Uchaguzi 2020 Kibamba: CHADEMA wadai Mwanachama wa CCM amechukua fomu ya kugombea Ubunge kwa jina lao

hapa walotendwa ni wote ,yaani tume ya uchaguzi na chadema .sasa nashangaa kuona tume inaona ni kitendo cha sawa . Maajabu ya mwaka .

sasa hapa kuna uzi uliletwa humu ya kuwa chadema wajiandae kisaikolojia . yaliyofanyika serikali ya mitaa yatajirudia tena . nchi ni ya amani kwa nini tuichafue .
 
ukiruhusu hili kesho litakuja kundi jingine kuchukua fomu so itakua chaos mkuu
Hapana, haitakuwa chaos na haipaswi kuwa hivyo. Uwekwe utaratibu ambao hautaruhusu barua tu ndiyo iwe kigezo cha kuchukua fomu.
Wanaweza kuweka utaratibu wa kuweka picha kwenye barua. Sura ya huyo mgombea fake ingeonekana. Hivi hakuna cctv camera kwenye hiyo ofisi?
Tujifunze kutokana na makosa na wala siyo kufanya makosa ili tujifunze. Litakuwa ni kosa kubwa sana kumnyima mgombea halali ambaye viongozi wa chama chake ndiye wanamtambua, eti kwa sababu kuna mgombea mwingine fake aliyeleta barua fake. Hiyo barua viongozi wameikana, sasa kuna shida gani kutoa fumo kwa huyo mgombea halali? Unadhani huyo fake ataridisha hhiyo fumo?
 
Aliyekuwa meya wa ubungo Jacob Boniface amesema kuwa mwanachama wa CCM aitwaye Athuman Abdallah Sudi amechukua fomu za kugombea Ubunge kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kwa jina la CHADEMA.

Jacob amesema hii ni mara ya pili Mkurugenzi huyo anaihujumu CHADEMA kwa kutumia barua fake.

Jacob ameripoti haya katika akaunti yake ya twitter.




Maendeleo hayana vyama!


Muda si rafiki kwao hawa CHADEMA...

Kama wana uhakika hawajamwidhinisha huyo mtu kwenda kufanya uhuni huo, wachukue hatua haraka za kisheria...

Na ni rahisi, waripoti polisi ama waende mahakamani na kula kiapo kuwa huyo aliyefanya hivyo ni mhalifu...

Kama atatafutwa na polisi na asipatikane kujibu kesi yake, basi kisheria CHADEMA watakuwa na haki ya kupewa fomu zingine kwa mtu halali...

All in all CCM ni wajinga na wahuni sana....

By all means, watamficha huyo mtu. Watamtafutia wadhamini. Na ataonekana kwenye ballot papers hata kama yeye personally hataonekana hadi siku ya kupiga kura....

Ni mchezo wa kijinga na kipuuzi sana...
 
Muda si rafiki kwao hawa CHADEMA...

Kama wana uhakika hawajamwidhinisha huyo mtu kwenda kufanya uhuni huo, wachukue hatua haraka za kisheria...

Na ni rahisi, waripoti polisi ama waende mahakamani na kula kiapo kuwa huyo aliyefanya hivyo ni mhalifu...

Kama atatafutwa na polisi na asipatikane kujibu kesi yake, basi kisheria CHADEMA watakuwa na haki ya kupewa fomu zingine kwa mtu halali...

All in all CCM ni wajinga na wahuni sana....

By all means, watamficha huyo mtu. Watamtafutia wadhamini. Na ataonekana kwenye ballot papers hata kama yeye personally hataonekana hadi siku ya kupiga kura....

Ni mchezo wa kijinga na kipuuzi sana...
Na huyo mkurugenzi inaonekana mchezo huo wa kihuni anaujua vizuri.
 
Na huyo mkurugenzi inaonekana mchezo huo wa kihuni anaujua vizuri.

Hili liko wazi bila shaka....

Lakini wanaweza kuwa - outmart na kuupangua mchezo kirahisi sana kwa kutumia taratibu za kisheria unless huo mtandao wa kihuni uwe umetambaa mpaka mahakamani na polisi pamoja na NEC yenyewe...
 
Sikiliza video kwa makini....

Alisindikizwa na baadhi ya viongozj halali wa chadema ngazi ya wilaya kwenda kwa DED kuchukua form na barua iliyosainiwa.

Nadhani kuna walioshikishwa pesa kusaliti chadema....

Then haiwi kosa la tume kama barua halali na alisindikizwa ma delegate ya chadema.

Sio kweli acha upotoshaji wa kijinga, anayeteuliwa na chama anapewa barua rasmi ya chama. Kama kila anayeshiriki kwenye kura za maoni anaweza kwenda akapewa fomu, huo utakuwa ni utendaji wa kijima sana wa tume ya uchaguzi. Na isitoshe anayekwenda anajaza jina na taarifa zake, kama sio mtu sahihi inabidi akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kinyume na hapo tume ndio inayohusika na huo upuuzi.

Na hapo ndio tunaposema tume hii ya uchaguzi ni sehemu ya hujuma kwenye chaguzi zetu. Na kutaka kudhibitisha kuwa tume ndio inayoratibu huo uhuni, ndio maana haitaki watu waende na msafara ili waweze kuendesha hujuma vizuri.
 
Kila Mtanzania ameona yaliyofanywa na Mkurugenzi wa Wilaya ya Ubungo, Kuwapandikiza CCM kwenye nafasi za CHADEMA na kuwapa fomu ili waziharibu na kupunguza nguvu za upinzani.

Nimemsikia huyo mama mkurugenzi akiongea, anajua alichokifanya. Ni uongo mtu aliofanya jana.

Hivi kweli wewe mama unayoyafanya huna hata aibu, wakurugenzi wanawawinda CHADEMA na ACT Wazalendo, Kwanini uwapandikize watu?

Huu uchaguzi ni wa kihuni, kwanini CCM na jeshi la Polisi mnawakataza watu wasilinde kura zao? Polisi hao na CCM ndiyo wezi wakubwa wa masanduku ya kura, tumeona mifano siku za nyuma polisi wakichukua sanduku la kura huko Kinondoni na kulirudisha baada ya masaa mawili. Hivi hamna aibu? Tendeni haki ili muwe na credibility.

Mnatafuta ushindi wa nguvu, kama hampendwi hampendwi tu. CCM hampendwi hata kidogo.
 
Kabisa hawapendwi, kama wanapendwa waache wananchi waamue sio kufanya upuuzi uliopitiliza yule Betrice anasema eti aliechukua fomu hamjui na hata namba ya simu eti hakuandika kwenye kitabu, hivi inaingia akilini kweli.
 
Hivi huyu mama hana ndugu wa kumshauri kuwa kitendo cha kugawa form ya Chadema kwa mwanaccm mwenzake kitazua balaa kubwa na waliomtuma watakuja kumruka kimanga? Shauri yake atakuja kunyea debe peke yake hata hiyo hela aliyopewa hataitumia kwani atakuwa jela.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom