Kibwana Dachi, Mwandishi wa habari anayejua mambo mengi Tanzania

Itzmusacmb

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
1,531
1,132
Wana JF,

Leo nawaletea mwandishi wa habari wa Tanzania ambaye anajua mambo mengi sana iwe kwenye nyanja ya afya,uchumi,siasa,biashara na hata kijamii pia
Jina lake kamili ni Kibwana Mustapha Dachi ni mwandishi wa kampuni ya Africa Media Group inayomiliki vyombo vya habari vya Channel 10, C2C, DtV, CTN Magic Fm na Classic Fm

Aidha mara nyingi sana hupenda kuwepo asubuhi kwenye kipindi cha Morning Magic ndani ya Magic Fm kuanzia saa 12 asubuhi hadi 4 asubuhi,
Kama una mengi ya kuongezea juu yake ongezea.

Nawasilisha.
 
ni mbishi sana huyo bwana Kidachi kila kitu anajua yeye

Nadhani mleta mada alikuwa anayataka majibu kama haya japo katika UZI wake amejifanya kuwa smart. Nishauri tu ni vyema kama unataka kujua tabia za Mtu positive na negative basi tuache " kuzunguka " KINAFIKI na badala yake tuwe tunauliza tu moja kwa moja.
 
Ni kweli
asee mi mwenyewe namkubaligi sana hua nafuatilia sana vipindi vyake!!!na ni muwazi sana aliwahi kusema mpaka anapoishi!!ila sii vema kutaja huku anapokaa!!
 
Ni kweli
asee mi mwenyewe namkubaligi sana hua nafuatilia sana vipindi vyake!!!na ni muwazi sana aliwahi kusema mpaka anapoishi!!ila sii vema kutaja huku anapokaa!!

Hata kama utataja huko anapoishi hutakuwa umekosea hasa ukizingatia kuwa kwa rekodi ya hilo eneo inakupasa uwe na moyo wa kijasiri sana kufika huko kutokana na kwamba " masela " wote na wazee wa " ndole " pamoja na visu au viwembe ndiyo makazi yao ya kudumu.
 
Huyu Jomba yuko sawa sana namkubali kuliko maelezo. Ktk kipindi cha morning magic mvurugaji na anaejisikia yeye ni mwanzo na mwisho ni huyu Orest, nafikiri atakuwa na mfupi wa kimo maana ubishi wake unajieleza.
 
Back
Top Bottom