Kibonzo cha Gado: Magufuli embracing with foreign opposition while harassing opposition at home

Ni upotovu wa uelewa! Mara ngapi tumeona wapinzani wakisimama kwenye majukwaa ya Magufuli? Magufuli kateuwa wapinzani kwenye serikali yake. Hayo yote mchora vikaragosi hayaoni. Nachelea kusema ana maslahi kwenye ufisadi wa nchi.
Hivi mrema ni mpinzani? si yeye na yule wa Zanzibar hamad Rashid ndio wamepewa vyeo kwa serikali ya ccm
 
Wapinzani gani aliowateua..kina Mrema?? Kwani kusimama kwenye majukwaa ya CCM ndo nini? Kwa nini asiwaache wapinzani wasimame kwenye majukwaa yao wenyewe. Uwe na soni angalau kidogo mkuu!
Wangekuwa na jambo la maaana wasingetoka bungeni. Wanataka kumtoa Mkulu kwenye target ili wapate kuongea kuwa hajatimiza ahadi zake. Kama wana jambo la maana watalisemea bungeni.
 
Thanks indeed mleta Thread na Mchora KIBONZO hakika ujumbe umefika pa husika sawia bin sawia.
 
akihutubia Dodoma mkutano wake wa kwanza baada ya kuteuliwa ilani yake ya kwanza ni kuvifungia vyama vya siasa makumbusho. pia yeye husema tanzania hakuna upinzani
 
Wangekuwa na jambo la maaana wasingetoka bungeni. Wanataka kumtoa Mkulu kwenye target ili wapate kuongea kuwa hajatimiza ahadi zake. Kama wana jambo la maana watalisemea bungeni.
Hivi hukuwahi kuona jinsi hotuba mbadala za upinzani zilivyokuwa zinahaririwa ili ziipendeze serikali na chama tawala? hii ilikuwa aibu kubwa sana. Tuacheni unafiki jamani
 
Ina maana huyo mchoraji kiroho na kiakili na kimaslahi na kiupendo ni Mkenya ila kiuhasilia ni Mtanganyika mpeni pole sana sijawahi kuona mchoro wake wowote positive kuhusu Rais wetu "la haula" Mtanzania Mkenya au ndio hawa wanaitwa Diaspora????? Looh
Kwani huo mchoro ni negative ?
 
Back
Top Bottom