KIBANDA: Richmond; Lowassa ni kafara sasa JK abebeshwe zigo

Kibanda kumtetea Lowasa? Hapana. Kama nimemwelewa vizuri Kibanda, yeye alitaka serikali nzima iwajibike kwa hili. Ana hoja nzito tu hapo. Angalia hata suala lenyewe lilivyokujamalizika.

Baadhi yetu tunaamini tukijapata Rais makini suala hili litakuja kuanza upya na wahusika halisi kutiwa pingu. Tafsiri ya maneno ya JK mwenyewe pale Diamond baada ya EL kujiuzuru kwamba ile ilikuwa ni "ajali ya kisiasa" yana maana na tafsiri pana zaidi kwa weledi.

Mgonjwa wa Lowasa kwenye TzDaima ni "Mwalimu Mkuu wa Watu", Paschal Mayega.
 
... yaani kuna kipindi anaongea pumba,pumba tu kwa ajili ya kumtetea Lowassa.

Kwa nini unasema amemtetea Lowassa?

Mtu akisema Kikwete amemtoa kafara Lowassa haina maana kwamba amemaanisha Lowassa hayumo kwenye kashfa. Kwa uelewa wangu wa lugha, maana yake ni kwamba Kikwete amemtupia mzigo wa kashfa Lowassa ambae anaweza kuwa yumo kwenye mpango mzima.
 
Nadhani wakati mwingine tusome makala na kuchangia makala na siyo mtu binafsi. Hakuna haja ya kumchambua mwandishi wa habari hii au hata mtu mmoja tu. Tuiangalie habari kwa undani wake kilichoko katika mistari iliyoandikwa.

Mwandishi nadhani ameandika habari ambaye kwa mwenye kuyafikiria mambo kwa undani wake atapata kuondoka na chochote. habari hii si kwa ajili ya kumsafisha Lowasa maana atasafishika natural way. Lowassa hakutajwa kuwa amechkuwa fedha yoyote na kwa kiwango gani bali ripoti tu inasema alikuwa anainfluence ndani yake lakini hiyo haiwezi kumwekea mtu kuwa amechukuwa fedha wakati hajachukuwa. Lowassa hakuchukuwa senti ya Richmond na ripoti imedhihirisha hivyo.

Ukweli ni kwamba CCM n serikali yake hawakufuata process na hilo nddilo lililokuwa tatizo. Na wale wot waliohusika wakiwa watendaji wakuu na si wanasiasa hawakuwa na kesi yoyote ya kujibu kwani hawakufanya kosa lolote ila kwa wanasiasa walifanya makosa.

Inawiwa mtu vigumu kutoamini kuwa hivi havikuwa vita vya kisiasa na has baada ya REDET kutoa taarifa kuwa Lowassa maarufu na anaheshimika na watendaji kuliko JK, vivyo hivyo Regina alikuwa juu kuliko Salma, vyote hivi vinaweza kuwa ni sehemu mojawapo ya process iliyotia mafuta kuondoka kwake.

Lakini ninachoamini, muda ni msema kweli, let wait and see and we who have unbiased eyes can see the yellow and the green and separate them.

1. Angalizo (kwenye red): Ni ukweli kabisa, usiotahitaji hata kutajwa, kwamba Lowassa hakuchukuwa hela ya Richmond, na kashfa hiyo haisemi kabisa kwamba milungula ilitembea kwa yeyote. Richmond ilikuwa ifaidishe watu hao baadaye kutokana na malipo ya Tanesco ya power charges hata pale hawachukui umeme. Hiyo ndiyo ilikuwa asali ya Richmond.

2. Kwa ujumla Kibanda hajasema kitu kipya sana hapa. Wengi wenye ufahamu wanajuwa wazi JK yumo hadi shingoni katika Richmond ila tu kama kawaida yake, mambo yanapokwenda sivyo, basi hujifanya kukaa mbali. Lakini hii haimtoi Lowassa hatiani katika Richmond.
 
Ninavyoona, imefikia time kwa Lowassa kuweka mambo sawa kuhusu Richmond -- kwa kupitia swahiba wake Kibanda -- kwamba hata huyo JK ambaye umma unatakiwa ufikirie kuwa ni msafi katika kashfa hiyo, naye siyo msafi kamwe. mimi nadhani hata wale wengine wawili -- Karamagi na Msabaha nao watajitokeza kuelezea mambo hasa yalivyokuwa, kuna mmoja keshaanza kufanya hivyo kama wiki tatu hivi zilizopita.

Sure, JK asipete kiulaini tu hivihivi katika uchaguzi ujao bila kwanza umma kuelezwa kwamba alitumia nguvu tu kujinasua katika Richmond.
 
Paragraph yenye red: Sina hakika Kibanda alikuwa upande gani (mwaka 2005) wakati mashushshu hao hao walipoandaliwa kuhakikisha wale wagombea tishio kwa JK hawaingii katika eneo la 18. Bila shaka hata Lowassa mwenyewe kwa namna moja au nyingine alishiriki katika ghilba na uharamia huo mkubwa uliofanyika.

Historia hujirudia. Miaka mitatu baadaye, ghilba ya namna hiyo ilifanyika kumuangusha Lowassa! Patamu hapo! Tutasikia mengi mwaka huu!
 
Ninavyoona, imefikia time kwa Lowassa kuweka mambo sawa kuhusu Richmond -- kwa kupitia swahiba wake Kibanda...

Bado sidhani kama akimwambia Kibanda ukweli wote watanzania wataupokea bila kudai 'Kibanda ni fisadi pia' tena 'amelipwa kwa kazi'.

Ila kama kuna wanaokumbuka; kuna siku Lowassa aliamua kuyaweka bayana yote via TBC1 wakamkatia na hakupewa air time tena! Alikuwa ameanza kupandisha hasira na kuamua kuuanika ukweli, matangazo yakakatika. Hakuwahi kusikika tena; ni nini alichokiongea? Nani anaweza kumpa air time Lowassa atueleze alichotaka kukiongea via TBC1 akakatiwa?

Anaweza asiwe msafi, lakini sidhani kama amepewa air time aweze kutueleza who was behind the whole saga.
 
Kwa kweli sioni uhusiano wowote kati ya maelezo ya awali ya Kiranja na makala ya Absalom Kibanda. Makala hii haithibitishi hoja za Kiranja kuwa Kibanda ana uhusiano na Lowassa.

Ni kweli kuwa Kibanda amemfananisha Lowassa na mbuzi wa kafara lakini ukisoma kwa makini hakufanya hivyo kwa minajili ya kumsafisha. Hoja yake ya msingi ya Kibanda ni kuwa wapinzani walipoteza fursa nzuri ya kumuunganisha Kikwete, ambaye kimsingi ndiye kiongozi wa serikali, na baraza lake la mawaziri katika sakata la Richmond na ufisadi kwa ujumla. Kwa mtazamo wa Kibanda serikali nzima ya Kikwete (yaani baraza la mawaziri) ilishiriki katika hatua zote za sakata la ufisadi wa Richmond na hivyo wote walitakiwa kuwajibishwa. Lakini wapinzani waliingia katika mtego wa kukubali kuwa ni baadhi tu ya viongozi wa serikali hii akiwemo Lowassa ndio waliohusika kitu ambacho siyo sahihi.

Vivyo hivyo Kibanda anajenga hoja ya msingi kuwa wapinzani walishindwa kumuunganisha Kikwete na sakata la Buzwagi na kuishia kumshikia bango Karamagi kana kwamba yeye ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa serikali. Kimsingi suala la Buzwagi lilimhusisha moja kwa moja mkuu wa serikali na hivyo alipaswa kuwajibishwa.

Sioni ni kwa jinsi gani suala la Kibanda kuwa kwenye gazeti linalomilikiwa na kiongozi wa Chadema linaingia hapa au ni kwa jinsi gani linahusiana na masuala yanayojadiliwa na Kibanda katika makala hii.
 
Bado sidhani kama akimwambia Kibanda ukweli wote watanzania wataupokea bila kudai 'Kibanda ni fisadi pia' tena 'amelipwa kwa kazi'.

Ila kama kuna wanaokumbuka; kuna siku Lowassa aliamua kuyaweka bayana yote via TBC1 wakamkatia na hakupewa air time tena! Alikuwa ameanza kupandisha hasira na kuamua kuuanika ukweli, matangazo yakakatika. Hakuwahi kusikika tena; ni nini alichokiongea? Nani anaweza kumpa air time Lowassa atueleze alichotaka kukiongea via TBC1 akakatiwa?

Anaweza asiwe msafi, lakini sidhani kama amepewa air time aweze kutueleza who was behind the whole saga.
..Bro Invisible hii ni weak sana..Hivi lazima azungumze TBC1?..
Media ngapi zimejaa?...

...incase vyombo vya ndani vimedhibitiwa...Hivi tangu litokee saga hilo mara ngapi amesafiri nje ya NCHi?..hivi kama yupo serious angeshindwa sema lolote?
 
Kibanda kama anataka tumuelewe kauli ya kusema Lowasa hajachukua hata sent ya Richmond...kaipata wapi? huku akisema serikali yote yahusika..Hivi kama JK kachukua sent...Lowasa atakosa kuchukua sent? wakati zoezi zima yeye ndie Msimamizi?
 
Kibanda inabidi kumuangalia mara 2mbili....Tangu atoe Makala tata ya kumkandamiza Zitto ktk Uchaguzi wa Chadema....anatia waswas...!!!
 
Mtikisiko huo uliojengwa katika misingi ya mazoea tayari umeshavifanya vyama hivyo vikijikuta vikiwa havina mikakati ya wazi hadi sasa ya kumkabili Kikwete katika ngazi ya urais na badala yake kwa ushawishi wa mazingira na uzoefu vimejikuta vikijizatiti zaidi katika ngazi za ubunge na udiwani.

Hivi utautakaje urais (ambao uko kwenye ngazi ya kitaifa) kama hujajizatiti kwenye mizizi (ngazi ya chini kabisa) yaani ubunge na Udiwani..?

Tafakari yangu binafsi inanionyesha bayana kwamba dhambi mbaya iliyofanywa na kambi ya upinzani ya kushabikia kwa mazoea tu, siasa za kinazi za CCM ndiyo ambayo kwa kiwango kikubwa imemfanya Kikwete na chama chake kuendelea kung'ara hata katika mazingira ambayo yalipaswa yawe yamemuangusha.
Hivi kweli Kikwete anang'ara...?? sidhani..!labda kwa wafuata upepo ambao hao hatuna jinsi ya kuwasaidia..!

Kwangu miye kama ilivyo kwa baadhi ya watu wenye mawazo na mtazamo kama wangu, ingekuwa katika nchi zilizostawi kidemokrasia na kimaendeleo kama ilivyo Tanzania, ilitosha kwa wapinzani kupata mwanya wa kumuangusha Kikwete na serikali yake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa kutumia hoja moja tu ya ufisadi.

Hili haliwezekani kwa Tanzania yetu hii...labda kwa nchi zilizoendelea (zenye wananchi wenye kujali mustakabali wao na wenye uelewa) ...Kwa Tanzania hii ambayo Fisadi anashangiliwa kuwa ndio mjanja haliwezekani...bado!

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba hata baada ya baadhi yetu kubaini njama hizo za CCM na za makachero mapema kabisa, na kuziandika katika safu kama hii na katika mijadala ya wazi, baadhi ya viongozi shupavu wa kambi ya upinzani walikuja juu wakitunyoshea vidole na wakati mwingine kutuzushia kashfa ambazo ni vigumu kuziweka katika maandishi leo hii.
Para hiyo juu inaonesha kuwa muandishi aliandika makala hii kwa msukumo fulani..! na hivyo kumuondolea "credibility"...kuna harufu ya kinyongo hapa..! na hivyo muandishi hawezi kuwa "objective" kwenye hoja zake..!
 
Kibanda is making a lot of Sense, hebu tuache ushabiki na chuki tutafakari hoja zake tuzijibu kwa Hoja, tuache kumshambulia Kibanda kama Kibanda bali tuangalie kama Hoja zake zina make any Sense?

I will come back later kwa sasa sina comment bado
ukishabikia ujinga nawe utaitwa mjinga ukitenda maovu nawe utaitwa mtenda maovu, wanao mmtaka lowassa 2015..... si dhani wapo sahihi kwa wayasemao ila wanajaribu kupima imani za watu na kujua ni kiasi gani anavyokubalika au au asivyokubalika WATANZANIA msichanganywe na maneno matamu pimeni wenyewe kisha chukueni hatua ....
 
There is a lot of sense in what Kibanda has put forward. It true that thie year the opposition will not gain as they did in 2005 especially on the presidential side. Perhaps this time they may agree to announce Hamad as the winner. You only need to read carefully between the lines to get sense out of Kibanda's column. As he promised, we will continue to read until we get where he is heading but the truth is JK is stronger now and opposition is weaker now than before!!!!
 
Naamini sana yote yasemwayo na nayatafakari sana na kwa kina....ila naogopa sana tanzania daima maana Lowasa amewakaa sana akilini mwao....namuogopa sana Lowasa maana ana nguvu za ajabu sana kama RA sasa...Membe na wenzake wakae sana chonjo
 
Personally huwa sipatani na Kibanda kwa hoja nyingi na nakala nyingi sana,

Sisiti kusema kwa mara ya kwanza nimeona nakala ambayo ndiyo hasa zinatakiwa kwa wengi wetu wenye tabia za ushabiki na kuingia porini.

Excellent article,explained logically ambao wenye uelewa mzuri wa political styles, hii haswa imeeleza ukweli,

alichosema ni kuwa, wapinzani hamna kitu, hilo nadhani halina ubishi, Mwakyembe alieonekana shujaa wa watanzania is actually 'the' traitor! yaani kila kinachoonekana na kusemwa na kufanywa , mara nyingi sio ukweli wake

Haya sasa Richmond iko wapi? mafisadi nchi hii na wote wanaopelekwa mahakamani huwa wanarudisha fedha?

Richmond issue na kuresign kwa Lowassa ndio kumempa sifa Kikwete even outside our boundary! sifa ya Kikwete in global levele ni kubwa mno, wakati actually very same and only guy who was supposed to be responsible for richmond!

Ona sasa wapinzani wote hoi, aibu hata kusema kuna chadema, cuf, sijui nani......

Big up Kibanda but it is 'too late! why?
 
Ndugu zangu, kuna wakati Dr. Mwakyembe alipoandamwa sana kwamba amepika ripoti aliwahi kutamka maneno haya: "Nitafyatuka!!!" Ni vizuri kuitafakari kauli hiyo. Na kama tuna kumbukumbu nzuri ni baada tu ya Mwakyembe kusema nitafyatuka, ndipo yale maneno maneno ya kwamba akina mwakyembe wamepika report ya richmond yaliisha. Ninyi mnafikiri Mwakyembe angefyatuka nini? Ni dhahiri kwamba mkuu wa kaya alishiriki kikamilifu, isipokuwa kilichofanyika ni kuepusha uwezekano wa serikali nzima kutakiwa kujiuzulu. Na Lowassa na washirika wake walijiuzulu kulinusuru taifa. Tukubali tukatae... Na ile kauli ya Mwakyembe ya nitafyatuka ilikuwa inamaanisha kwamba iwapo angeendelea kusakamwa basi angeusema ukweli kama ulivyo, jambo ambalo pengine lingemtaka Kikwete ajiuzulu. Ni mtizamo wangu tu, msininukuu.
 
Back
Top Bottom