Kibosile amfumania mkewe akigawa tunda nje ya Ndoa!...check photos | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibosile amfumania mkewe akigawa tunda nje ya Ndoa!...check photos

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Boflo, Jan 27, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Gazeti ‘Very Classic’ kwa habari za kufichua maovu ya chini ya zulia, Risasi Jumatano, lipo kamili kuanika kila kitu, jinsi mtego ulivyoandaliwa mpaka fumanizi ambalo lilichukua nafasi kwenye Gesti ya Makanya, iliyopo Manzese Uzuri, Dar es Salaam.

  Mtoa habari wetu alieleza kuwa fumanizi lilifanyika baada ya mume wa Eliza, Hamis Bashaija kuanza kunusa ‘harufu mbaya’ ya usaliti ndani ya nyumba yake ambapo alisoma dalili na kupata hisia kwamba mkewe anagawa zabibu zake kwa mwanaume mwingine.

  Mleta ‘niuzi’ wetu anaendelea kumwagika kuwa kutokana na kuhisi mke wake anatoka na mwanaume mwingine, alianza kufanya uchunguzi mpaka alipobaini ukweli, hivyo akaandaa mtego wa kumkamata ‘mbogo’ wake.

  Alisema, Hamis na Eliza wanaishi maeneo ya White Inn, Sinza Kijiweni, Dar es Salaam lakini ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawia, ilimlazimu mume kupanga safari ‘feki’ ya kwenda mkoani Singida kwa lengo la kumhadaa mkewe na kumkamata kwa urahisi.

  Mnyetishaji wetu aliendelea kusema kuwa Januari 23 mwaka huu (Jumamosi iliyopita) asubuhi, Hamis alimuaga mkewe kwamba anakwenda Singida kikazi na kuacha mahitaji yote muhimu ambapo Eliza alimtakia safari njema.

  “Ilipofika jioni Hamis alimpigia simu Eliza na kumueleza kuwa amefika Singida, Eliza akampa pole kwa safari,” alisema mleta niuz wetu na kuongeza:

  [​IMG]

  “Kumbe Hamis alikuwa amejificha mtaa wa pili kutoka nyumbani kwake na alikuwa ameweka mitego kufuatilia nyenndo za mkewe. Aliweka mashushushu ambao muda wote walicheza na safari za Eliza kisha wakawa wanampa taarifa jamaa.”

  Mleta niuz wetu anaendelea kupayuka; Ilipofika majira ya saa 12:30, mtego ulianza kuonesha matumaini baada ya mashushushu kubaini kwamba Eliza alikuwa anaupara bila kujua anakoelekea.

  “Alipomaliza kuupara, taratibu kwa mwendo wa kinyonga huku akiikanyaga ardhi kwa kudonyoa kama siyo kunyata, alivuka daraja na kuingia Makanya Guest ambayo ipo jirani kabisa na nyumba anayoishi na mumewe.

  “Alipofika hapo, Eliza alikutana na njemba aliyenaswa naye, wakatulizana sehemu moja iliyokuwa na mwanga hafifu, hapo wakaanza kunywa mvinyo. Walipokolea kilevi, walikodi chumba namba 26 kwa ajili ya kuichinja amri ya sita.

  “Wakati hayo yote yanafanyika, kila hatua ilikuwa inafuatiliwa na wapambe wa Hamis na ilipofika hatua ya kuingia chumbani, timu nzima akiwemo Hamis mwenyewe waliizingira Makanya Guest na kuingia chumba husika.

  “Waliingia chumbani bila kumuuliza mtu, walisukuma mlango kwa nguvu, ukaitika, wakawakuta wote wakiwa wamevaa nguo za ndani, hapo ikawa inaonekana wazi kabisa kuwa walikuwa wakikaribia kuifumua fumua amri ya sita.

  “Baada ya hapo, ikawa ni piga … piga … yule jamaa aliyenaswa ugoni alipigwa mno na wapambe wa Hamis ambaye naye alimpa kipigo cha aina yake mke wake na matukio yote hayo yalikuwa yanarekodiwa kwa picha.

  “Kutokana na kuzidiwa na kipigo, mgoni huyo alichoropoka na kutokomea akiwa na nguo ya ndani, huku nyuma Hamis alimchukua mke hadi nyumbani kwake na muda wote Eliza alikuwa anaomba msamaha kwamba harudii tena.”

  [​IMG]

  Risasi lilipopata habari hiyo pamoja na picha, kesho yake (Jumapili), lilituma paparazi wake kwenye gesti hiyo na kuongea na meneja aliyejitambulisha kwa jina la Said Omari, ambaye alikiri tukio hilo kutokea lakini akadai hana maelezo kwa sababu hakuwepo.

  SAKATA LINAENDELEA…
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ""Gazeti ‘Very Classic’"


  mhh....
   
 3. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hahahahaha!
   
 4. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Sasa huyo mwanaume aliyeweka mtego wa fumanizi ndio kaambulia nini? Pressure tu na aibu ya mwaka!
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  hicho chanzo cha habari mie ckiaminigi/kubali kabisa....
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  "no comments"
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280
  mi ssijaona ubaya
  angekuja na shahawa za huyo mwanaume sawa lakini umeomba kusafiri unasaidiwa unapiga aaaaa nt fair
  Geoff r comments pls
   
 8. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Huyo Hamisi kafumania. Kwa hiyo huyo mkewe bado anaye tu? Kama anaye na anampenda sasa kamuaibisha ili iwe nini. Otherwise hakuwa na sababu za kuingia gharama zote hizo angeachana naye au avumilie tu. Kupenda kuna gharama sana
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hayo ndiyo mambo ya BWABWA!

  Gazeti "Very Classic" ni Risasi Jumatano?

  Ukistaajabu ya Mussa....
   
 10. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  yukkkkhhh....
   
 11. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  |Classic kwa ma-bwabwa mtepeto
   
 12. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aaaarghh..
  Hizi habari za kutunga tu!! Hao watu hawa exist au wamelipwa watoke gztn kwa hbr fake!! Kwa kweli mi binafsi zinaniboa mana hata uongo unatakiwa uwe na creativity fulani lol..but Same design kila cku!! Ndo kama wale walowai tolewa kukamatwa uchawi kumpaisha mganga na wakakili kuwai piga pia za fumanizi fake!! Ujinga mtupu..aaargghhh...
   
 13. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  hapo ndipo huwa cyaamini hivi vyanzo vya kidaku.....srori yenyewe kama anawacmulia watu wa vijiweni.
   
 14. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wengine wanamwagia mdomoni sasa kama hajui atang'amua vipi? Huenda huyo mwanaume anampiga tiqo ndo maana demu kampenda
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Jan 27, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Paparatzzi hawakuwepo eneo la tukio aliyepiga picha na kuzipeleka kwao ni nani kama wapambe walikuwa buzzy na mgoni na mume akiwa buzzy na mkewe? Ah amejiaibisha mwenyewe Bwana Hamis

  Pili hata kama amemfumania mkewe kwa nini ampe kipigo cha mbwa mwizi? Umenikuta na kosa huna haki ya kunipiga hata kidogo nichukue nipeleke kunakohusika unanipigia nini? Ningetoka na kipande cha sikio.

  Na we Eliza, nyambafu zako!! kwani hiyo ilikuwa ya dhahabu?
   
 16. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Bwabwa unapenda mambo kama haya....lol

  Mimi nahisi hawa watu wa magazeti ya udaku wanatuchezea akili tu!

  Qn1. Mbona hizo picha kila matukio wanakuwa wanafumwa wakati wakiwa wanakaribia kula tunda?

  Qn2. Mtu ukimfumania kweli unamkuta kwenye hali kama hiyo? eti anafunika manyonyo vizuri kabisa?

  Qn3. Inakuwaje kila anayeingia gesti na mke au mume wa mtu hawafungi mlango na ufunguo?

  Qn4. Ina maana milango ya gesti ni vimeo kiasi cha kusukuma kwa mguu na mlango unafunguka?

  Qn5. Hao watu wanaofumania wanajua vipi muda na dakika ya fumanizi? Kwanini wasifumanie wakati wawili hao wakitoka? bali wanafumania dakika chache kabla ya kuanza kula tunda?

  Note: Mimi nahisi hizi habari ni za kutunga tu. Biashara imani!

  Chanzo: gonga hapa!
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  hapa nimeshindwa kukomenti
   
 18. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dah hii kwa Dunia ya sasa watu wanamalizana palepale!! si unajua tana Hasira za kumegewa mke!!
   
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  Jan 27, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sawa sasa mimi kama mke ukishanipiga ndo nichukulie kuwa meshaniadhibu na kesi imekwisha tunarudi kuendelea na maisha kama zamani? Sio unibonde halafu bado unipeleke Bakwata sijui au unipe talaka. Nitakutafuta mtaani nikulipizie kweli!!
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280

  subiri aliwe wako ndio utajua awa watu wanatunga
  aku mi sitakagi hata kujuana nao
   
Loading...