Kibongo bongo iPhone ni taashira ya hadhi au?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,641
Nianze na fasili kwanza maana wengi wenu nyie 'millennials' hamjui lugha. Iwe Kiswahili au Kiingereza, hamko vizuri kivile. Ni wababaishaji tu:D.

Taashira maana yake ni ishara/ au dalili. Naamini mnajua maana ya ishara na dalili.

Sasa kuna jambo nimeliona ambalo ningependa kusikia maoni ya wengine kulihusu.

Hivi hapa bongo iPhone ni ishara ya hadhi [ya juu]? Nauliza hivyo kwa sababu nimeshapigwa sana mizinga ya 'Ngabu naomba niletee iPhone basi...hata kama ni iPhone 5 au iPhone SE'.

Kwa nini iPhone kwa sana na si Samsung, LG, Motorola, au zinginezo?

upload_2017-11-17_8-51-25.jpeg
 
Ni ukweli kwamba iphone ndo simu zina bei mbaya sana, kama nikiona mtu ana iphone najua ametumia hela ndefu kununua hiyo iphone.

So, ninachofanya napiga hesabu za haraka haraka kwamba kama anaweza kutumia 1M+ lazima atakuwa na kipato kizuri sana, kwa sababu ninaamini hawezi kukopa kwenda kununua simu.

Mimi nina tecno w3 ya sh 180,000, siwezi kujilinganisha na mtu wa iphone.
 
Yani kitendo cha kuianzisha thread hapa JF tayari ushaipa status ya juu kabisa,kwakweli iPhone mahaba yake sio ya nchi hii kwanza lile tunda pale nyuma wacha weeee,kingine ukishika mahala pako na watu wengi tayar watakupa status yako kua we sio mtu wa sport sport kingine ukianza tumia iPhone huwez acha ina levya zaidi ya cocaine TEAMAPPLE. Mahaba to the moon and back.
 
IPhone ilisababisha nikaachana na demu wangu nilimnunulia Samsung, baada ya miezi sita nikanunua Techno akaa nayo mwaka nilipopandishwa kazi taasisi fulani ya kimataifa akasema nimnunulie iPhone ili tubadilishane ksb simu yangu ilianza kusumbua nikasema sawa...lakini sikuwa na wazo nikafikiria nitoe 1m plus wkt mama yangu hana kilinuka sana akasema hawezi kuwa na mwanaume nae ahidi sitimizi akaa baada ya mwezi akarudi anaomba nimsaidie helaso kila nikiona neno iPhone nakumbuka sana tukio hilo nacheka sana zinawatoa roho sana hao viumbe wa kike
 
Yani kitendo cha kuianzisha thread hapa JF tayari ushaipa status ya juu kabisa,kwakweli iPhone mahaba yake sio ya nchi hii kwanza lile tunda pale nyuma wacha weeee,kingine ukishika mahala pako na watu wengi tayar watakupa status yako kua we sio mtu wa sport sport kingine ukianza tumia iPhone huwez acha ina levya zaidi ya cocaine TEAMAPPLE. Mahaba to the moon and back.

Ama kweli USA kiboko yao!!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom