Kibiti: Polisi yaua watu wanne(4) wanaodhaniwa kujihusisha na mauaji wilayani humo

jwtz komandoo wasingewaua wangewateka kininja live na kuwanyang'anya silaha kisha wahojiwe vizuri Ukweli ujulikane, nina imani hapo walienda Asikari waoga na watakuwa waliwakata hai wakaamua kuwaua wenyewe kisha wamezuga kuwa ni mapambano ya nusu saa bila kuongezeka dk kwa kweli kuna Sinema hapo hilo tukio ni la kutengeneza yapaswa lichunguzwe kwa undani zaidi.
Mkuu wewe una lako jambo rohoni, ulitaka usike askari polisi wameuwawa ushangilie na kuwakebehi hawana utaalamu. Matukio mangapi ya ujambazi hapa mjini mchana kweupe tunaona majambazi wanauwawa na polisi hakuna anayejeruhiwa? Unataka waelezee kila lkilichofanyika wavujishe siri? Pengine askari walitega mtego wa kuwavizia baada ya kupewa taarifa na raia wema? Wakisema ukweli si kuna watu watasakwa na wahalifu waliobakia?
 
Nimeisoma habari na michango ya watu mbalimbali naomba niseme machache.

Kwanza japo mpaka sasa sikufurahishwa na jitihada za vyombo vyetu vya usalama katika kumaliza hili tatizo, leo naomba nipingane na wengi wanaokejeli kwenye huu uzi bila kutafakari sana. Natoa sababu zangu.

1. Kama hao marehemu walikuwa watu wema kwanini baada ya kukutana na polisi wa doria wakimbie??

2. Kwa nini watu hawa ambao wengi tunasema wamedhaniwa waanze kurushiana risasi na polisi kwa muda wa nusu saa nzima?

3. Je hizo silaha wamezipata wapi na risasi zote hizo zaidi ya 17?

4. Mwisho, Je hao marehemu walikuwa wakienda wapi na silaha usiku huo na hali wakijua hali imechafuka huko na yeyote akutwae na shaka anaweza kuingia matatani?

Ndugu zangu japo tuna shida kubwa na mfumo wa Jeshi letu la polisi na mimi nikiwa muungaji mkono wa uhitaji wa mageuzi katika jeshi hili, nawaomba tuwe makini katika kutoa hoja ili hata kuwapa nguvu wale wachache wanaojituma kufanya doria usiku huo na kuacha familia zao katika mashaka ili tu kuokoa maisha ya watanzania waishio kwa shaka kubwa. Jeshi la Polisi lahitaji mageuzi makubwa si tu kiutekelezaji bali kifikra lakini nasi katika kuchangia yatubidi kuchangia kifikra zaidi na kuweka mihemko pembeni ili hata wanadhimu wa jeshi hili watakapolitia humu wapate cha kuongea kwenye vikao vyao.
 
Kumbuka kuwa hairuhusiwi kwa RAIA kutembea usiku kwa maeneo hayo. Hawa walikuwa wanatembea usiku tena kama kikundi halafu wakiwa na silaha! Bado mnawatetea!
Hakuna mtu anayewatetea.

Kutembea usiku ni kukiuka amri halali, hakumfanyi mtu awe jambazi kumbuka hilo.
Ikiwa walibainika kuwa na Silaha hilo ni kosa
Ikiwa walirusha risasi, hakuna namna bali kujibiwa kwa risasi na walinzi wa amani

Jamani eleweni ninachosimamia. Kauli ya 'sadikiwa' haina mantiki ikiwa hakuna uhakika hao ni majambazi wa kupora au ni majambazi ya Pwani.

Kauli imelenga kuoanisha tukio la jana na la mauaji bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Hiyo si sahihi, matukio yatakapojirudia kutakuwa na maswali, si waliuawa?

Picha kwa mtu wa kawaidi ni majambazi yaliyouawa yanahusiana na mauaji ya Pwani

Inaweza kuwa kweli ndivyo ilivyo lakini pia inaweza kuwa sivyo

Hilo ni tukio la Polisi kukabiliana na majambazi , inatosha bila kusema ''wanaosadikiwa''

Ukiwepo ushahidi wa ku link tukio na mauaji tutakuwa na ushahidi wahalifu wameondoka.

Tunasema bila forensic examination si sawa ku link tukio la jana na yale ya Pwani.

Ni kosa kwasababu tutapoteza focus tukiamini majambazi ya Pwani yamekabiliwa kumbe inaweza kuwa ni majambazi ya kupora tu, ya Pwani yamejificha kwasababukusadiki
 
Kama habari hii ni kweli lipo tatizo

Kudhania tu hakumfanyi mtu kuwa na hatia na adhabu!
Mbona huzungumzii bunduki walizokua Nazo.... anyway bunduki kwako ni kama mswakii ndo mana unatafuta hatia
 
Na jeshi letu lijifunze kusitiri miili ya askari wake pindi wanapopatwa na maafa kama wanavyofanya kwa majambazi kwamba miili yao haionyeshwi ovyo ovyo, nilisikitika jinsi picha za askari zilivyosambaa wakigalagazwa kwenye pick up nyuma
Ile ni raia hasa waandishi wa habari ndio walisambaza hizo picha. Inabidi sheria kama ya Uingereza ifanye kazi hapa Bongo.
 
Mbona huzungumzii bunduki walizokua Nazo.... anyway bunduki kwako ni kama mswakii ndo mana unatafuta hatia
Kwa mantiki gani?
Mimi sikuwepo nimesoma taarifa kwanini unadhani ni muhimu kuzungumzia?
 
Mkuu wewe una lako jambo rohoni, ulitaka usike askari polisi wameuwawa ushangilie na kuwakebehi hawana utaalamu. Matukio mangapi ya ujambazi hapa mjini mchana kweupe tunaona majambazi wanauwawa na polisi hakuna anayejeruhiwa? Unataka waelezee kila lkilichofanyika wavujishe siri? Pengine askari walitega mtego wa kuwavizia baada ya kupewa taarifa na raia wema? Wakisema ukweli si kuna watu watasakwa na wahalifu waliobakia?
kule mwanza Rais magufuli alisema polisi watumie mbinu za medani kuwanyang'anya silaha majambazi, kumbuka kipindi cha Zombe polisi waliwaua wafanya biashara wakasingizia ni majambazi
 
duh hapa nadhani ndio tunaenda kuchochea moto zaidi!!!na wasi wasi sana na awa waliouliwa kama kweli ni wahusika halisi!!tusije umiza watu wasiohusika hili mradi tuuridhishe umma!!hizi ni roho za watu jamani!!tujiakikishe!!maana hizi kauli za wanahoisiwa alaf roho zishtoka!!!mh!!
 
Sifa ya kwanza ya police ni kumkamara mhalifu sio kuua....

mpaka Hapo wamesema wanadhania hawana uhakika hawa police wa ncha kali unaweza kuta wamepwleka wafungwa huko na kufanya maigzo
 
Ukisoma hii habari vizuri utagundua Kuwa Polisi Haina uhakika kwamba waliouawa ni wauaji kwa kuwa waliouawa WANASADIKIKA KUWA HUENDA NDIO WANAOJIHUSISHA NA MAUAJI YA MKIRU.
WATU WANAOSADIKIKA KUWA NI WAHAALIFU!
 
Tumia common sense kama wewe ndio polisi na mtu unamwambia asimame anakujibu kwa risasi.
Ungemchukulia kama raia mwema??
how far are we sure kweli kulikuwa na majibizano ama so jamaa walikuwa na silaha!!hizi nyimbo majibishano ya polisi tumeshashuhudia watu wengi sana wasio na hatia kwa kutumia hii swaga!!cha ajabu ktk hayo majibizano yao hakunaga hta askari utakayesikia kalengwa hata kidole!!!mh watu wangu wanateketea kwa kukosa maarifa
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom