Kibano cha Ngeleja Bungeni: Hotuba ya Madini na Nishati 2011

Status
Not open for further replies.
Mh ngeleja kubali kuwa umeshindwa kutimiza matarajio ya wananchi!ukosefu wa umeme ni wa kiwango cha hali ya juu,kiwango ambacho hakivumiliki.madhara ya kukosa umeme ni makubwa kuliko unavyofikiria.mfano mmoja nimeshuhudia katoto kachanga kakipoteza maisha baada ya kukosa oxygen ambayo ilikuwa ikitolewa na machine inayotegemea umeme.mahospitali mengi hayana standby generator hivyo umeme unapokosekana hupelekea vifo vya vichanga hivi,kwa ufupi ngeleja na wizara yako mnachangia vifo vya watoto.sasa kama wewe ni waziri mwenye utu ni lazima uwajibike!!
Ndugu wabunge tuache mzaha tusicheze na maisha ya wapiga kura.
 
Aloshindwa sio Ngeleja bali ni JK na utawala wake wa CCM. Ni lini watanzania tutafikia kutambua - who is responsible ili awe accountable?.. Badala yake kila siku tunatafuta mchawi na urahisi wa kutoa lawama kama vile ni ukosefu wa abadu baba akijamba ukasema baba umejamba!

Ni makosa makubwa kwa upinzani kuelekeza mapigo yao kwa Ngeleja kwa sababu huyu ni waziri wa tatu kama sikosei ktk wizara hiyo toka JK ameshinka madaraka, na ikumbukwe tu kwamba msisitizo mkubwa wa utawala wa JK kutoka kwa Mkapa ulihusisha zaidi ukosefu wa umeme nchini na kwamba swala hilo litakuwa la kihistoria ikiwa wananchi watampa kura zao.

Leo matatizo ndio kwanza yanazidi, baada ya JK kutuletea mikataba feki ambayo haina tija lakini wepesi sana wa kulaumu Mwenyezi Mungu kwa kutokutujalia mvua ya kutosha. Kama kweli tunategemea mvua zaidi basi kuna sababu gani ya kuwa na waziri...Ngejela ni ktk mfululizo wa viongozi ambao wanakabidhiwa jembe la mkono kulima hekta 2,000..

Na labda kwanza tuangalie nini aliomba yeye kabla ya bajeti na kitu gani amepewa lakini kulaumu waziri ambaye atatumikia kutokana na kile alochokabidhiwa haiwezi kupoteza ukweli kwamba JK ndiye aloshindwa na ndiye anatakiwa kuondoka. kwanza alikuwepo Msabaah akajiuzuru, kaingia Karamagi akajiuzuru leo tena mnataka Ngeleja ajiuzuru wakati kujiuzuru kwao hakusaidii Taifa kwa lolote ikiwa utawala upo chini ya JK..

Vyama vya Upinzani mnajua wapi pa kumgonga nyoka hizi habari za kujivua magamba, sijui kulalama na makelele ya nyoka huyo nyoka huyoo huku nyie wenyewe mnakimbia kuparamia juu ya viti na meza haziwezi kusaidia kitu isipokuwa kusanyeni nguvu zetu na kushika rungu kumponda nyoka kichwani! mtakuwa mmemaliza matatizo ya Watanzania.
 
Naomba mwenye hotuba ya wizara ya nishati na madini aiweke tuione!
 
Aloshindwa sio Ngeleja bali ni JK na utawala wake wa CCM. Ni lini watanzania tutafikia kutambua - who is responsible ili awe accountable?.. Badala yake kila siku tunatafuta mchawi na urahisi wa kutoa lawama kama vile ni ukosefu wa abadu baba akijamba ukasema baba umejamba!Ni makosa makubwa kwa upinzani kuelekeza mapigo yao kwa Ngeleja kwa sababu huyu ni waziri wa tatu kama sikosei ktk wizara hiyo toka JK ameshinka madaraka, na ikumbukwe tu kwamba msisitizo mkubwa wa utawala wa JK kutoka kwa Mkapa ulihusisha zaidi ukosefu wa umeme nchini na kwamba swala hilo litakuwa la kihistoria ikiwa wananchi watampa kura zao.Leo matatizo ndio kwanza yanazidi, baada ya JK kutuletea mikataba feki ambayo haina tija lakini wepesi sana wa kulaumu Mwenyezi Mungu kwa kutokutujalia mvua ya kutosha. Kama kweli tunategemea mvua zaidi basi kuna sababu gani ya kuwa na waziri...Ngejela ni ktk mfululizo wa viongozi ambao wanakabidhiwa jembe la mkono kulima hekta 2,000..Na labda kwanza tuangalie nini aliomba yeye kabla ya bajeti na kitu gani amepewa lakini kulaumu waziri ambaye atatumikia kutokana na kile alochokabidhiwa haiwezi kupoteza ukweli kwamba JK ndiye aloshindwa na ndiye anatakiwa kuondoka. kwanza alikuwepo Msabaah akajiuzuru, kaingia Karamagi akajiuzuru leo tena mnataka Ngeleja ajiuzuru wakati kujiuzuru kwao hakusaidii Taifa kwa lolote ikiwa utawala upo chini ya JK..Vyama vya Upinzani mnajua wapi pa kumgonga nyoka hizi habari za kujivua magamba, sijui kulalama na makelele ya nyoka huyo nyoka huyoo huku nyie wenyewe mnakimbia kuparamia juu ya viti na meza haziwezi kusaidia kitu isipokuwa kusanyeni nguvu zetu na kushika rungu kumponda nyoka kichwani! mtakuwa mmemaliza matatizo ya Watanzania.
ngeleja ajiuzulu kwa sababu karudia madudu yaleyale ya waliomtangulia.
 
Waheshimiwe pitieni michango ya hapa jamvini kabla ya kufanya maamuzi yenu!
 
Bajeti inapitishwa bungeni na siyo JF. Wewe unatoa kilio hapa unafikiri nani anakusikiliza? Wabunge wenyewe wa CHADEMA hamfikii hata theluthi ya wa CCM halafu unawaza kuzuia bajeti.
kuna ndoto zaweza kuwa kweli!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom