Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Wiki iliyopita Balozi wa India nchini, Sandeep Arya alimtembelea Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula, jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha pamoja na kufahamu majukumu ya Tume hiyo.
Hata hivyo, wajuvi wa mambo wanadai kuwa, Ziara hiyo ya Balozi ni matokeo ya kibano cha Tanzania cha kuzuia utoroshwaji wa Tanzanite kupitia magendo kupitia uzio uliojengwa kuzunguka Migodi ya Tanzanite iliyopo Mirerani, Simanjiro Manyara.
Ingawa Tanzania ndiye mzalishaji pekee wa Tanzanite lakini India imekuwa ikiuza sana Tanzanite kutokana na biashara ya magendo. Kufuatia Zuio la Serikali, Ziara ya Balozi ni mkakati sahihi kwao kutazama namna ya kuendelea kufanya biashara katika mazingira mapya ya uwepo wa Tume na udhibiti ulioimarishwa.
Masonara wakiwa kazini huko Jaipur, Rajasthan India.