Kiboko ya Wanandoa na wapenzi wasio waaminifu

Inteligence

Member
Dec 12, 2009
36
0
Hi JF:

Inteligence anaileta kwenu software ya simu za mkononi yenye uwezo wa kujua,kusoma,kusikiliza simu/sms kutoka kwa mpenzi/mke/mume kama kwa ujumla
unahisi anaeza akawa anatembea nje ya ndoa au nje ya urafiki wenu.
Software itakwenda kwa jina la kiboko,kukamilika mwisho wa mwezi huu.

Utangulizi:
Kiboko ni software iliyoundwa na inteligence(JF member) ambayo kwa sasa iko ktk majaribio.

Fikiria, mkeo au mmeo wa ndoa anakucheat na mara nyingi mara kwa mara anatuma meseji/piga simu kwa demu au buzi la nje ya ndoa?

Fikiria, Mtoto wako wa KIKE anapoteza muda wa kusoma na kuanza mapenzi kabla ya miaka 18?

Fikiria mpenzi wako anakucheat na kutuma msg kupiga simu kwa kutumia SIM card nyingine kwa siri

Fikiria ungejua nini kinaendelea ktk ndoa yenu na wasiwasi wa maisha kwa kukosekana kwa uaminifu hivyo UKIMWI.

FIKIRIA KITU KINACHOWEZA KUKUONYESHA NANI ANATEMBEA NA MKEO/MUME na kufanya maamuzi mbadala kabla ya ukimwi KUKUPATA.

KIBOKO: Itakuwezesha kujua haya yote:

KIVIPI: simu (maongezi) Pindi mkeo akipiga simu kwa mtu yeyote yule,kuna tone itakualert wewe ikikuuliza irecord maongezi hayo ya mkeo na pengine buzi au usikilize in real TIME

Kurecord: maongezi yao (mkeo na buzi may be) yatarecordiwa na baada ya maongezi yatatumwa kwako kwa njia ya internet muda huo huo.

Real time kusikiliza-Hapa namaanisha mwingiliano wa simu (Utasikiliza kila kitu wanachoongea wakati huo huo bila wao kujua unawasikiliza) na unaweza kurecord maongezi kwa simu yako pia.

SMSindi mkeo/mume anapotuma meseji kwa demu/buzi copy ya meseji inakuja kwako bila wao kujua.

Hivyo hivyo kwa watoto/na wengineo.

KIBOKO SOFTWARE: itakamilika ktk kipindi hiki cha majaribio mwishoni mwa mwezi huu.
Haitouzwa KIHOLELA.

SOFWARE HII itatakiwa kuwa installed/configured kwa simu yako na huyo unaetaka ku mmonitor.

Hutauziwa software bali itakuwa installed remotely

BEI YAKE ITAKUWA KUANZIA DOLA 80:

HAITOUZWA KIHOLELA:NARUDIA HAITOUZWA KIHOLELA:

Katika kipindi hiki cha majaribio, KIBOKO imefanikiwa sana ktk simu za aina zote isipokuwa za KICHINA. (WORKING ON IT)

NAKARIBISHA MAONI YENU KWANI YANAWEZA KUNISAIDIA AU KUWASAIDIA NANYI PIA.

Asanteni.
 
Nikitaka kucheat si natumia line/simu ya mwenzangu au simu za kamba(ttcl)?
Atanipata wapi!
Kama unaweza (wewe wakala)waambie hao watengenezaji tayari huku Bongo tushapata ufumbuzi wa kuikwepa hiyo teknology, hivyo wakaanze upya!
 
Ok,watengenezaji ndo mimi;Asante kwa mchango wako mzuri lakini ikitokea ukitumia simu ya mtu line ile ile,kuna interface nitaiweka ktk kipindi hiki cha majaribio na UTAKAMATIKA tuu.
 
kunguru hafugiki tuuuuuuu!!! wewe huwezi kumchunga kama kuku! So kaa naye chini mzungumze na siyo kumwekea mitego isiyokuwa na A wala Z! Eti Simu??????
 
Kama ni kweli hongera, wasiwasi wangu naiona story kama ya kina Karimanzira vile. Lakini mtu unaye m spy utaipata wapi simu yake ili iwe configured? Na utathibitishaje kwamba huyo mtu ninaye takwa ku m monitor nina uhusiano naye?

Ninaona kwamba utajiingiza bure kwenye matatizo kwani privacy ni rights za mtu. Ushauri ni kwamba nenda kawauzie watu wa inteligence kwani wao wana haki ya kisheria kufuatilia interest za kitaifa kama kuna mtu wana mfuatilia.
 
asante kwa ushauri,mpaka sasa na order kama 1324 hivi,natarajia nipate kama wateja million moja hivi kwa makisio ya chini.
 
Kama ni kweli hongera, wasiwasi wangu naiona story kama ya kina Karimanzira vile. Lakini mtu unaye m spy utaipata wapi simu yake ili iwe configured? Na utathibitishaje kwamba huyo mtu ninaye takwa ku m monitor nina uhusiano naye?

Ninaona kwamba utajiingiza bure kwenye matatizo kwani privacy ni rights za mtu. Ushauri ni kwamba nenda kawauzie watu wa inteligence kwani wao wana haki ya kisheria kufuatilia interest za kitaifa kama kuna mtu wana mfuatilia.

naomba kukuelewesha:

Wewe unaweza kummonitor mtu mmoja at a time.wewe na mkeo say,au wewe na mpenzi wako kwa simu hizi mbili kuwa installed and configured na KIBOKO.

Nimetumia takribani wiki kumi na mbili kuikamilisha kazi hii.na najua side effects zake ,faida na hasara.

Huna haja ya kumvizia mmeo aende kuoga ndo usome meseji zake,au phone book zake yote hii inawezekana na KIBOKO.
 
why??? why? monitor some one? binadamu ajiheshimu mwenyewe bana. ni kujiongezea kazi kuanza kumonitor mtu/watu/mpenzi. bongo kuna mapenzi basi??? nyumba ndogo kibaooo! hasa wanaume sio waminifu kabisaaaa! na huenda itawasaidia kumonitor small house , anyway!
wazo la kuwauzia Intelligency ni bora zaidi work on that.....wanaolazimisha mapenzi watakuja lakini kuweka order.
 
Mmmh, it looks like unataka kuongeza idadi ya watu watakaokufa kwa pressure uuh? Si bora UKIMWI unaua slowly? Utanipa na muda wa kuiweka fresh familia yangu? Kisa cha kuanza kujipandisha pressure na kufa ghafla kwa stroke/shinikizo la damu nishindwe hata kuwaachia msingi mzuri wanangu? Inaelekea huwatakii mema watanzania wewe. Stop it!
 
wazo zuri.asante kwa ushauri.
 
Hahahaha........
 
Si rahisi kumchunga binadamu akitaka kufanya vitu vyake. Mtu akiwa na namba ya siri yenye jina bandia ambayo mkewe/mumewe/boyfriend au girlfriend haijui basi si rahisi kabisa kuifuatilia ili kusikiliza/kurecord mazungumzo ya muhusika.
 
Hiyo ni kama kujaribu kutaka kujua moyo wamwenzio unawza nini. Itazuia ufanisi na kudumaza maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuwafanya watu wame wanafuatiliana muda wote. Na kifupi hakuna teknolojia ya aina hiyo inayoruhusiwa kwani mbali na kuingilia taarifa binafsi za watu (right to privacy) italeta mafarakano ya sio na msingi. Ya nini umfuatilie mtu ambaye ana nafsi ya kutenda kwa utashi wake??? Jaribu nyingine yenye kutuletea maendeleo, hiyo ni kama ile ya manyau ya kuwanatisha watu katika shughuli ambayo kimsingi haisaidi kuleta suluhsisho katika jamii bali inaongeza matatizo, chuki, kuwindana na kupotezeana wakati kama sio mashinikizo ya damu!

Ningefurahi kama ningesikia teknologia yako inaweza kubaini ufisadi ndani ya ofsi za umma, kujua sadaka tunazotoa makanisani na miskitini zinatumkaje, kujua kama pombe na mijinyma tunayokula inashughulika vipi na miili yetu, kujua kama mvua zitanyesha kwa mtawanyiko upi, kujua kama mazao yatauzika vipi nk nk nk.

Haya ya kufuatiliana kwenye simu yatakubana hata na wewe mzee, wagunduzi makini hawaruhusu kitu kama hicho ambacho kinaweza kuwaletea nao mateso baadae..kuna watu wapo allergic na sauti za kwenye simu hata ikiwa ya mamako mzazi tasema ni kimada wako!utatambuaje mahusiano kwa kuongea kwenye simu?? akitaniwa, we jaza??!

Naikenea hiyo teknolojia yako ni IBILISI, IKAPATE KUSHINDWA MILELE!
 
kwa huu muda mfupi niliobandika hili Tangazo nimeshapata order kama 2134.

Kanyaga twende.
 
Ha ha ha ha na wale wote wanaocheat na kuliona tangazo hili basi watabadilisha mienendo yao ili wasigundulike, si rahisi kumchunga binadamu siku zote amini hivyo au unajitafutia matatizo tu.
 
Mkuu wa kaya:nimekugongea senksi hapo.

Nami nimekutunuku Mkuu, kama humuamini mamie mwali au njemba badala ya kuanza kupanga mikakati ya kufuatilia nyendo zake 24/7 ili kujua kila kinachojiri katika mazungumzo yake ni bora kuchora talaka tu au kuomba uchorewe talaka.
 
Back
Top Bottom