Kibonzo: Kweli tozo za miamala huenda ni kazi bure?

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
5,262
12,835
Ukiangalia kwa makini kibonzo cha Masoud kipanya unafikilia mengi, nikama kodi zote zinazo umiza wana nchi, hazitafaidi nchi hi paka pale watakapo ziba matundu yanao vujisha maji.

Wewe umeelewaje hili litakua na ukweli wowote

Kipanya.jpg
 
Tumekusanya tozo 49bn hizi zitaenda moja kwa moja kwenye miradi ya maendeleo, Baada ya week 1:

1. Ubadhirifu wa 126bn, vigogo kisutu.
2. Waziri mkuu ang’aka 46bn zaliwa.
3. Mkandarasi kisutu kahujumu 270bn.

Sisi tunafanya tu Kazi kwa bidii, wacha watuibie, waibie Mama zetu kule Tandahimba, watoto wetu vyuoni, sie twawashtaki tu kwa Mungu.
 
Tumekusanya tozo 49bn hizi zitaenda moja kwa moja kwenye miradi ya maendeleo, Baada ya week 1:

1. Ubadhirifu wa 126bn, vigogo kisutu.
2. Waziri mkuu ang’aka 46bn zaliwa.
3. Mkandarasi kisutu kahujumu 270bn.

Sisi tunafanya tu Kazi kwa bidii, wacha watuibie, waibie Mama zetu kule Tandahimba, watoto wetu vyuoni, sie twawashtaki tu kwa Mungu.
Dua la kuku bro!
 
Wananchi wanachangishwa za kizalendo kulijaza pipa, wakiamini kuwa ipo siku pipa litajaa. Maji miguuni mwao pengine ni yale yanayomwagika wakati wakijaza pipa wasijue kuna matundu upande wa pili tena chini chini kabisaa, hakuna wa kuyaziba kwakuwa yatatirirshia kuliko lengwa
 
Hii picha navyowaza mimi.

Kwanza yanaonekana maji yaliko ndo hayo hayo hukazaniwa kuyajaza kwenye pipa. Na sehem yenyewe sio chanzo cha maji na Panaonekana pakame(Hali ni mbaya kitaa).

Ila maji yaliyoko kwenye pipa ndo maji yanayochuruzika na muda huo huo wanayarudisha kwenye pipa ni watoto(nguvu kazi au tuseme vijana) na nikupitia watu wote yaan ki vyama kwani vinarangi ya kama chama Chadema na ccm.

Ila kwa yanayochuruzika na kuelekea nje wanaonekana watu wazima wakiyabeba . Ni kama neema kwao kupata maji(hapa ndo hzo tozo kama kweli zitaenda tumika kwa usahihi) Kama walivyodai kujengabarabara na vituo vya afya.
 
Back
Top Bottom