Kibonde: Nashangaa wabunge wanaoongea kuhusu kutekwa

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,936
3,958
Mtangazaji wa Clouds fm Kibonde amesikika kwenye kipindi cha Jahazi leo akiwaponda wabunge wanaoongelea kuhusu kutekwa badala ya kutoa hoja za kukuza uchumi na maendeleo ya wananchi.

Huyu jamaa mweupe sana kwa kweli, wabunge wataongeleaje maendeleo kama hali ya usalama wao na wananchi hauko sawa? Wananchi wanatishwa, viongozi wanatishwa halafu mtu anatoa hoja zisizokua na mashiko. Nahisi atakua ametumwa awaponde wabung,e ila nimuambie tu kwamba wananchi tunaelewa kinachoendelea na wabunge wanafanya kitu sahihi kutetea usalama wao na wa wananchi.
 
Hii ndio Clouds mliokuwa mnaitetea walipotembelewa na mkuu wa mkoa saa 4 usk mkasema wamevamiwa lakini nataka kuwambia hakuna watu wanafiki kama Ruge na Clouds yote kwa ujumla na kila neno ambalo wanatangazaji wa CLOUDS wanatangaza muhariri ni Ruge na yeye ndio mwandika script
 
Kila MTU na mtizamo wake si kama mnavyopenda nyie muhim wabunge wako ktk kupitisha bajeti polojo waache wafanye mambo ya msingi wabunge sasa polojo tu Mara natishwa Mara kuna watu 11 wanatafutwa Mara naleta hoja saanane haonekani Mara vitu kibao mwisho siku polojo kibao
 
Huyo jamaa mbona ni mweupe siku nyingi, wewe ndo leo unalijua hilo, siku zote huyo jamaa hatumii weledi wake katika kuchambua mambo badala yake huwa anafanya kazi ya kujipendekeza pengine akumbukwe katika teuzi za mzee
 
Hii ndio Clouds mliokuwa mnaitetea walipotembelewa na mkuu wa mkoa saa 4 usk mkasema wamevamiwa lakini nataka kuwambia hakuna watu wanafiki kama Ruge na Clouds yote kwa ujumla na kila neno ambalo wanatangazaji wa CLOUDS wanatangaza muhariri ni Ruge na yeye ndio mwandika script
Hawa wafu FM wanajichimbia kaburi, iko cku na nyinyiem yao nao wataisoma namba
 
Mtangazaji wa Clouds fm Kibonde amesikika kwenye kipindi cha Jahazi leo akiwaponda wabunge wanaoongelea kuhusu kutekwa badala ya kutoa hoja za kukuza uchumi na maendeleo ya wananchi.

Huyu jamaa mweupe sana kwa kweli, wabunge wataongeleaje maendeleo kama hali ya usalama kwa wao na wananchi haiko sawa? Wananchi wanatishwa, viongozi wanatishwa halafu mtu anatoa hoja zisizokua na mashiko. Nahisi atakua ametumwa awaponde wabunge ila nimuambie tu kwamba wananchi tunaelewa kinachoendelea na wabunge wanafanya kitu sahihi kutetea usalama wa wananchi wao.
Kibonde ni mlevi hajielewi
 
Back
Top Bottom