
Sasa tumesha ambiwa na serikali wahudumu walikimbizwa na chuma na huyo mwendawazimu alipo rudi akaanza kuwaponda wenzie.Swali hii tume inachunguza nini?Na kwa manufaa ya nani?Gharama ni za nani?Wanataka nini katika uchunguzi wao wkt wanajua kabisa yule alikuwa kichaa?Baada ya uchunguzi waziri anataka afanye nini na report ya tume?Maana tume ya makosa ya upasuaji imepotea hivihivi bila wahusika kuchukuliwa za kinidhamu.
Waziri wa Afya na Naibu wako mnapaswa kujiuzuru mmeunda tume kumridhisha nani?Mbona tukio hili mnataka mlihusishe na siasa?Tunaomba mpumnzike kazi imewashinda angalia migomo ya madaktari angalia mitambo ya kisasa inashindwa kufanya kazi mpo mpo tu hakuna hatua mlio chukua.Kaendi pembeni.
 
Hii tume imeundwa kuchunguza mtiririko mzima wa tukio,kama kuna makosa yalifanyika na nani anahusika,kuhakikisha jambo kama hili halitokei tena.Hapa mgonjwa labda litaangaliwa faili lake kuona kama dawa alizopewa ni sahihi na dozi kama ilikua sawa na vitu kama hivo.Sasa tatizo litakuja katika kutujulisha wananchi matokeo, na utekelezaji wa mapendekezo.
 
[QUOTE=khoryere;268393]Hii tume imeundwa kuchunguza mtiririko mzima wa tukio,kama kuna makosa yalifanyika na nani anahusika,kuhakikisha jambo kama hili halitokei tena.Hapa mgonjwa labda litaangaliwa faili lake kuona kama dawa alizopewa ni sahihi na dozi kama ilikua sawa na vitu kama hivo.Sasa tatizo litakuja katika kutujulisha wananchi matokeo, na utekelezaji wa mapendekezo.[/QUOTE]

Suala hili ni purely administrative. Halihitaji tume wala utume.

Toka Mwakyusa aingie madarakani keshaunda tume zaidi ya tano. Hii ni dalili ya management by crisis.
 
Kichaa ni Profesa Mwakyusa ambae kaunda tume lakini kuchukua hatua ya kumpeleka kichaa mahakamani. Ama kweli viroja. Inanikumbusha enzi za mzee Nyerere akiwa Rias alienda kutmbelea hospitali ya vichaa mirembe. Kwa ukichaa wa wenyeji wa uongozi wa mirembe wakaamua kumsalimisha mwenye ugonjwa wa kichaa ambaye wao walimuona ana nafuu. Yule mtu aliposalimishwa kwa nyerere akashangaa kwa kumwambia mzee nyerere ' Aisee kumbe wewe mwenzangu ukichaa wako ni mkubwa kuliko wangu. Kwa sababu wakati mimi nakuja hapa nilisindikizwa na askari mmoja tu. Wewe mwenzangu askari wote hao wamekusindikiza?' I hope u get my point. Huko ndiko kukurupuka.
 
wote hao ni vichaa

.... waziri aliyeunda tume inayotumia kodi ya wananchi kumchunguza kichaa
.... hakimu anayeisimamia sheria kwa kusoma shitaka la kichaa
.... polisi wanaohusika na upelelezi wa kesi ya kichaa
... serikali inayoona na kukaa kimya na kuacha pesa na muda upotee kwa suala la kichaa

ukijumlisha unapata utawala wa vichaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom