Kibosile wa wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika mashahriki ajisalimisha polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibosile wa wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika mashahriki ajisalimisha polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Oct 20, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti wa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki - EAC - jana alijisalimisha kwa polisi kutokana na kutoa kauli ya uzushi na yenye kudhaniwa ilikuwa ya kichochezi pale alipodai mmoja wa wastaafu hao aliyemwagiwa maji moto yenye kuwasha sana maarufu kama "maji pilipili" alikuwa ameuawa na maji hayo.

  Baada ya mzushiwa ufu huyo kuibuka na kudai maji hayo yalimpa madhara madogo tu lakini hayakumuua basi polisi walianza msako mkali wa kumtafuta kibosile yule wa EAC ili wamfikishe kwenye mahakama kwa uchochezi na uzushi.

  Kibosile tajwa alijisalimisha polisi na kukiri ya kuwa taarifa zake hazikuwa sahihi na hivyo aliomba msamaha.

  Haikufahamika mara moja kama polisi wataendelea na hatua zao za kumfikisha mahakamani au wamemsamehe. Lakini afande Kova ambaye ni mtu wa busara sana ninahisi atakuwa amemsamehe ili mradi asirudie tena kutoa taarifa ambazo hana uhakika nazo...............
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Huu ni mtego ulio backfire kwa CCM....walipanga hii kitu ili Dr Slaa aingie kichwakichwa halafu wamlete huyo Mzee hadharani ili Dr AONEKANE MZUSHI
   
 3. m

  mbea Member

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo naye ni Chedema for-RAM.
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  tupe ushahidi wa hili, au na ww ni wlwl?
   
 5. minda

  minda JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hivi ni kova ndiye anayetakiwa kusamehe au mahakama. mi nionavyo kazi ya polisi ni kusimamia sheria na si kufanya kazi za mahakama. huyo kibosile anatakiwa kusamehewa na mahakama; hapo ndipo haki inaweza kupatikana.
   
 6. Butterfly

  Butterfly Senior Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  MWENYEKITI wa Kamati ya Wastaafu wenye madai wa iliyokuwa Jumua ya Afrika Mashariki, Nathaniel Mlaki, akisindikizwa na polisi kwenda kizimbani katika Mahakama ya Hakim Mkazi,Kisutu, Dar es Salaam, kujibu kesi ya kufanya vurugu, katika barabara ya Kivukoni, mjini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

  [​IMG]

  MWENYEKITI wa Kamati ya Wastaafu wenye madai wa iliyokuwa Jumua ya Afrika Mashariki, Nathaniel Mlaki, akipanda 'defender' la Polisi kwenda rumande, baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

  Mi ni likuwa naongezea msisitizo tu
   
 7. m

  mbea Member

  #7
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kapewa dhamana ya watu 2 kila mmoja kasaini dhamana ya tsh.500,000/-hivyo jamaa yupo nje kuendelea mapambano aliyotumwa na chama fulani yeye na wenzie Tamwa,Tgnp n.k
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Wewe kaa ukisubiri ushahidi...habari ndiyo hiyo...huyo Mlaki hatafungwa wala nini...subiri muda tu
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  .kwa ww asipofungwa maana yake walimtuma?!. Kwani ni lazima kila mwenda mahakamani afungwe?!
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Hayo ni yko wewe.....kwa mujibu wa Kova ni mhalifu lazima afungwe...asipofungwa tafsiri utakavyo
   
Loading...