KIBANDA: Richmond; Lowassa ni kafara sasa JK abebeshwe zigo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KIBANDA: Richmond; Lowassa ni kafara sasa JK abebeshwe zigo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Apr 15, 2010.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Jamani naomba kuwasilisha,

  KWA KUWA, makala hii imeandikwa na Kibanda, ambaye ametajwa kuwa karibu na Lowassa,
  NA KWA KUWA, amesema kwamba Lowassa alikuwa mbuzi wa kafara,
  NA KWA KUWA, yuko katika gazeti linalomilikiwa na kiongozi wa CHADEMA,
  NA KWA KUWA ameonyesha kwamba kuna udhaifu ndani ya wapinzani wakiwamo CHADEMA,
  NA KWA KUWA Lowassa alikuwa karibu sana na JK kabla, alipokuwa na baada ya Uwaziri Mkuu,
  NA KWA KUWA sasa haijulikani kama bado JK ana mahusiano na Lowassa,

  HIVYO basi Lowassa anataka JK atwishwe mzigo na wapinzani sasa wahamishe nguvu zao kumng'oa JK na serikali yake nzima kwenye uchaguzi ujao wa 2010 na baadaye sasa Lowassa aonekane safi baada ya 2010 ili awe RAIS WETU 2015.

  Naoma kuwasilisha.


  Tunapumbazwa na ushabiki wa kijinga
  [​IMG]

  Absalom Kibanda


  NI jambo la kheri kwangu na kwa wasomaji wa safu hii ya ‘Tuendako’ kwamba nimepata fursa hii adhimu kuendeleza mjadala nilioanza nao upya wiki iliyopita baada ya kuusitisha kwa miezi kadhaa. Naamini wasomaji waliopata wasaa wa kuisoma mada hiyo kuhusu adha ya ushabiki katika medani ya siasa wiki iliyopita, watakuwa na wakati bora zaidi wa kuufuatilia na kuelewa mwelekeo wangu wa hoja kuhusu suala hilo ambalo kwa maono yangu, naliona kuwa ni moja ya matatizo ya msingi ya kimtazamo yanayotukabili Watanzania tulio wengi kwa miaka mingi.

  Uzoefu ambao Watanzania tuliupata kutokana na matukio makubwa mawili niliyoyataja na kuyajadili katika makala iliyopita nikianza na kishindo cha kundi la G 55 lililokaribia kabisa kulimega taifa katika vipande vipande na lile la mvumo wa Augustine Mrema kujitoa CCM, kujiunga na NCCR Mageuzi kabla ya kugombea urais mwaka 1995 ulipaswa kuwa fundisho la msingi kwetu.

  Ni jambo la bahati mbaya kwamba, hata baada ya matukio hayo makubwa mawili kulikumba taifa na kufuatiwa na mengine mengi mengine ya namna hiyo hiyo, uzoefu umeonyesha na kuthibitisha kuwa ugonjwa huo wa kuendekeza ushabiki tena katika misingi ya hovyo limekuwa ni donda ndugu.

  Baya zaidi katika hilo ni kwamba matokeo ya udhaifu huu wa Watanzania tulio wengi ndiyo ambao umekuwa ukitumiwa kama silaha ya ushindi na baadhi ya wanasiasa na wataalam wa propaganda wa Kitanzania waliosoma katika mifumo wa kikomunisti duniani wanaofanya kazi katika taasisi kadha wa kadha za kikachero hapa nchini.

  Leo hii unapotazama, kuyatafakari na kuyapima kwa kina baadhi ya mambo yanayotokea hapa nchini leo hii na mengine yaliyopata kutokea katika miaka ya karibuni ni rahisi kabisa kuthibitisha na kuona kwa uwazi mkubwa namna hulka za kishabiki zilivyofikia hatua ya kutuyumbisha kama taifa.

  Moja miongoni mwa hayo ambalo, wadadisi wengi wa mambo wamepata kuliandika na kulitafakari ni lile linalogusa jina la Rais Jakaya Kikwete kabla hajaingia madarakani na hata baada ya kuyapata madaraka hayo makubwa nchini.

  Ni wazi kwamba umuhimu wa mjadala ulio wazi na unaofanywa katika misingi ya haki na isiyotawaliwa na ushabiki juu ya Kikwete unaweza ukawa muhimu leo kuliko ilivyokuwa wakati mwingine wowote kabla.

  Kikubwa kinachotulazimisha Watanzania kama taifa kumjadili Kikwete si tu kama mtu binafsi bali pia kama kiongozi mkuu aliye na dhamana kubwa ya kutuongoza ni ukweli kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu ambao unamgusa moja kwa moja, yeye binafsi, serikali, vyama mbalimbali vya siasa kikiwamo chama chake na wananchi kwa ujumla.

  Lakini kikubwa katika yote hayo ni ukweli kwamba, tunaingia katika uchaguzi huo wakati taifa na hususan kizazi cha wapiga kura na viongozi kikiandamwa na ugonjwa mbaya kabisa wa kuendekeza ushabiki ambao aghalab msingi wake ni jazba, unazi na kwa upande mwingine chuki na husuda.

  Ni wazi kwamba, iwapo kama taifa tuendelea kuendekeza hulka tunazoziona leo hii za wapenzi na mashabiki wa Kikwete na manazi wa CCM kutoa matamshi na kuchukua hatua za kumuunga mkono kiongozi huyo kwa mbwembwe nyingi ili mradi tu ateuliwe na chama chake kuwa mgombea urais na hatimaye apate ushindi mnono Oktoba, tutakuwa tumetimiza matamanio ambayo hayana msingi wowote wa maana.

  Ni katika misingi hiyo hiyo pia tutakuwa tukifanya kosa kubwa la ukiukwaji si tu wa misingi ya kidemokrasia bali pia ya kizalendo, iwapo kama taifa, tutakubali kijuu juu kubebwa na ushabiki wa kinazi na makundi ya watu yenye chuki na husuda binafsi ama na Kikwete, serikali yake au chama chake.

  Hata hivyo, kwa namna mambo yanavyokwenda sasa hivi, upepo umeshaanza kuonyesha na kimsingi unaendelea kuonyesha wazi kwamba, ushabiki unaojengwa ndani ya CCM na nje unazidi kumuweka Kikwete katika nafasi kubwa ya kupitishwa na chama chake kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu ujao kuliko ilivyo kwa mwingine yeyote ndani na nje ya chama hicho.

  Ni jambo la kusononesha kwamba upepo huo mbaya unaovuma ndani ya CCM leo hii ambao ni wazi umeanza kuwaathiri wananchi walio wengi, unaonekana kwa namna moja au nyingine umefikia hatua ya kuvitikisa vyama vya upinzani.

  Mtikisiko huo uliojengwa katika misingi ya mazoea tayari umeshavifanya vyama hivyo vikijikuta vikiwa havina mikakati ya wazi hadi sasa ya kumkabili Kikwete katika ngazi ya urais na badala yake kwa ushawishi wa mazingira na uzoefu vimejikuta vikijizatiti zaidi katika ngazi za ubunge na udiwani.

  Ukigeuka nyuma na kutafakari ni kitu gani hasa kilitokea hata kusababisha hali hii ya mambo kuwa hivi ilivyo hata kusababisha Kikwete, ambaye hakuna shaka rekodi yake ya uongozi mkuu wa nchi inaibua maswali mengi pengine kuliko majibu kuonekana akipata nafasi kubwa kuliko mwingine yeyote ndani na nje ya CCM ya kuendelea kuongoza nchi kwa muhula wa pili.

  Tafakari yangu binafsi inanionyesha bayana kwamba dhambi mbaya iliyofanywa na kambi ya upinzani ya kushabikia kwa mazoea tu, siasa za kinazi za CCM ndiyo ambayo kwa kiwango kikubwa imemfanya Kikwete na chama chake kuendelea kung’ara hata katika mazingira ambayo yalipaswa yawe yamemuangusha.

  Kwangu miye kama ilivyo kwa baadhi ya watu wenye mawazo na mtazamo kama wangu, ingekuwa katika nchi zilizostawi kidemokrasia na kimaendeleo kama ilivyo Tanzania, ilitosha kwa wapinzani kupata mwanya wa kumuangusha Kikwete na serikali yake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa kutumia hoja moja tu ya ufisadi.

  Katika hili wapinzani walipaswa kuhakikisha tena kwa msisitizo na kwa vielelezo vyenye ushawishi, wanafanya kila liwezekanalo kuitumia hoja ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuhusu kuwapo kwa mazingira ya rushwa katika mkataba wa Buzwagi kuiunganisha serikali nzima katika sakata hili badala ya kunaswa katika mtego rahisi wa kumsakama aliyekuwa Waziri wa Nishati, Nazir Karamagi.

  Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, hata baada ya Zitto kupata umaarufu mkubwa kutokana na hoja hii ya Buzwagi kwa kiwango cha kulitikisa taifa, kambi ya upinzani ambayo awali ilionekana kuwa nyuma ya mbunge mwenzao ndani na nje ya Bunge, taratibu ilionekana kuanza kuyumba kabla ya ajenda yao nzima kuporomoka na kuzimwa.

  Katika mazingira ambayo si rahisi kuyaeleza, wabunge wa upinzani, wakiongozwa na Zitto mwenyewe kwa kujua au kutokujua walionekana wakifanya juhudi kubwa kumsakama Karamagi na kuiacha serikali nzima ikiwa safi.

  Huku wakijua fika kwamba, Karamagi alikuwa ni mteule wa rais ambaye alikuwa hana mamlaka ya kuingia katika mkataba mkubwa kama ule uliohusisha kampuni kubwa yenye jina kubwa la Barrick, pasipo kulishirikisha Baraza la Mawaziri na pengine Kikwete binafsi, wapinzani walionekana wakitishwa na kivuli cha urais na kuishia kumwandama mtu mmoja.

  Hoja za wapinzani hao kwamba eti Karamagi alisaini mkataba huo kinyume cha ahadi ya rais ya kutosainiwa kwa mkataba mwingine wowote mpya wa madini kabla ya kutungwa kwa sheria mpya, iligeuka kichekesho baada ya rais mwenyewe kuendelea kumwacha mwanasiasa huyo akiendelea kubakia madarakani hata baada ya kusakamwa kote huko.

  Ni wazi kwamba, kambi nzima ya upinzani ambayo iliibua hoja nzito kabisa ilishikilia msimamo wao wa kutaka kuona Karamagi akianguka huku ikisahau kuwa, historia ya mawaziri kuangushwa kwa kashfa za kisiasa hapa nchini, tangu walipoanguka, Profesa Simon Mbilinyi, Dk. Hassy Kitine na Iddi Simba hazikupata kuiteteresha serikali na rais aliyepo madarakani.

  Mbaya zaidi ni kwamba, hata baada ya wapinzani kukwamishwa na mahesabu mabaya ya kishabiki katika sakata hilo la Buzwagi walijikuta wakiingia tena katika mtego huo huo miezi kadhaa baadaye katika sakata la Richmond ambalo kama lingetumiwa sawasawa lingeandika historia bora kabisa ya uwajibikaji wa kiserikali katika taifa hili.

  Katika hili nalo, kambi nzima ya upinzani ilijikuta ikipigwa chenga ya mwili na makachero wa kisiasa na kidola wa CCM ambao walikuwa na lengo moja tu la kuhakikisha rais anayetokana na chama chao na serikali haanguki na hachafuliwi kwa namna yoyote katika sakata hili.


  Ili kufanikisha ajenda hii muhimu, nyeti na ya siri, makachero hao walilazimika kujipanga sawa sawa ndani na nje ya Bunge na wakapenya hadi katika Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe na kuhakikisha inaandaliwa ripoti ya kishushushu ambayo hatimaye ilifanikiwa kuiokoa serikali. Huku wakijua fika kwamba gharama ya kufanikisha azma hiyo ilikuwa kubwa, makachero hao wakauhadaa umma kwa kuwatoa kafara, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na mawaziri wengine wawili: Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha.

  Yalipofanyika hayo, haraka haraka na pasipo kujua kuwa walikuwa wakitafunwa na laana ya ushabiki, wapinzani wakajikuta wakifanya kosa kubwa la kushangilia matokeo ya kina Lowassa, Karamagi na Msabaha kuanguka, huku wakisahau kwamba hesabu zao hizo zilikuwa zikimjenga zaidi Kikwete, serikali yake na chama chake.

  Matokeo ya kundi kubwa la wanasiasa wa kambi ya upinzani kuungana na makachero wa CCM katika sakata hili la Richmond, yalikuwa ni kusalimika kwa serikali na Kikwete mwenyewe hata baada ya kuwapo kwa mazingira ya wazi kwamba vikao vyote vya baraza la mawaziri vilivyojadili Richmond viliongozwa na yeye na kila maamuzi ambayo ama yalifanywa na Lowassa, Msabaha au Karamagi yalikuwa na baraka au maelekezo yake.

  Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba hata baada ya baadhi yetu kubaini njama hizo za CCM na za makachero mapema kabisa, na kuziandika katika safu kama hii na katika mijadala ya wazi, baadhi ya viongozi shupavu wa kambi ya upinzani walikuja juu wakitunyoshea vidole na wakati mwingine kutuzushia kashfa ambazo ni vigumu kuziweka katika maandishi leo hii.

  Maradhi haya ya kushabikia mambo yaliyoikumba kambi ya upinzani iliyokuwa ikiongozwa na majemedari kadhaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mara moja yalianza kuwakumba wananchi kwa staili ya kuambukizana.

  Maambukizi haya ndiyo ambayo hatimaye yalisababisha majemedari wa kweli wa vita ya ufisadi wasiwe tena kina Zitto, Dk. Wilbrod Slaa, Freeman Mbowe na wenzao na badala yake sifa zikawaendea wabunge wapambanaji ndani ya CCM waliokuwa wakiongozwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

  Matokeo haya ya mabadiliko ya upepo, yalikuwa ni hatua ya kwanza muhimu iliyoanza kujenga upya taswira ya Kikwete iliyoanza kuonekana ikipwaya katika macho ya wananchi kabla ya upepo huo kuendelea kubadilika na kulifikisha taifa hapa tulipo leo. Tutaendelea na mada hii wiki ijayo.
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Daima nimekuwa nikitilia shaka maoni na mawazo ya Kibanda hasa katika Issue zinazomuhusu Lowassa, maana amekua akijitoa muhanga kutuletea utetezi wake, kweli inafikirisha.
   
 3. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kazi kubwa sana, hapo ndio mjue huyo anakuja kuwa Rais wenu, mtake msitake, asiyetaka atafute pwa kwenda kama siye, maana tushajijua hakuna kati yao woooote atakayeweza hata huyo Mpendazoe, ni wale wale mzao wa kifisadi, watatudanganyia pipi watumalize
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kweli inafikirisha
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kumbe ufisadi una maana pana kuliko wengi wetu tujuavyo!

  This is ana organized group of criminals, fully furnished with all the necessary machineries and equipment to rip out Tanzania!

  Mungu Ibariki TANZANIA!
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli Kiranja ameibua jambo zito sana.
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,082
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi Kibanda ndiye alienifanya nilichukie gazeti la Tanzania Daima....!!potelea mbali hata watu niliokuwa na wakubali kama Ansbert Ngurumo nao imebidi niwaache japo kwa masikitiko.
  Sijui alipewa nini na Lowassa???? yaani kuna kipindi anaongea pumba,pumba tu kwa ajili ya kumtetea Lowassa.
   
 8. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kapewa Sabuni ya Roho kama ile aliyopewa Yuda Iskariyote
   
 9. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  No amount of soap or lye can make you clean. I still see the stain of your guilt. I, the Sovereign LORD, have spoken!
  (Jeremiah 2:22)
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Sote tufahamu kuwa media is very strong, especially to politicians!!! Watakubomoa au kukujenga!!! Editors, please tusaidieni tuikoe Tanzania, your role is crucial guys!
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kibanda is making a lot of Sense, hebu tuache ushabiki na chuki tutafakari hoja zake tuzijibu kwa Hoja, tuache kumshambulia Kibanda kama Kibanda bali tuangalie kama Hoja zake zina make any Sense?

  I will come back later kwa sasa sina comment bado
   
 12. N

  Nanu JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani wakati mwingine tusome makala na kuchangia makala na siyo mtu binafsi. Hakuna haja ya kumchambua mwandishi wa habari hii au hata mtu mmoja tu. Tuiangalie habari kwa undani wake kilichoko katika mistari iliyoandikwa.

  Mwandishi nadhani ameandika habari ambaye kwa mwenye kuyafikiria mambo kwa undani wake atapata kuondoka na chochote. habari hii si kwa ajili ya kumsafisha Lowasa maana atasafishika natural way. Lowassa hakutajwa kuwa amechkuwa fedha yoyote na kwa kiwango gani bali ripoti tu inasema alikuwa anainfluence ndani yake lakini hiyo haiwezi kumwekea mtu kuwa amechukuwa fedha wakati hajachukuwa. Lowassa hakuchukuwa senti ya Richmond na ripoti imedhihirisha hivyo.

  Ukweli ni kwamba CCM n serikali yake hawakufuata process na hilo nddilo lililokuwa tatizo. Na wale wot waliohusika wakiwa watendaji wakuu na si wanasiasa hawakuwa na kesi yoyote ya kujibu kwani hawakufanya kosa lolote ila kwa wanasiasa walifanya makosa.

  Inawiwa mtu vigumu kutoamini kuwa hivi havikuwa vita vya kisiasa na has baada ya REDET kutoa taarifa kuwa Lowassa maarufu na anaheshimika na watendaji kuliko JK, vivyo hivyo Regina alikuwa juu kuliko Salma, vyote hivi vinaweza kuwa ni sehemu mojawapo ya process iliyotia mafuta kuondoka kwake.

  Lakini ninachoamini, muda ni msema kweli, let wait and see and we who have unbiased eyes can see the yellow and the green and separate them.
   
 13. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Inataka TAFAKURI makini. Ni kweli CCM na mfumo mzima umeoza, lakini je, ndio uozo wa CCM, JK, na mfuko mzima unatosha kumsafisha LOWASSA?
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wapi Makala hii imesema Lowasa ni Msafi?
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Na hatimaye wale waliokuwa wansema JK anaangushwa na Watendaji wake Wakashinda kwa Hoja
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Na sasa umaarufu wa Kikwete unawatisha wapinzani wake Ndani na Nje ya CCM
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Bado nawaza sana!
   
 18. Y

  YE JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye nyekundu pana make a lot of sense ukizingatia 1+1.....
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwa Lowassa hana hata chembe cha usafi, lakini ndugu zangu ukweli utabaki pale pale kuwa mhusika mkuu katika sakata la Richmond alikuwa ni Jakaya Mrisho Kikwete.

  Alichofanya Lowassa kwa kujiuzulu nafasi yake ni kumsaidia mshikaji wake na timu nzima ya mafisadi kubaki madarakani. Siku ukweli utakapofichuka wengi mtabaki midomo wazi kwani kamati ya Mwakyembe pamoja na kumshutumu Lowassa iliamua kufunika kombe kwa kuficha ukweli kuilinda serikali isibaki uchi.

  Mwenye akili atatambua mara moja waliyekuwa wanamsetiri ni nani !
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jun 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu mimi nimemsoma mwandishi na hakika anavilaumu vyama vyote vya Upinzani kwa Ujumla wao wameuziwa mbuzi ktk gunia.

  Tatizo letu Wadanganyika siku zote tunasoma majina ya watu kisha tunayatafutia issues badala ya issues zenyewe kutupa majina ya wahusika.. Sakata la Buzwagi, BoT na Richmond haya yote yalikuwa yakimalize chama CCM kiuongozi. The fact that CCM came out of that inaonyesha wazi jinsi siasa za Bongo zisivyokuwa na sura.

  Lakini haina maana Lowassa, Karamagi na Msabah were innocent, hawa walikuwa Kafara ya chama wakihakikishiwa usalama wao ili chama kipate kuendelea kutawala.. Na kafara iliweza kufanya kazi kwani CCM bado wanaongoza na hakuna Mpinzani mbadala..Kina Lowassa ni majina yaliyotokana na kukisalimisha chama. Hii ndio maana haswa ya mwandishi nilivyomsoma mimi..Kama mnakumbuka vizuri JK alibadilisha baraza zima la Mawaziri wakatoka wengi tu kina Meghji, Rostam, Chenge na wengineo lakini bado wana nguvu ndani ya chama kwa heshima zote.

  Hakika mwandishi anatuonyesha jinsi tulivyo WAJINGA na wepesi sana wa kunyoosha vidole hali kitulacho kii nguoni mwetu..Upinzani hakuna jamani hakuna! Soote tuliachia pale tulipotakiwa kukandamiza hadi CCM waachie ngazi lakini badala yake tukawa watetezi wa CCM na serikali ya JK, wengine tukitoa heko na pongezi kwa Lowassa kujiuzuru pasipo kujua kwa nini Lowassa as a Prime minister alikubali kujiuzuru pasipo kusimama kujibu mashtaka. Kujiuliza huko kujiuzuru kwao kutaathiri vipi mashtaka dhidi ya viongozi ambao wamevunja sheria lakini tayari wamekubali kuachia ngazi huku wakidai wao ni innocent - wasidai kufikishwa mahakama kuitafuta haki..

  Na kina sie tukaridhika na uamuzi ule kwa roho safi na kushangilia - mchezo umekwisha! CCM imeongoza kwa miaka mitano saaafi na wamekula haswaaaa..na bado wanachukua tena mwaka 2010 na hata 2015 kwa sababu kama Upinzani ulishindwa kutumia UFISADI kuiondoa CCM sidhani kama kuna sababu nyingine yeyote kiutawala inayoweza kuzidi Corruption!

  2015 Wapinzani watakuja na silaha gani...hawana silaha yoyote 2015 ya kuwavuta wananchi maskini... Matukio yoote haya yatabakia hadithi za simulizi kama kawaida yetu ya unafiki -Tunamlaumu Nyerere baada ya.....
   
Loading...