Kibatala and Team, Mwenyezi Mungu anawasimamia -- msikate tamaa kamwe!

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Mpaka sasa mmeshafanya kazi kubwa sana! Kesi za jinai huangalia Kanuni ya "Beyond reasonable doubt" na mpaka sasa meshatengeneza "doubts" kibao na hata Mh. Jaji anajua fika.

Mtafikiri Jaji hayupo na ninyi lakini ukweli ninamwona kabisa yupo na ninyi na mnafanya kazi kubwa sana.

Mwisho wa siku Jaji huyo ataishangaza Serikali na pia hata Mawakili wa Serikali ninaamini wanalijua hilo ila wanapigana kiume wasionekane hawataki kuitumikia nchi.

Mpaka sasa Jaji amejitahidi sana kuchukua ushahidi wote ili asiache kakitu. Angalia issue ya Diary - Jaji ndiye alikuwa kama ameisisitiza issue hiyo iangaliwe na kaiangalia kwa umakini sana - ninaamini kuna kitu kimeonekana humo.

Mpaka sasa hamna ushahidi wowote unaoweza kumshawishi mtu, hata asiye na elimu ya sheria,kuwa kuna ukweli wa makosa ya kigaidi yamefanyika humo.

Jaji anachofanya ni kuchukua kila kitu then atakuja kuchambua na kuamua against Serikali na haitaweza kukata hata rufaa.

Kibatala and Crew please endeleeni kuweka mapingamizi tena na tena. Hayo yanachangia sana kuleta "doubts" na hivyo mapingamizi hayo ndiyo yatawshindisha kesi - msichoke na kukata tamaa kuweka mapingamizi yana umuhimu sana sana.

Mwisho pamoja na kuwa mimi ni MCCM asili, ninaamini katika upendo na umoja - sifurahishwi kamwe na kesi hiyo mbaya kuwakumba wenzetu.

Ninaumia sana sana kwa mateso wanayopata hao ndugu zetu kwani Mungu awaongoze tu wao, familia zao, marafiki na hata jamii inayowakubali wasijenge chuki dhidi ya watesi wao, kwani maisha haya ni ya Mungu mwenyewe na kila nafsi itaonja mauti.
 
Kumfunga mtu maisha ama miaka 30 ni LAZIMA mahakama ijiridhisihe kwamba mtuhumiwa alitenda PASI NA SHAKA, sasa ukingalia ushahidi wote unaacha maswali mengi mno kuliko majibu, hakuna mtiririko wa ushahidi toka Shahidi no 1 hadi huyu wa sasa.

Ni ngumu mno kumfunga mtu ambaye hakutenda kosa.
 
Mpaka sasa mmeshafanya kazi kubwa sana! Kesi za jinai huangalia Kanuni ya "Beyond reasonable doubt" na mpaka sasa meshatengeneza "doubts" kibao na hata Mh. Jaji anajua fika. Mtafikiri Jaji hayupo na ninyi lakini ukweli ninamwona kabisa yupo na ninyi na mnafanya kazi kubwa sana. Mwisho wa siku
Naomba msaada mwenzenu tangu kesi hii ianze sijaona mashitaka ya ugaidi wa Mbowe, ila naona yanazungumzwa mambo ya taratibu za kipolisi tu. Mara Mbege, daftari la mahabusu, tuliwaambia wakae chini, wachuchumae, mbweni, Central Dar, kukata miti ya barabara ya Iringa, n.k
 
Kumfunga mtu maisha ama miaka 30 ni LAZIMA mahakama ijiridhisihe kwamba mtuhumiwa alitenda PASI NA SHAKA, sasa ukingalia ushahidi wote unaacha maswali mengi mno kuliko majibu, hakuna mtiririko wa ushahidi toka Shahidi no 1 hadi huyu wa sasa.

Ni ngumu mno kumfunga mtu ambaye hakutenda kosa.
Kumfunga mtu maisha ama miaka 30 ni LAZIMA mahakama ijiridhisihe kwamba mtuhumiwa alitenda PASI NA SHAKA, sasa ukingalia ushahidi wote unaacha maswali mengi mno kuliko majibu, hakuna mtiririko wa ushahidi toka Shahidi no 1 hadi huyu wa sasa.

Ni ngumu mno kumfunga mtu ambaye hakutenda kosa.
Meona eee?
 
Siku njema haionekani asubuhi. Hadi sasa kesi hii inashughulikiwa na wateuliwa wa jiwe.

Kilichopo ni kufikishwa hukumu waliyo nayo.
 
IMG-20211123-WA0024.jpg
 
Back
Top Bottom