Kibwagizo Kipya...Mtikisiko na kuanguka kwa uchumi wa Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibwagizo Kipya...Mtikisiko na kuanguka kwa uchumi wa Dunia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Apr 7, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180

  Wimbo wetu ulio bora, ule ule wenye viitikio vingi visivyoleta maana wala mwelekeo umepata kibwagizo kipya "mtikisiko wa Uchumi wa Dunia na kuanguka kwa uchumi wa nchi Tajiri'! Naam, wanasiasa na watendaji wa Tanzania wamepata kibwagizo kipya kuwaimbisha Watanzania wimbo wa uvumilivu wa umasikini wao kwa kudai kuwa hali yetu inaendelea kuwa ngumu kutokana na kutikisika kwa uchumi wa dunia na kuanguka kwa mfumo wa fedha na mabenki katika nchi tajiri.

  Hebu tafakari, tangu tulipopata Uhuru wetu, tumekuwa tukipata kibwagizo kipya kila siku kuhalalishiwa umasikini na uduni wetu kila siku kutoka kwa watu tuliowapa dhamana ya kutuongoza.

  Tulianza na ukabaila, tukaja na ukoloni, tukaupandisha madaraja kadhaa, kama vile ukoloni mamboleo, ubwanyenye, ubepari, ikaja hekaya ya uchanga wetu, ukosefu wa wataalamu wa kutosha, ikaja unyonyaji tulioufuta kwa kutumia Azimio la Arusha, kukawa na maasi ya jeshi, uasi wa kina Kambona, kifo cha Karume, vijiji vya ujamaa, maduka ya ushirika, bei za mafuta 1974, ukame, vita vya Kagera, Makaburu, Walowezi, Manyang'au wa Kenya na kuanguka kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulanguzi, uhujumu uchumi, uhaini, mpasuko wa chama, ruksa, kutokwajibika, Benki ya Dunia, Vyama vingi, uwekezaji, kodi, mikataba ya madini, utalii, umeme wa shida, bei za mafuta, ufisadi, VAT, mvua, ukame, ubinafsishaji na sasa tunalaumu kuanguka kwa uchumi wa dunia!

  Hivi, katika sababu zote hizi, ni lini tuliweza kuamka, kujipangusa vumbi na kuanza kupiga hatua kwa kujifunza kujikinga na dhoruba kwa yaliyotukumba na kujijenga kwa uimara na kinga kama ule wimbo maarufu wa mipira ya kiume wa "Salama, chaguo la Kisasa, Salama kinga njema"? Ni lini tulijipima nguvu zetu kwa dhati na kutumia bidii zetu zote, zikiandamana na maarifa na ufanisi na fikra bora kujiimarisha kutoka umasikini na unyonge?

  Yaani ina maana katika miaka karibu 50 tangu tujitawale, bado hatujaweza kuvumbua njia bora ya kujiimarisha kiuchumi bila kulaumu wengine kwa udhaifu na umasikini wetu?

  Majuzi, mamlaka ya ukusanyaji kodi na mapato ya Taifa maarufu kama TRA, imetamka kuwa ilitarajia kukusanya mapato ya Takriban Shilingi Trilioni 2.62 katika kipindi cha miezi 6 iliyopita, lakini imeweza kukusanya Shilingi Trilioni 2.45 na kupungukiwa mapato ya Shilingi Bilioni 200.00. TRA imesema kuwa kupungukiwa kwao kukusanya mapato haya, kumetokana na mtikisiko na kuanguka kwa Uchumi wa Dunia! Nimepiga mahesabu ya haraka haraka na kubaini kuwa TRA wamekusanya takriban asilimia 94 (94%) ya makisio au makadirio ya mahesabu yao, nikajiuliza, je kupungukiwa kwa asilimia 6 (6%) ni kweli kumetokana na kusuasua kwa uchumi wa dunia? na jee mtikisiko huu utatuumiza kiasi gani kwa kupungukiwa asilimia 6 ya mapato mpaka tuanze kusema hatuna pesa za kununulia madawa?

  Nikakumbuka Serikali ilisitisha kununua magari mapya, na hili limeokoa fedha nyingi tuu, hivyo basi pengo la 6% litajiziba! Zaidi, ni kuwa Mwezi Januari ya mwaka huu 2009, mapato yaliyokusanywa na TRA yalikuwa ni asilimia 23 (23%) zaidi ya mapato yaliyokusanywa mwezi januari ya mwaka 2008! Sasa kama uchumi wa dunia ambao tunajua ulianza kuyumba mwezi wa Septemba 2008, ulikuwa ni mbaya iweje mapato ya mwezi Januari 2009 yawe makubwa marudufu kuliko mapato ya Januari 2008?

  Je Serikali yetu imewahi hata mara moja kubana na kupunguza matumizi yake ambayo mara nyingi si kwa manufaa ya Taifa? Ikiwa ripoti za Utoh, mdhibiti mkuu wa mahesabu wa Serikali zinaonyesha matumizi mabaya na kukosekana kwa uhakiki na uadilifu katika kuthibitisha matumizi au kuweka kumbukumbu za matumizi kwa mujibu wa kanuni za mahesabu na kihasibu, ni vipi leo tulaumu kuyumba kwa uchumi wa Dunia kama mapato yetu yamepungua lakini hatjali jinsi tunavyoyatumia kwa kuwa tumejijengea umaarufu wa kufuja, tunakodai "Pondamali, kufa kwaja"?

  Nikakumbuka kauli za Rais Kikwete mwaka huu 2009, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita ambapo aliashiria kuwa kushindwa kwa Tanzania kujinasua kiuchumi, kunatokana na hali mbaya ya uchumi duniani. Kwanza alitangaza kuomba stimuli kutoka kwa nchi tajiri, akisema ni lazima na sisi tupewe mgawo wa fedha kusisimua na kufufua uchumi wetu, baadaye akalaumu bei ya mafuta kuwa ghali sana na hivyo kutuangamiza kiuchumi.

  Bei ya mafuta Duniani, imeshuka tangu Julai 31 2008 ambapo pipa moja lilikuwa likiuzwa kwa Dola za Kimarekani 145, mpaka bei ya leo hii April 6 2009 ambapo pipa ni Dola za Kimarekani 52, hii ikiwa ni punguzo la asilimia 65 (65%) katika kipindi cha miezi 10! Sasa najiuliza, kama kwa miezi 10 bei ilishuka mpaka ikafika dola 33 Disemba 30 2008, iweje tuendelee kulaumu bei za mafuta kuwa ghali? Je kama bei ya mguu wa ng'ombe imeshuka, kiasi kuweza kununua miguu mitatu badala ya mmoja kwa gharama hiyo hiyo, hivi tutaendelea kulia kuwa hatuna uwezo wa kujipatia Protini za kutosha?

  Kila kiongozi na mtendaji wa Tanzania anakimbilia kuimba kibwagizo kipya, "uchumi wa dunia", najiuliza ni lini tutajiangalia ndani na kubaini kuwa hatujaathirika sana na tunaweza kupona? Nitaelewa kuwa tunaumia kama mfumo wetu huu mpya wa uchumi wa soko huria na uwekezaji ungekuwa umeshafikia hatua kuwa wawekezaji wote wameulaza na kutuachia majengo na mashimo matupo huku wao wakiwa wamekimbia na hela.

  Lakini hilo si kweli kwa kuwa tumeambiwa majuzi kuwa yale makampuni ya uchimbaji dhahabu, yalijikusanyia mapato ya Dola Bilioni 3 na Seikali yetu ikaambulia mapato ya Dola milioni 1 ikiwa ni asilimia 3 (3%) tuu! Baya zaidi kwa hawa waimbishaji wa kibwagizo kipya wanaendela kutafuta mbinu za kuwapa wawekezaji ahueni na kutupunguzia mapato. Ole Naiko katangaza wiki mbili zilizopita kuwa TRA na TIC wanaunda kamati ya kuwapa Wawekezaji mfumo bora na wa unafuu wa kodi! Astaghafulahi, leo tunalia tuna mapato duni, bado tunafikiria kupunguza mapato kwa kutoa misamaha ya kodi?

  Ni lini tutajifunza kutokana na makosa tuliyoyafanya hapo kale? Ni lini Watanzania na hasa Viongozi wetu na Watendaji watabadilisha mitazamo yao na ufikiri wao na kuanza kukubali kuwa jawabu pekee la Tanzania kuendelea si visingizio bali ni kuongeza uzalishaji mali wa ndani ambao utatokana na jasho letu na juhudi zetu na si kutegemea misaada au kulalama kuwa kuungua kwa mwingine, kumeangamiza nyanya zetu zilizo kilometa 100 mbali na kwetu na tunachokiona ni moshi angani?

  Sina maana ya kukataa kuwa Uchumi haujayumba Duniani, lakini si kweli kuwa Tanzania inashindwa kupiga hatua mbele kwa kuwa Mabenki ya Marekani yanafilisika. Serikali yetu badala ya kuweka kipaumbele kujenga mfumo mzuri na bora wa uzalishaji mali, kama vile Rwanda walivyoamka, imeendelea kupitisha bakuli kuombaomba kila kona.

  Mizengo Pinda akiwa Ireland akitembelea wafugaji na wakulima, aliomba misaada na kukaribisha wawekezaji. Je ni lini ametoa ruzuku ya maana kwa yule mkulima kule Simanjiro ili ajinunulie pembejeo au alipwe bei bora ya mazao yake?

  Viongozi wetu wamebakia kuwa mapambo, watalii na omba omba, kutwa kucha kupiga domo bila kufanya kazi wala kutoka jasho kuona kuwa kuna ulazima wa kubadilika vitendo na tabia kama tunataka Taifa letu lipate maendeleo ya kweli.

  Benki Kuu majuzi imetoa takwimu kuwa kilimo kinaingizia Taifa letu asilimia 26 (26%) ya mapato yake kutokana na mauzo ya mazao yetu. Asilimia 80 (80%) ya Watanzania wanaishi vijijini, wakijilimia kijima na zile zama za kale za mawe! Kwa nini basi kama Watanzania Milioni 30 wanaishi vijijini na takriban nusu yao wana uwezo wa kuzalisha mali, kwa nini tunaendelea kuagiza vyakula kutoka nje ya nchi na si kuzalisha kwa ziada na kuuza nje ya nchi ili tusikumbwe na mtikisiko wa Dunia?

  Marekani, Uingereza, Uchina, Ujapan na nchi zote tajiri, bado zinahitaji chakula, migahawa yao bado inauza Kahawa na Chai, inahitaji maharage, nyanya, bamia, vitunguu, viwanda vyao vya nguo vinahitaji pamba, nyumba na maofisi na watu wao wanapenda maua na matunda. Hata Kenya, Congo na Zambia, wanahitaji Chakula! Oman wanakodisha ardhi Kenya walime chakula, sasa iweje tusema hatuwezi kujikwamua kiuchumi kisa Mabenki ya Marekani yamefilisika kutokana na uzembe na ukosefu wa maadili, gonjwa ambalo ni kubwa nchini mwetu?

  Nilichojifunza kutokana na kuanguka kwa Uchumi wa Dunia safari hii, ni kuwa kama nchi yangu ni mzalishaji imara na fanisi, haiwezi kutikiswa kutokana na njaa ya jirani! Nimejifunza kuwa Watendaji wengi wetu, ama ni Wasomi Wajinga au ni Mapunguani fuata Upepo wasio na uwezo wa kukaa chini na kufikiria kwa kina njia rahisi na madhubuti za kuongeza uzalishaji huku ukipunguza matumizi yasiyo na maana!

  Leo hii Singapore, Spain na Ireland ambazo zilijenga uchumi wao kutokana na uwekezaji wa Soko huria, wamekuwa ni wa kwanza kupiga yowe la kichaga lile la "yewomi, yeleuwi", uchumi wao ukiteketea kutokana na wawekezaji kukimbia na kwenda kwenye soko la bei nafuu kuzalisha!

  Sisi tumeambiwa,tujifunge mkanda, tujikaze kiume, tuvumilie, tuhimili makali ya umasikini yanayoongezeka kutokana na kuyumba, kutikisika na kuanguka kwa uchumi wa dunia!

  Uuwi, Yewomi, yeleuwi, wimbo ni ule ule, tumepata Kibwagizo kipya, tuvumilie machungu na tunogewe na umasikini wetu kwa kuwa Uchumi wa Dunia Umeyumba na Kutikisika!
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lakini ni hao hao ambao aali walitupa moyo wakituambai hatutaathirikla sana klwa sababu uchumi wetu haujaunganika sana na uchumi wa dunia. Yaani tyunalishwa maneno na termilogies kama amauzuz
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama nilivyokwisha sema huko nyuma tatizo letu kubwa ni viongozi tunaolazimishwa kuwaweka madarakani hawana vision wala uwezo wa kuongoza ndio maana kila kukicha hawaoni aibu kwenda kwa wazungu kutembeza bakuli huku nchi yetu imejaa mali lukuki!! Matamshi yao kila wakati yanakinzana kwasababu wanatamka bila kufanya tafakuli za kina ndio maana leo utasikia hii economic meltdown haiwezi kutuathiri kwasababu benki zetu hazina ushirikiano wa karibu na hayo mabenki ya nchi zilizoendelea ; ukilaza wao unawafanya wasijue kuwa global finacial crisis hii lazima utatuathiri kwani uchumi wetu unategemea watalii kutoka ulaya na America; mazao yetu yanategemea masoko ya huko huko, kwahiyo tupende tusipende lazima tutaathirika!! Ni vyema tukajikita kuhakikisha kuwa katika kipindi hiki tunahakikisha kuwa tuna chakula cha kutosha na kwamba bandali yetu inafanya kazi kwa ufanisi ili itusaidie in the short-run. Viongozi wetu hasa muungwana waache uVasco Dagama wakae nyumbani wasimamie miradi ya maendeleo badala ya kushuhulikia ngoma za unyago!!
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Apr 7, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Tutapiga kelele weee! mchawi ni rais, msomi wa uchumi ! asiyejua hata vocabulary moja ya economy, anajua kugawa kadi za CCM!

  Rais akiwa mzuri, wengine wote watanyoka tu,

  ukitaka kuua nyoka piga kichwa!
   
 5. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ukweli unabaki palepale kuwa hiki chama hakina jipya. Hivyo inatakiwa kuanza upya kwani sasa hivi hakuna kinachofanyika zaidi ya siasa tu.

  Kuna study zilifanyika kuhusu bonde la rufiji kuna implementation yoyote? Hakuna. Yale ambayo hatuyajui ndiyo tunayakimbilia. Mfano MADINI, UVUVI na NISHATI. Vitu ambavyo vinatak maandalizi kabla ya kuingia sisi tunarukia tu. Hivyo we need new ideas from different peoples up there.
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Lakini hii economic meltdown si ndio kisingizio chetu kipya kuhalalisha umasikini wetu na ufinyu wetu kuzalisha mali?

  Sijawahi kusikia siku ambayo Tanzania hatuna kisingizio kwa nini watu wetu ni masikini au maendeleo yetu kudorora!

  Ardhi tunayo, watu tunao, maliasili na malighafi tunazo, lakini kila siku tunategemea na kuhemea kwa wageni waje kutuokoa n akuzalisha kitu kile kile tulicho na uwezo nacho na kisha hukimbilia tafuta sababu kuonyesha kwa nini hatukuweza sisi wenyewe!

  KUanguka kwa uchumi wa dunia haujatugusa sana, na hilo la kutegemea utalii pekee linaonyesha ni jinsi gani tulivyokosa dira ya kujipatia mapato! Nalo pia latumika kama kisingizio, maana sisi tunafikiri utalii ni lazima awe mzungu, na ndio maana sera yetu ya utalii inalenga Mzungu na mwindaji na si kila mtu ili iweze kukua kwa uimara!
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ..."na samaki huoza kwanza kichwani!"

  nadhani, huu ni wakati muafaka kina Professor Lipumba, Mbowe nk kuweka wazi ajenda za vyama vyao jinsi watavyounusuru uchumi wa nchi badala ya kusubiri wakati wa kampeni 2010.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Kuna wakati hufikiria pengine labda hata hizo nafasi za Mawaziri zigombewe kama Ubunge maanake imekuwa aibu tupu...au pengine Mawaziri wote ni lazima wapitishwe na Bunge ambalo pia linaendeshwa na hao hao, wachovu wa kufikiri..Yaani hata sioni ndani mkuu wangu..

  Hata kama tukifikiria Utalii, mwaka kesho tu soccer World Cup inachezwa South Afrika, nambie nchi yetu imejiandaa vipi kuitangaza nchi yetu?..Hakuna..au kuna timu zipi zimelikwa kucheza Tanzania baada ya mashindano hayo kuwavuta watalii nchini..Hakuna!..
  Je, hawa viongozi hawajafikiria kwamba kuna uwezekano wa kuwavuta watalii hao kuja Tanzania kama sehemu ya matembezi yao wakiwa Afrika!..
  Leo hii Zanzibar inapata Watalii wengi kutoka bara kuliko hata Wazungu wenyewe, kila Ijumaa watu kibao huenda kutumia Zanzibar wakarudi Jumapili, ni sababu zipi zimewavutia wananchi wa bara kwenda Unguja kila weekend?..Kwa ujumla Zanzibar wanapata Watalii wengi kwa mwaka kuliko bara kwani hata hao wazungu wanaokuja Bara wengi wao hufika Zanzibar..
  Tuna historia kubwa sana ya Utumwa ktk Afrika tukiondoa Benin, lakini tumeweza vipi kuhifadhi na kuitangaza historia hiyo..Hakuna, nani anaijua Bwagamoyo (Bagamoyo) nje ya sisi wenyewe, tena nasikia baadhi ya majengo hasa lile walilokuwa wakifungwa Watumwa kule Unguja limeuziwa mzungu ambaye kafungua madudu mengine kabisa kuifuta historia hiyo..
  Kila unapotazama mkuu wangu ni vituko vitupu, sijui tumelogwa au ndio laana!.. Wahindi (Hindu) wanaamini kabisa kwamba kuna makabila au kundi la watu waliolaaniwa au wameumbwa kuomba na huko kuomba ndio mafanikio yao, yaani kila race imebarikiwa kitu fulani na ndio destiny yao.. haiopindiki. Hivyo omba omba sio matatizo ya kujitakia isipokuwa Imeandikwa hivyo - NDIVYO WALIVYO!..
  Bila shaka sisi ni mfano bora wa imani yao na nadhani pale jamatini huwaonyesha waumini wao mifano ya hekma ya maandishi yao.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nadhani sisi ni Taifa la watu wasiotaka kusumbuka; tumeridhika na tunaridhika kirahisi mno. Halafu hatupendi kugonganisha vichwa kwani tukianza kulumbana watu wanaingilia kati; ukiwa msemaji sana utaambiwa unaharatisha amani, ukitaka kufanya maandamano watakuitia mapolisi kibao... yaani, sisi tunatakiwa kuwa kwenye huu mtumbwi na mtu asitikisike hata kama mtumbwi haunde popote!

  Mchungaji nimeipenda hii!!
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii inafanana na Mkulima mmoja wa Viazi ambaye alitoka shambani na Gunia la Viazi akafika Mjini akaliuza kwa Shilingi elfu Mbili halafu akapitia kwa Mchoma Chips akanunua Chips Mayai za Shilingi Elfu Moja Mia tano na Mia tano iliyobaki akatumia kama Nauli kurudi Nyumbani. Hii ina maana kwamba.

  1: We have Leaders ambao WANAWAZA badala ya KUFIKIRIA

  2: Badala ya KUFIKIRI ni vipi watumie Rasilimali kwa ajili ya kuzalisha na KUUZA nje wao WANAWAZA ni nani wamkabidhi Rasilimali Azalishe ATUUZIE.

  Hivi Tanzania pamoja na Mapori yote leo hii Kuna Watu huko Karatu wanakufa Njaa,jamani hii ni Laana kabisa.

  This is a country ambapo hata Tundu la Choo sha Shule ni Mpaka tupate Mwekezaji au Mfadhili kutoka Ulaya.

  Hivi wameshakaa wakajiuliza Wamefanya nini na

  1: Maziwa na Bahari ambayo yameizunguka Nchi yetu, Hivi hawajui kama ni Makazi ya SAMAKI
  2: Mito itirrikayo karibu kila kona ya Nchi kwa Mwaka Mzima, How many IRRIGATION Schemes do have in our Country? Tunasubiri Mwekezaji aje Alime Mahindi, Mpunga, Maharage.
  3: Tuna MBUGA Ngapi wa Wanyama, hivi wameshawahi kujiuliza ni Watanzania wangapi hawajahi Kuona Simba au hata Tembo, je Ni Watalii Wangapi wa Ndani Wanaotembelea Vivutio vyetu? Kama ni Wachache Kwa nini? Au wayalii ni Wazungu tu?
  4: MINING SECTOR, Ni ni tunapata kutoka kwa hawa wawekezaji? Si ni Bora tungewapa Wachimbaji Wadogo ambao wangeiuzia Serikali Madini nayo ingekuwa ni Exporter Mzuri wa Madini hayo. Serikali ingeweza kuwa na Centralized Ghala kwa ajili ya Kununua Madini kutoka kwa Wachimbaji wadogo.
  5: VIWANDA, Ndugu zangu hakuna nchi Duniani ambayo imeendelea out of Production Industries, sisi badala ya kuendeleza Viwanda tumeua. Tunalima Pamba so why should we export Clothes from outside? Tuna Madini CHUMA so why should we export Zana za Kilimo? Tuna Gold, tuna Almasi kwa nini tuagize Cheni na mikufu kutoka China?
  6: Tuna bandari ambayo Nchi nyingi zinaitumia kama Zambia, Malawi, Congo, Zimbabwe but Bandari yetu ni Pango la Wezi la Wezi Wajulikanao na Viongozi wetu.


  Hivi ni nini Ambacho hatuna Jamani? If we have everything tatizo ni nini? Tumerogwa? Or May be Watson wa Right!
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ndege ya uchumi,

  Nitasema Shabash! maana huo mfano wa mkulima wa viazi, ndio taswira halisi ya taifa letu!
   
 12. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hapa Kichwa cha jipu kilipo.

  Na hakuna namna nyingine ya kulitibu zaidi ya kulitumbua hapo hapo.

  Nimemuangalia na kumfuatilia kiongozi wangu mkuu kwa makini kabisa. Nikaruduia tena na tena kufuatilia na udadisi mkuu kuona kama anaamini nini katika swala la na dhana nzima ya KUJITEGEMEA kwa kweli imenikatisha tamaa.

  Huu msamiati hauko kwenye fikra, hisia , ufahamu au kauli yake. Is completely incompatible na hili.

  Hana undani wowowte wala chimbuko la kuelewa kuwa HUO ndio msingi wa UTU na UHURU wa kweli wa mwanadamu kuanzia mtu mmoja, familia na jamii yeyote. Haoni na haelewi kuwa maana ya kiogozi ni kuogoza mtu akajitegemee kwa kila hali na hata ikipi kutokumhitaji kiogozi. KUJITEGEMEA huku hakuoni kabisa na hakuna mkakati wowote wa kutuelekeza huko.

  Ndani ya ilani ya chama chake hakuna hata harufu ya dhana hii...Ilikuwapo sijui nini kimewaigia na kuitupiliambali....AIBU KUBWA!!!

  Nimefikiritena sana huu ogonjwa kaupta wapi au nana kamuambukiza na wapi vijimelea vyake vilipo?

  Nikajiwa na majibu.

  1. Labada walichoka matamshi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea kwa kuwa tu pale mwanzoni ilikuwa haijakomaa na hivyo tukakosa vipodozi, suti na vipoozea vingine?Hili Limewapotosha na kutoona picha kubwa ya mchakato. Labda hili limekuwa ni mwiba makali kwa viogozi wengi na yeyote angepata UONGOZI angekimbiza viji mitumba ya magari, vigauni na viposho vya wahongaji wakubwa wa dunia hii...na hivyo kuididimiza nchi..na kiwekea mtizamo wa kuikwepa kwa kila hali dhana ya kujitegemea.

  2. Kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na kuzoea kuruka huko na huko ianakuwa adictive kiasi ambacho ..iankuwa ndio sera ya chama na taifa...?


  LAKINI

  Mtikisiko wa hao wanao Tulisha sisi na wake zetu umewatikisa hata wao?

  HATARI?

  Ni kuwa tusipokuwa macho tutapoteza wake na binti zetu maaana wanajua aliyekuwa anatulisha na sasa Hawezi kutulisha tena...Akiwaiti wake na Binti zetu akawalishie nyumbani kwake na sio kwetu..wasiende? Huu sio utani hali ni tete kuliko tunavyochekeana chekea hapa ..tunapoteza familia jamii na Nchi!!

  Tukae chini tuangalie kama Kiasi gani Tunaweza kuendelea kufikiri Tunweza kuendeshewa familia zetu kutoka Ulaya na amrekani ...mpaka lini.

  SI UTU wala UBINADAMU kwa familia yako na Taifa Kushibishwa kwa kiwango cha 46 asilimia toka kwa Wanaume wenzetu!!!! Si jambo la kujivunia na kupigiwa makofi hata kidogo...Kwa kupitisha libakuli kila kona ya dunia kwa visingizio vya kijinga ...na hata vingine kuitwa vya kusomi. Usomi wa kiakili ni tofauti na usomi wa kiutu. UTU kwanza na mambo mengine baadaye.

  Hao wanaume wanatushinda nini?

  Shame ..shame.....shame.....!!!!
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ya G20 na utegemezi wa Kikwete!

  Johnson Mbwambo Aprili 8, 2009


  Source: Ya G20 na utegemezi wa Kikwete!
   
Loading...