Kibali cha ujenzi

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
7,587
12,114
Heshima kwenu wakuu!
Naomba kujua kwa wenye kujua.

Hapa mtaani kwetu wamekuja maafisa kutoka jiji na kupita kila nyumba na kuwaandikia "STOP KIBALI" na wamefanya makadirio kila wanavyoithaminisha nyumba,wakiona nyumba nzuri wanasema malipo ya kibali ni laki moja na faini ya kujenga bila kibali ni laki na hamsini.Jumla laki mbili na hamsini.

Najiuliza huu utaratibu unaotumika na hawa watendaji upo kisheria au?
Maana nyumba zimejengwa miaka mingi zaidi ya 10 iliyopita lakini leo wanatuandikia STOP KIBALI.

Ukizingatia maeneo hayo bado hayajapimwa na hayana hati miliki/plot numbers.

Je sheria inasemaje kwa watu waliojenga maeneo yasio pimwa au yasio na gari miliki ni lazima kabla ya kujenga uwe na kibali?
Asanteni.
 
Serekali haina hela baba. Pambana nayo hivyo hivyo utafika tu. Al muhimu lipa walichokuaandikia. Usibishane na serekali yako. Hapo pesa yako ndio itasaidia kule kwa Elimu bure na mambo mengine.
 
Kuna utaratibu wa kupata kibali cha ujenzi kwenye eneo ambalo halijapimwa. Peleka
1.vielelezo vya mauziano ya kiwanja kutoka serikali za mitaa
2.mchoro wa unachojenga ambatanisha na form za maombi utapata kibali cha ujenzi
 
Nenda manispaa ya sehemu husika, ukifika pale utapewa fomu za kujaza ili ueleze nyumba yako ni mfuto au ghorofa
Fomu utasaini kwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa, then diwani then afisa tarafa, wakisaini hao wote unarudi tena manispaa pale unakutana na town planner anachukua GPS mnaenda nae site kwako,
Mkifika site utamuonyesha mipaka ya kiwanja chako na majirani zako then atachukua coordinate, mtarudi tena manispaa then ataingiza zile data ktk computer kuangalia kama eneo lako liliandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa Makazi, viwanda , biashara , barabara n.k,
Kama ni eneo la Makazi itakua nafuu kwako watakusainia then utaenda idara ya ujenzi ili upewe kibali, ili upate kibali unapaswa uwe na mchoro wa nyumba yako na ipigwe muhuri,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama town planner wa manispaa kashindwa kuona katika mchoro wa manispaa basi zile coordinates peleka wizara ya ardhi then wao watakuambia lile eneo ni eneo la Makazi ama laa

Ulisha jaribu na kuona inachukua Muda gani? Na Russa kiasi gani?
Kila mtu anataka kibali ila hawa ma fisi wanatukwamisha ndio maana tunajijengea tu. Jiulize kwa mwaka Jana mzima. Jiji au wizara imepima na kuuza viwanja vingapi ?
Remember. Nature abhors a vacuum
 
Kama nimeshajenga miaka 10 nyuma ila ninepata pesa kidogo nataka kuendeleza hata plasta vyumba viwili je hapo kunahitaji kibali?na je vp kama naishi humohumo kwenye nyumba ambayo haina kibali cha ujenzi?

tatizo lugha
 
Siku hizi baadhi ya halmashauri wameanzisha utaratibu wa kutoa vibali vya ujenzi hata katika maeneo yasiyopimwa, pia kama ulijenga zamani unapigwa faini ambayo ni asilimia ya makadirio ya gharama ya jengo na unalipia gharama ya kibali. Nadhani pia ni njia ya kuongeza makusanyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wahindi mbona ni mabilionea na hawajenga?
Wahindi waliacha kujenga baada ya sheria ya utaifishaji wa majengo ya mwaka 1971 ambapo nyumba zote zenye thamani ya zaidi ya shilingi 100,000/= wakati huo zilitaifishwa. Hivyo kama ulikuwa na nyumba zaidi ya moja uliachiwa moja tu kwa ajili ya familia na nyingine kutaifishwa. Inasemekana familia ya Karimjee walipoteza zaidi ya nyumba 100 kwa Dar es salam pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulisha jaribu na kuona inachukua Muda gani? Na Russa kiasi gani?
Kila mtu anataka kibali ila hawa ma fisi wanatukwamisha ndio maana tunajijengea tu. Jiulize kwa mwaka Jana mzima. Jiji au wizara imepima na kuuza viwanja vingapi ?
Remember. Nature abhors a vacuum
Niko kwenye process.
 
Kama town planner wa manispaa kashindwa kuona katika mchoro wa manispaa basi zile coordinates peleka wizara ya ardhi then wao watakuambia lile eneo ni eneo la Makazi ama laa

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko wizarani wakiona ni eneo la makazi watakupa nyaraka gani ili uitumie kama uthibitisho kutoka kwao na hivyo kuendelea na huo mchakato wa kupata kibali cha ujenzi kule manispaa ulikoanzia?

Maana ukitoka wizarani lazima manispaa nao wajiridhishe na matumizi ya eneo kabla hawajakupa hicho kibali.
 
Ingekuwa mtu anaishia serikali ingekuwa afadhali lakini ni eti hadi manispaa?!
Hali hii imefanya ujenzi wa mtu mmoja mmoja kutofanyika kabisa kutokana na huo urasimu wa nenda kule na kule!
Pamoja na kwamba sababu kubwa ni changa ya kiuchumi iliyopelekea kiwango cha ujenzi kushuka sana lakini pia swala la vibali limeathiri sana ujenzi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom