Kiburi si maungwana

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,313
10,017
SIKIA
Bissmillah naanza, kwa jina lake manani,
Kwa maneno nakufunza, na wala sina utani,
Umeshageuka funza,kutukuza ushetani.
Ewe kiumbe sikia, yalo mazuri chukua.

Unaliza waungwana, kwa kuupenda ubwana,
Wasababisha tosana, badala ya kuungana,
Kila Mara kutishana, raha kwako kuuana,
Ewe kiumbe sikia, yalo mazuri chukua.

Wafanya hofu tawala, mwenye akili ni wewe,
Umbwa wadogo wawala, kwa kutaka sujudiwe,
Vyote shaghalabaghala, twahitaji tuachiwe,
Ewe kiumbe sikia, yalo mazuri chukua.

Umeshachokwa na wote, tatuingiza vitani,
Ukisemwa na yeyote, namuweka matatani,
Fikra zako zi kiwete, mithili ya punguani,
Ewe kiumbe sikia, yalo mazuri chukua.
 
huko nyuma mlisema,tumemchoka muungwana!
sasa kaja mjuza,hamtaki mwatukana!
hebu acheni mapuuza,nchi msije iuza
kama pumzi yawabana,pumulieni hata uvinza!

kiburi si muungwana,upole mliutukana!
mlishiba titi la mama,na mlimfunga ndama!
naye bila hiyana,alikula majani kwa sana.

usiempenda kaja,uliempenda kafa!
uliemtenda kaja,aliekutenda kafa

shubiri ya mshubiri,hakuja kwa mahubiri
wandani msitiri,nje kuna utitiri
bila kufikiri,utamdondosheapilipili

usiempenda kaja:D
 
Bwana mkubwa Farao,duniani amepita
Hasimu miongoni mwao,hakuna wa kumpita
Amekwenda na mwambao,wakati umempita
Wakati ukishafika,mauvo yatajalipwa.

Umejivikaje mwao,eebwana mfikirika
watupiga dafarao,sio wako washirika
Tukikosoa mwendao,si uzalendo wa rika?
Wakati ukishafika,Matendo yatajalipwa.
 
Back
Top Bottom