Kibaoni-Uvinza: Barakoa imekuwa biashara dili

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,358
2,000
Habarini wadau,

Juzi, jana na leo nikiwa katika shughuli zangu nimepata nafasi ya kupita katika geti lililopo Kibaoni Uvinza ambapo kuna huduma ya upimaji wa joto kwa ajili ya utambuzi wa korona.

Kilichonishangaza kwa kweli ni biashara ya kuuza barakoa ambapo baadhi ya vijana wakiwekewa kifua na wahudumu wa afya, polisi na mgambo kama huna barakoa wamekuwa na tabia ya kulazimisha wasafiri kununua barakoa kwa lazima kwa bei ya Tshs. 1000 kama hununui hupimwi joto na huvuki.

Kinachokela zaidi vijana wanauza barakoa za vitambaa za kushona ambazo hazijadhibitishwa na chafu, wenyewe pia hawajavaa barakoa.

Hili jambo liangaliwe kwa makini sana kwani badala ya kudhibiti korona sasa watu waambukiza korona,mwenzetu mmoja alipojaribu kuhoji askari polisi mmoja alisikika akisema "mkuu wa mkoa ndiyo kaagiza wauze barakoa,sasa wewe nakupeleka kituoni", alipomhoji kwa sheria ipi, kijana mmoja anayeuza barakoa alichombeza kwa kusema "afande usimlegezee huyo kanipiga picha".

Afande alichukua simu ya mwenzetu huyo na kujaribu kufuta ambapo hakuweza na picha ikaingia kwa dustbin.

Hawa watu wachukuliwe hatua mapema la sivyo kwa uchafu huu korona itatumaliza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom