Utaratibu wa kupata kibali cha uvunaji miti

Fideline

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
234
124
Umuofia kwenu! Kwenu!

Wadau nimekuja hapa kuomba mwongozo juu ya taratibu za kupata kibali cha uvunaji miti ya asili shambani kwangu.

Nimenunua shamba wilaya ya Kilindi na niko mbioni kulisafisha kwa kukata miti iliyopo ili niweze kufanya kilimo.

Baadhi ya wanakijiji kwa kuogopa urasimu ama kwa kutokujua wanasafisha mashamba yao kwa njia zisizo na tija kwa kuichoma miti iliyopo.

Naomba ufafanuzi kwa anayejua taratibu za kuomba kibali maliasili ili niweze kuikata miti iliyopo shambani na kupasua mbao.

Nawasilisha kwa msaada zaidi.

miti.jpg
 
.....Yaweee!!

Mkuu, cha kufanya andika barua ya maombi ya kutaka kuvuna miti ya asili iliyopo katika Shamba lako kwa lengo la kusafisha Shamba, barua hiyo iende kwa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uvunaji wa Wilaya. Nakala ya barua ipeleke kwa Meneja wa Wakala wa Misitu Wilaya ya Kilindi.

Huko watakupa ruhusa/kibali na taratibu za kufuata.

Ukishaandika barua uwe unafuatilia maana navyozifahamu Ofisi za Serikali hususan Wilayani huwa wanachukua maamuzi slowly sana.

Ni hayo tu!!
 
Wala usitumie nguvu nyingi mkuu kwenda mpaka wilayani utapoteza pesa myingi sana.
Issues kama hizi maliza hukohuko kijijini ndo utafanyakazi bila zengwe.

Muone mtendaji wa kijiji akuandikie kibali ni sh50000 baada ya hapo cheza na kamati ya mazingira hapo kijijini bila kumsahau m/kiti wa kijiji.

Katika mlolongo wote huo haitazidi 250000 ila utakiwa umejitengenezea mazingira mazuri sana ya ufanyajikazi maana hata ukitaka kusafirisha mzigo kibali muhimu ni kile cha kijijini.

Halafu kingine mhimu kabisa kabla hujaanza pilika za mkaa na mbao wadau wakuu wa kusafirisha mzigo kwenda dar wapo Mkata na Mbwewe wana magari na vibali rasmi kwajili ya kazi hiyo.

N.B Kwa info zaidi tuwasiliane mkuu.
 
Kisima Naungana nawe,
Anzia ofisi ya kijiji, hasa kamati ya ardhi ili wakwambie kama eneo lako liko kwenye zone ya kilimo, kisha kama wakikwambia eneo lako ni la kilimo, omba kibali cha kusafisha shamba kwa kuvuna mbao na mkaa.

Wilayani ungeenda kama wewe ni mfanyabiashara wa mbao/mkaa,au kama scale ya shamba lako ni kubwa sana kuzidi eka 50 hivi za msitu, au kama ungekuwa unapakana na hifadhi ya msitu.
 
Back
Top Bottom