Kibondo, Kigoma: Majambazi watishia amani, Wananchi waishi kwa hofu

gwankos

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
324
419
Habari zenu wana familia ya Jamiiforum,

Poleni na majukumu yenu ya kutafuta mkate wa kila siku japo kwa wakazi wa Kibondo mkoani Kigoma hali si shwari hasa kwa Wale wananchi ambao hujitafutia riziki yao kutokana na kuporwa na majambazi hadi kupelekea vifo kwa baadhi ya wananchi.

Wilaya Kibondo ipo Kusini mwa mkoa Kigoma ambapo kumekuwa na matukio ya UJAMBAZI ya kujirudia rudia hasa kijiji cha Busunzu ambapo Wananchi wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na kuvamiwa kila mara wengi wameporwa mali zao, pia abiria nao wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo hasa katika pori la mto Malagarasi na pori la Nduta

Kumekuwa na Majambazi ambao huteka kila Mara wajisikiapo na Hakuna hatua zinazochukuliwa zaidi ya familia za wahanga kuishi kwa hofu huku wakitanga tanga kila kukicha inasikitisha sana. Mfano kuna Mzee mmoja alitekwa na majambazi na kuondoka nae ilikuwa tarehe 13 mwezi wa kwanza 2019, tukio la pili likatokea kesho yake ambapo gari aina ya hiace ilitekwa na mkulima mmoja kuporwa pesa zake alizo kuwa ameuza mpunga wake pale Busunzu.

Imekwenda mbali zaidi baada ya wiki kama mbili mfanyabiashara mmoja maarufu Kama Nick (mmiliki wa M-pesa) alitekwa majira ya saa moja usiku katikati ya mji kwa wenyeji wa Kbondo ni sehemu ya Station One, tukio jingine wiki moja iliyopita hapo hapo Kibondo majambazi waliteka maeneo ya Kumwayi kisha usiku huo huo walienda Kijiji cha Bitare na kupora kwa mzee mmoja na kusababisha kifo cha mzee huyo huku familia ikibaki na simanzi,masikitiko makubwa sana.

Wananchi wameshindwa kupaza sauti zao na kushirikiana na Jeshi la Polisi kutokana na baadhi ya Askari kutokuwa waaminifu na wazembe wa kufuatilia au kuzifanyia kazi taarifa wanazopewa kabla ya matukio kutokea. Wanachi wanashindwa kufanya shughuli zao kwa amani kutokana na hofu iliyotanda kila kona na kupelekea shughuli za maendeleo kukwama, nadhani ni wakati sasa kamati ya ulinzi na usalama kujitathimini kwa kile kinachoendelea hapa Kibondo.

Tunaomba mkuu wa Jeshi la Polisi na Waziri husika kuliangalia hili jambo kwa jicho la tatu maana hali si shwari kabisa hapa Kibondo. Familia za watu zinatanga tanga kwa hofu kubwa sana huku wakilala kwa kuhama hama kila kukicha, ndani ya nyumba zao hapakaliki kwani majambazi huteka na kurudi mara kwa mara, mfano kwa Eliud Bendiliba amevamiwa zaidi ya mara mbili

Bwana shamba wa kijiji cha Busunzu, Mzee Edward Denja ambae alitekwa na kuondoka na majambazi lakini Mungu alisaidia akarudi, yupo mfanyabiashara mkubwa maarufu kama Mashaka amevamiwa zaidi ya mara mbili Pia.

Kuna baadhi ya vocha za halotel ziliokotwa na wananchi katika misitu ya sanganyama wakati wakimtafuta huyo mzee alietekwa, ambazo watalamu WA TEHAMA kitengo cha Polisi mnaweza kuzitumia vocha hizo kutafuta waharifu kushirikiana na kampuni ya Halotel kama kweli mpo seriously na vocha hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa kituo cha Polisi Busunzu

Vile vile kuna simu ziliporwa na majambazi hao ambapo wahanga na wamiliki wa simu hizo wana Imei za simu hizo ambapo zinaweza kutumika kuwatafuta waharifu hata kama WataFlash au kureset simu hizo kuna uwezekano wa kuwatrack kupitia imei za simu kwa wataalamu wa TEHAMA wanaelewa.

Tafadhari wenye mamlaka na dhamana katika suala la kuhakikisha raia anaishi salama na mali zake tunaomba msaada wana Kibondo tumechoka kuishi kama wakimbizi ndani ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkitaka kupata msaada wa haraka semeni kwamba majambazi hao wanatumwa na chadema, baada ya wiki moja ujambazi utakuwa umeisha wilaya zote za kigoma ikiwepo kibondo
 
Simple sana mkitaka polisi waje alikeno viongozi wa kitaifa wa CHADEMA itisheni maandamano makubwa ya kumpongeza Tundu Lisu. Tutaleta jesi kabisa litakaa hukohuko ujambazi utabaki hisitiri.
Sio jambo la kisiasa ndugu kuwa srz basi huku mambo ni magumu Sana ikifika usiku hofu hutanda kila kona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana aise,

Majambazi wasikie tu ,nilisha chezea bakora za kutosha pori la nduta ilo sina hamu nao,

Busunzu hapo si kuna kituo cha polisi lkn mkuu?

Pori la nduta ilo si kuna geti wanakaa Polisi kwenye kona zile?

Nduta wale Polisi wakambini si bado wapo wakutosha gari na mafuta wanapewa na UNHCR?

Kuna uzembe mkubwa sana basi, kama majambazi wanapiga tukio Station One pale saa Moja jioni na wanatoka salama kazi ipo,
 
Hivi kumbe kuna baadhi ya maeneo ndani ya nchi hii ujambazi bado upo kwenye awamu hii ya tano? Kwa kweli huku kwetu tumeshausahau, na imani tatizo hilo litakwisha mda mfupi uzi huu ukisomwa na wakuu. Mimi na ungana na wewe kunabaadhi ya askari sio waaminifu na sidhani kama wananafadi awamu hii. Poleni sana watu wa Kibondo.
 
Kituo cha polisi kipo Busunzu, mkugwa, kifura pia nduta lkn Sana wanadeal na wauza gongo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kumbe kuna baadhi ya maeneo ndani ya nchi hii ujambazi bado upo kwenye awamu hii ya tano? Kwa kweli huku kwetu tumeshausahau, na imani tatizo hilo litakwisha mda mfupi uzi huu ukisomwa na wakuu. Mimi na ungana na wewe kunabaadhi ya askari sio waaminifu na sidhani kama wananafadi awamu hii. Poleni sana watu wa Kibondo.
Nasi tunaomba wenye mamlaka wapate ujumbe na waufanyie kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamati ya ulinzi na usalama walishindwa kudhibiti ujambazi sasa matokeo yake yanazidi kuwa mabaya zaidi baada ya baadhi askari kujeruhiwa vibaya sana
Habari zenu wana familia ya Jamiiforum,

Poleni na majukumu yenu ya kutafuta mkate wa kila siku japo kwa wakazi wa Kibondo mkoani Kigoma hali si shwari hasa kwa Wale wananchi ambao hujitafutia riziki yao kutokana na kuporwa na majambazi hadi kupelekea vifo kwa baadhi ya wananchi.

Wilaya Kibondo ipo Kusini mwa mkoa Kigoma ambapo kumekuwa na matukio ya UJAMBAZI ya kujirudia rudia hasa kijiji cha Busunzu ambapo Wananchi wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na kuvamiwa kila mara wengi wameporwa mali zao, pia abiria nao wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo hasa katika pori la mto Malagarasi na pori la Nduta

Kumekuwa na Majambazi ambao huteka kila Mara wajisikiapo na Hakuna hatua zinazochukuliwa zaidi ya familia za wahanga kuishi kwa hofu huku wakitanga tanga kila kukicha inasikitisha sana. Mfano kuna Mzee mmoja alitekwa na majambazi na kuondoka nae ilikuwa tarehe 13 mwezi wa kwanza 2019, tukio la pili likatokea kesho yake ambapo gari aina ya hiace ilitekwa na mkulima mmoja kuporwa pesa zake alizo kuwa ameuza mpunga wake pale Busunzu.

Imekwenda mbali zaidi baada ya wiki kama mbili mfanyabiashara mmoja maarufu Kama Nick (mmiliki wa M-pesa) alitekwa majira ya saa moja usiku katikati ya mji kwa wenyeji wa Kbondo ni sehemu ya Station One, tukio jingine wiki moja iliyopita hapo hapo Kibondo majambazi waliteka maeneo ya Kumwayi kisha usiku huo huo walienda Kijiji cha Bitare na kupora kwa mzee mmoja na kusababisha kifo cha mzee huyo huku familia ikibaki na simanzi,masikitiko makubwa sana.

Wananchi wameshindwa kupaza sauti zao na kushirikiana na Jeshi la Polisi kutokana na baadhi ya Askari kutokuwa waaminifu na wazembe wa kufuatilia au kuzifanyia kazi taarifa wanazopewa kabla ya matukio kutokea. Wanachi wanashindwa kufanya shughuli zao kwa amani kutokana na hofu iliyotanda kila kona na kupelekea shughuli za maendeleo kukwama, nadhani ni wakati sasa kamati ya ulinzi na usalama kujitathimini kwa kile kinachoendelea hapa Kibondo.

Tunaomba mkuu wa Jeshi la Polisi na Waziri husika kuliangalia hili jambo kwa jicho la tatu maana hali si shwari kabisa hapa Kibondo. Familia za watu zinatanga tanga kwa hofu kubwa sana huku wakilala kwa kuhama hama kila kukicha, ndani ya nyumba zao hapakaliki kwani majambazi huteka na kurudi mara kwa mara, mfano kwa Eliud Bendiliba amevamiwa zaidi ya mara mbili

Bwana shamba wa kijiji cha Busunzu, Mzee Edward Denja ambae alitekwa na kuondoka na majambazi lakini Mungu alisaidia akarudi, yupo mfanyabiashara mkubwa maarufu kama Mashaka amevamiwa zaidi ya mara mbili Pia.

Kuna baadhi ya vocha za halotel ziliokotwa na wananchi katika misitu ya sanganyama wakati wakimtafuta huyo mzee alietekwa, ambazo watalamu WA TEHAMA kitengo cha Polisi mnaweza kuzitumia vocha hizo kutafuta waharifu kushirikiana na kampuni ya Halotel kama kweli mpo seriously na vocha hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa kituo cha Polisi Busunzu

Vile vile kuna simu ziliporwa na majambazi hao ambapo wahanga na wamiliki wa simu hizo wana Imei za simu hizo ambapo zinaweza kutumika kuwatafuta waharifu hata kama WataFlash au kureset simu hizo kuna uwezekano wa kuwatrack kupitia imei za simu kwa wataalamu wa TEHAMA wanaelewa.

Tafadhari wenye mamlaka na dhamana katika suala la kuhakikisha raia anaishi salama na mali zake tunaomba msaada wana Kibondo tumechoka kuishi kama wakimbizi ndani ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom