Kibo Seeds kumbe Matapeli wakubwa wa Mbegu!

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Kampuni ya Kibo Seed au Kibo Seed company ni kampuni ya mbegu kutoka nchini Kenya na ina ofisi yake kubwa mita kama hamsini kaskazini mwa stend ya hiace opposite na Annex Hotel hapa mjini Arusha.

Naomba niandike kwa masikitiko makubwa sana kwa sababu hii imenikuta mimi personally. Mwaka huu nimenunu kila 50 za mbegu ya mahindi variety inaitwa Kitale ambayo inachukua muda wa miezi mitatu kukomaa. Niliipanda mwaka huu kwa mara ya kwanza kwani miaka mingine nimekuwa nikipanda SEED.Co au DK 8031 ya Zambia na Malawi.

Mbegu hii ya kitale wakati inapandwa shambani niligundua kwamba ilikuwa siyo clean kwani ilikuwa na makapai ya maganda ya mahindi pamoja na mbegu zilizo oza na nyingine vipande jambo ambalo si kawaida kwa mbegu iliyoidhinishwa. Mahindi yalipoanza kuzaa nikaona kioja cha mahindi yenye tabia za aina tofauti tofauti kwani mengine yalikuwa yamezaa mbili mbili na nyingine moja moja. Shapes za mahindi pia pamoja na urefu ulikuwa tofauti tofauti. Ikumbukwe kamba eneo lilipandwa haya mahindi lina rutuba inayofanana na all agronomical practices zilifuatwa including plant density au spacing, timely weeding n.k.

Wakati mahindi yanakomaa nikagundua wazi wazi kabisa kuwa shamba lilikuwa na mchanganyiko wa varieties lukuki na siyo Kitale kama nilivyodhani na ukubwa wa mahindi ukawa tofauti tofauti. Baada ya miezi 5 muda ambao mahindi yangetakiwa yote yawe yamekomaa na kukauka uniformly nikashindwa kuvuna kwani mengine bado yalikuwa na majani mabichi.

Watu wote wengine wakavuna na mahindi yangu yakabaki shambani peke yake na matokeo yake wezi wakaanza kuiba. Ilibidi nivune mahindi mabichi na makavu pamoja ili kuzuia kupata hasara. Mahindi niliyovuna yakawa kama ya kienyeji kwani mchanganyiko wake ulikuwa wa kutisha.

Ikanibidi last week niende kwenye duka moja la mbegu kuuliza kuhusu mbegu ya kitale ndo wakanipasulia jipu kuwa Kibo Seed ni matapeli na huwa wauzaji wa hiyo kampuni hununua mahindi sokoni na kwenda kuyabadilisha rangi ku pack na kuweka dukani. Mbegu hizi zinaandaliwa na kufanyiwa packing sehemu isiyojulikana huko UNGA LTD.Katika utafiti wangu nimeambiwa maduka mengi ya pembejeo hapa Arusha huwa hawapendi kuuza mbegu ya Kitale kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wakulima.
Hali hii imeniogopesha kwani kwa namna hii wanaua uchumi kwa kudidimiza kilimo na hivyo kusababisha upungufu wa chakula nchini. Niko tayari kutoa ushirikiano kama watu watataka ushahidi kwani kama wakifanya hivi kwa mkulima mwenye elimu kama mimi je itakuwaje kwa wale ambao hawana elimu na wantegemea kwa asilimia 100 kilimo kama chanzo cha kipato cha familia na chakula.

Ninasema Kibo Seed Company ni matapeli kwa sababu katika hali ya kawaida mbegu au variety ya aina moja haiwezi kuzalisha mimea iliyopishana tabia za ukuaji kwa kiasi kibubwa hivi.Pia mbegu nyingine kama DK na SEED Co. ziko uniform katika ukuaji ,kukomaa, na hata kukauka na hizi ndizo sifa za improved variety yoyote ile.
Wakati mwingine serikali inajikuta inasingizia hali ya hewa kama chanzo cha mavuno kidogo kumbe sababu nyingine ni kuwepo kwa kampuni za mbegu zinazofanya uhuni wa kutengeneza mbegu feki na kusababisha hasara si kwa wakulima tu bali hata njaa kwa waTZ. Hii ni hatari sana.!!!

NAOMBA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA KAMA TOSCA KUTUSAIDIA KUPAMBANA NA HUU UHUNI AMBAO KWA KIASI KIKUBWA UNADIDIMIZA KIPATO CHA MKULIMA NA HATIMAYE UCHUMI WA NCHI HIVYO KUONGEZA UHABA WA CHAKULA NCHINI.
 
Back
Top Bottom