KIBANDA : Mambo haya si ya bahati mbaya

Izz

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
750
318
"Nikiwa bado Muhimbili kabla ya kupelekwa Afrika Kusini, nilizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova; na nilipokua Afrika Kusini nilitembelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi na kwamba wote waliniahidi serikali ingefanya kila linalowezekana kuwakamata wahalifu hao.

Hata Rais Jakaya Kikwete alinitembelea hospitalini Milpark, alinieleza maneno hayo hayo. Lakini leo ni miezi mitatu, hakuna mtu aliyekamatwa. Hili ni jambo la kusikitisha sana; inanifanya ni muulize Mungu kwa nini aliruhusu niwe hai hadi sasa" Absalom Kibanda, M/Kiti Jukwaa la Wahariri Tanzania

SOURCE: Mawio
Kwa habari zaidi soma gazeti hilo.
 
hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
kibandaaa nawewe nae unadanganyishiwa pipi?
sijategemea duuuuu pole sana we endelea kuchapa
kazi hayo yasahau na usirudie tena kubishana na hao
jamaa watakurestisha.
 
Wee Kibanda,watu waliomuua aliyekua mkurugenzi TISS-Amran Kombe,walihukumiwa kifo,cha ajabu wapo mtaani sasa wamepata msamaha ambao Jk na Mkapa wanatupiana mpira nani kawapa.
 
"Nikiwa bado Muhimbili kabla ya kupelekwa Afrika Kusini, nilizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova; na nilipokua Afrika Kusini nilitembelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi na kwamba wote waliniahidi serikali ingefanya kila linalowezekana kuwakamata wahalifu hao.

Hata Rais Jakaya Kikwete alinitembelea hospitalini Milpark, alinieleza maneno hayo hayo. Lakini leo ni miezi mitatu, hakuna mtu aliyekamatwa. Hili ni jambo la kusikitisha sana; inanifanya ni muulize Mungu kwa nini aliruhusu niwe hai hadi sasa" Absalom Kibanda, M/Kiti Jukwaa la Wahariri Tanzania

SOURCE: Mawio
Kwa habari zaidi soma gazeti hilo.

Pole sana Kibanda, wee tulia Mshukuru Mungu kwa kukupa uhai uendelee kushuhudia uchafu ulio zaliwa Tanzania, Tanzania ya sasa ipo tofauti sana, watu wapo Tayari kumtoa mtu roho ili kutaka ku-justfy kitu kidogo sana cha kisiasa, hebu niambie huu ni utu kweli mtu anafanya fitna zinazo sababisha mtu ateseke, asikae na familia yake, ikiwezekana afe kabisa aiache familia yake ikiteseka huku waliosababisha unyama huo wametulia majumbani mwao na familia zao zenye furaha wakipongezana kwa E-mail za KUDOZ as if wao ndo wanastahili kuishi vizuri hapa Tanzania. To me naamini wanaofanya unyama huu ni Dolar, na ndo wenye uwezo wa kumfanya wawezalo mtu na kumfumba mdomo kwa ghalama zozote zile sidhani kama mimi Mvaa Tai naweza nikamfanyia unyama mtu kama aliofanyiwa Dr Ulimboka na akaamua tu from nowhere awe kimya kabisa, posible ametishwa kwamba akiendelea na mdomomdomo watamtupa kwenye Kisima cha maji, hivyo nakushauri hata wewe kaa kimya ulee familia yako.
 
Eng. Y. Bihagaze nafikiri angeongea kile anachojua na kilichomtokea kama aanamhisi mtu yoyote au ana taarifa za wabaya wake wowote au kuna mkono wa mtu au serikali maana sometime haya mambo yatakaishia kama ya Dr Ulimboka hakuna aliyekamatwa"mhusika "mkuu zaidi ya kukamatwa kwa mkenya ambaye matukio yalishindwa kuumuunganisha na utekaji huo na yeye Dr kuishia kisema anamwachia Mungu.
Ukishaona inteligensia ya polisi haina majibu kwa miezi mitatu fanya private investigation kumpata muhusika
Issue ya Padre wa Zanzibar ya Shekhe aliyemwagiwa tindikali hakuna aliye kwenye vyombo vya sheria kama "mhusika mkuu zaidi ya bla bla
 
Last edited by a moderator:
Wale misukule wa Chama cha wangoa meno,kucha na kutoboa macho kwenye uzi kama huu hawatakanyaga kwani wanajua aliefanya haya yote ni Mwigulu Nchemba kwa kushirikiana na usalama wa kikwete..
 
Last edited by a moderator:
We Kibanda kaa kimya.Ila kama unataka kulazwa mahali pema peponi kabla ya wakati endelea kuropoka.
 
Eng. Y. Bihagaze nafikiri angeongea kile anachojua na kilichomtokea kama aanamhisi mtu yoyote au ana taarifa za wabaya wake wowote au kuna mkono wa mtu au serikali maana sometime haya mambo yatakaishia kama ya Dr Ulimboka hakuna aliyekamatwa"mhusika "mkuu zaidi ya kukamatwa kwa mkenya ambaye matukio yalishindwa kuumuunganisha na utekaji huo na yeye Dr kuishia kisema anamwachia Mungu.
Ukishaona inteligensia ya polisi haina majibu kwa miezi mitatu fanya private investigation kumpata muhusika
Issue ya Padre wa Zanzibar ya Shekhe aliyemwagiwa tindikali hakuna aliye kwenye vyombo vya sheria kama "mhusika mkuu zaidi ya bla bla

Mkuu nikuhakikishie kwa kuwa serikali inahusika kwa maswala haya kamwe uchunguzi hautakamilika mimlele labda chama kingine kiingie madarakani, Kubenea anaushhidi wa walio mkatakata na kikwete anajua kuwa kubenea anawajua, Dr Ulimboka hivyo hivyo, Mwakyembe na sasa Kubanda na kupa siku chache habari ya kubanda itafutika kama zingine kwasababu vitendo hivyo viovu havifanywi kwa bahati mbaya ni vya kupangwa na wakubwa wanajua kuwa wanao fanya hivyo wako kwenye haraka za kuokoa chama chao...
 
Eng. Y. Bihagaze nafikiri angeongea kile anachojua na kilichomtokea kama aanamhisi mtu yoyote au ana taarifa za wabaya wake wowote au kuna mkono wa mtu au serikali maana sometime haya mambo yatakaishia kama ya Dr Ulimboka hakuna aliyekamatwa"mhusika "mkuu zaidi ya kukamatwa kwa mkenya ambaye matukio yalishindwa kuumuunganisha na utekaji huo na yeye Dr kuishia kisema anamwachia Mungu.
Ukishaona inteligensia ya polisi haina majibu kwa miezi mitatu fanya private investigation kumpata muhusika
Issue ya Padre wa Zanzibar ya Shekhe aliyemwagiwa tindikali hakuna aliye kwenye vyombo vya sheria kama "mhusika mkuu zaidi ya bla bla

Jamaa anaongea.. Napenda sana watu jasiri..

ni ngumu sana kupambana na system, matokeo yake huja baada ya muda mrefu sana kupita!
 
Huyu kaka asitafute hata umaarufu kwenye media
kama umaarufu angeupata ulimboka, lakini yako wapi,
kwa kuwa amepona afanye kazi zake aangalie na familia yake
kufa ni mara moja tu na hautarudi tena milele. Mshukuru sana Mungu wako kwa kuwa bado upo.
 
Kibanda tulia ndugu yangu, hao hata uwapigie gitaa utaishia kucheza mwenyewe tena wakiona gitaa linanoga kusulubiwa bila ganzi inakuhusu or wakurest in peace kabisaa.

Shukuru Mungu umzima sasa, na Mungu atawaumbua na kuwahadhibu kwa wakati wake
 
Pole Kibanda maana hatawamelazimisha kusema eti ni mambo ya wanawake za watu ndio sababu ya kuteswa kwako!sidhani wale wamefunzwa ile kazi na ni wataalamu ambao wamesomea kabisa wala sio wahuni wa kulipiza visasi vya mambo ya wanawake uswahilini!
 
Kibanda usijute kuzaliwa tanzania...ata watakaokamatwa si wahusika halisi watakuwa kama yule wa uli waliyekamata kichaa tanzania ya baba nanii ni zaidi ya huijuavyo...waliokufanyia unyama ni maadui wa kisiasa wa mabosi wako na wa kalamu yako....god bless u kibanda...say hello to all...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom