Kibanga Ampiga Mkoloni mnakumbuka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibanga Ampiga Mkoloni mnakumbuka?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 10, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Katika upekuzi wangu jana nikawa nimekifuma kitabu hiki na mwisho nikakutana na hadithi hii ungana nami kuisoma ina toka katika kitabu cha 6 Tujifunnze Lugha Yetu!

  Zamani za ukoloni, palitokea Mzungu mmoja. Mzungu huyo hakuwa mtu mwema. Alikuwa mkali na mkatili sana. Kwa ajili ya ukatili wake watu walimwita mkoloni. Wanancgi wote walimchukia sana popote pale alipokwenda.

  Mzungu huyo alikuwa Bwana Shamba. Alikuwa na bakora iliyokuwa imetengenezwa kwa mkwaju. Kila alipokwenda kukagua mashamba, alikuwa na bakora hiyo mkononi. Alipendelea sana kuitwa "Bwana Mkubwa". Mkolono huyo alifurahia sana kupiga watu. Aliwapiga watu waliposhindwa kupalilia mashamba. Aliwapiga pamba yao ilipokuwa chafu. Aliwapa taabu sana.

  Katika kijiji cha Kwachaga, Wilaya ya Handeni, alikuwapo mzee mmoja aliyeitwa Kibanga. Mzee huyu alikuwa mwenye nguvu, hodari na shujuaa. alikuwa fundi wa mieleka. Ingawa alikuwa mwenye nguvu, alikuwa mpole. Hivyo watu wa Kwachaga walimpenda na kumtegemea kuwaongoza vitani.

  Siku moja yule Mzungu alifika Kwachaga kukagua mashamba ya mihogo. Jumbe pamoja naye wakatembelea mashamba. Kwa bahati mbaya mwaka ule haukuwa na mvua ya kutosha. Kwa hiyo mihogo haikustawi. Kila wakati yule Mzungu alipotazama mashamba alitikisa kichwa na kufoka. Mwisho akamwagiza Jumbe kuitisha mkutano wa watu wote wa kijij. Waliporudi kijijini Jumbe akapiga mbiu. Watu wote wakakusanyika. Walipofika tu, yule Mkoloni akaanza kuwatukana, akawaambia, "Ninyi watu weusi ni wavivu sana. Hamfanyi kazi sawa sawa. Mashamba yenu ni mabaya sana". Jumbe akataka kumjibu ili kumweleza kwa nini mihogo haikustawi. Kabla hajamweleza yule Mzungu alimrukia na kumpiga kofi. Kisha akasema, "Sitaki kijibiwa na wewe, mvivu wa wavivu". Watu wote wakakaa kimya. Hakuna aliyeweza kufanya kitu.

  Kibanga akajitokeza, akasimama. Akamtazama yule Mkoloni kwa dharau sana. Kisha akamwuliza, "Kutuita sisi wavivu ndiyo nini? Na kumpiga Jumbe wetu mbele yetu, maana yake nini?"

  Kabla ya kumaliza kusema, Mkoloni aliamka kitini kwa hasira , akataka kumpiga Kibanga. Alishika bakora yake mkononi. Akasedma, "Nitakuadhibu vibaya kima we! Unajifanya kuwa shujua? Huwezi kucheza na bwana mkubwa. Nitakupiga, kisha utakwenga jela miezi sita." Lakini Mkoloni hakuwahi kumwadhibu Kibanga. Aliadhibiwa yeye. Kabla ya kumfikia, Kibanga alimpiga chenga. Kisha akamrukia, akamnyangánya bakorta yake. Akaitupa, ikaokotwa na vijana, wakaificha.

  Kibanga alimshika yule Mzungu akamwambia. "Wewe umezoea kutoa amri kila siku, lakini leo utashika adabu, mbwe wee!" Papo hapo alimnyanyua juu na kumbwaga chini, puu! Yule Mkolono akaumia sana. Kabla ya kuamka, Kibanga alimwinua tena na kumbwaga chini kama furushi la pamba. Akamkalia.

  Hapo yule Mkoloni akawa hana la kufanya. Bila ya bakora alikuwa hana nguvu. Akaomba radhi akilia, "Samahani! Naumia! Nihurumie! Sitafanya tena hivyo." Kibanga alimjibu kwa dharau, "Sikuachi mbwa wee! Leo utakiona cha mtema kuni! Ulijiona una nguvu. Leo nitakutengeneza."

  Wazee wakamshika Kibanga na kumwomba asimpiga tena. Akamwacha. Kwa shida yule Mkoloni akajikokota kwenda hemeni. Alikuwa amejaa vumbi huku damu zikimtoka. Wazee wengine wakamfuata nyuma. Walinyamaza kimya, wakimhurumia. lakini vijana walifurahi sana.
  Baadaye waliimba wimbo wa kumsifu Kibanga.

  Jioni yule Mkoloni aliomba radhi kwa wazee. Mzee mmoja akasimama na kumwambia, "Umefanya vizuri kuomba radhi, nasi tunaipokea. Lakini tangu leo usijivunie ubwana. Jivunie utu. Ninyi wakaoloni mna kiburi. Mnatudharau. Kama ungetuuliza tungekuambia kwa nini migogo haikustawi. Haya yote yamekupata kwa sababu ya kiburi chako. Katika nchi hii tuanaamini kuwa kiburi si maungwana".

  Baada ya hapo wazee wakamsamehe, lakini hawakumpa bakora yake. Ikabaki nyumbani kwa Jumbe. Yule Mkoloni akaondoka. Tangu siku hiyo hakufika tena Kwachaga. Kila mara alipokutana na watu aliyakumbuka maneno ya yule mzee, "Kiburi si maungwana".

  Siku hizi kijiji cha Kwachaga kina maendele mazuri ya kilimo na mifugo. Maendeleo yote yamepatikana kwa sababu ya uongozi bora wa Serikali ya wananchi.
   
 2. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  =Jogoo aliesema
  =Siku ya Gulio Katerero!
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Makubwa haya!! Sisi wazee mnatukumbusha mbali jamani. Halafu tuna nostalgia ya wakati wetu huo!
   
 4. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Baada ya kusoma hadithi - tuliimba wimbo huu tukiwa tumesimama huku tukipiga makofi kuonyesha heshima kwa Kibanga baada ya kumchapa mkoloni.

  *** kibangaaa ampiga mkoloniiiii --- tumsifu tumsifuuuu
  ***kibangaaa ni shujaaa mkuuuu ---tumsifu tumsifuuuuu

  duh - those days bwaanaaaa........
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,946
  Likes Received: 37,199
  Trophy Points: 280
  Sizitaki mbichi hizi
   
 6. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Juma ana dada,dada wa Juma anaitwa Roza..............
   
 7. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Juma anasema...kunywa chai dada, kunywa upesi! Roza una kiu?

  Ha ha ha!
   
 8. U

  Upanga Senior Member

  #8
  Feb 11, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Sadiki mimi maskini je unamkumbuka!!!!!!
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mnawakanyaga wenzenu kama majani ..........
  Kheri mimi sijasemaaa..............
   
 10. M

  Mbonafingi Senior Member

  #10
  Feb 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KARUME KENGE ALIKATAA KWENDA SHULE BABA YAKE AKAMWAMBIA MBWA JE MBWA HUTAKI KUMUUMA KARUME KENGE ILI APATE KWENDA SHULE?. Mbwa akakataa, baba yake akaiendea fimbo akasema, je fimbo hutaki kumchapa mbwa, naye amuume Karume Kenge ili apate kwenda shule? fimbo ikakataa...
  Mbuzi akakubali , akayanywa maji, yakazima moto, ukachoma fimbo ikamchapa mbwa akamuuma karume kenge naye akaenda shule.
  enzi hizo hakukuwa na malumbano ya vitabu vya kiada wala ziada library iko darasani na kila darasa lina kabati limesheheni vitabu. STD 1 Forodhani primary school 1971 darasa moja term 4
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Kapulya apambana na chui.
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Mandenge na mandaw a
   
 13. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,359
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Mandawa na Manenge
   
 14. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,359
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Binafsi nakikumbuka kitabu cha Shida cha Ndyanao BALISIDYA..Na naikumbuka zaidi ile sehemu ambayo Chonya alisema 'If the police come tell Chonya of Chilonwa me take the girl to the hospital'

  Halafu kuna sehemu Chonya akauliza: 'Sipitali iko wapi??'

  Ilikuwa burudani kwa kweli
   
 15. K

  Konaball JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 2,123
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  kula mno ni hasara,
  karudi baba mmoja toka safari ya mbali
  kavimba yote mapaja na kuteteme mwili
  watoto wake wakaja ili kumtaka hali ...
   
 16. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,864
  Likes Received: 2,620
  Trophy Points: 280
  Asante PJ kwa kumbukumbu hizi.
  Marekebisho kidogo ni "Kapulya Mdasisi"
  "Chilunda apambana na Chui"

  Kaaazi kweli kweli.
  Lakini hizi mada zote zimejadiliwa katika mada inayosomeka hivi "Tulipokuwa Primary Unakumbuka?"
  Mada yenyewe iko hapa. Soma nawe utoe machozi ya furaha kwa kumbukumbu hizi.

  Idimi
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,359
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Hahaaaaaaaaa

  Chopeko na mnofu
   
 18. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kwakweli umenikumbusha mbali sana na ninavitafuta sana hivi vitabu sivioni madukani
   
 19. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,864
  Likes Received: 2,620
  Trophy Points: 280
  Vipo. Unaweza kuvikuta maktaba ya taifa, watakuelekeza namna ya kuvipata.
   
 20. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bulicheka na wagagagigikoko! Kabila lao ni huihuihuihuihuihuihui!!!
  NYANI "ABIZIANI" UPOOO??
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...