Diana-DaboDiff
JF-Expert Member
- Jul 13, 2009
- 376
- 18
Kwenye miaka ya tisini baada ya tume ya Nyalali kurekebisha sheria kipengele cha kuomba kibali polisi kilifutwa na tukaambiwa mkitaka kuandamana munawajulisha polisi watoe ulinzi. Kuna nyimbo ya Bob Mapesa wa Kenya anauliza kila mara 'tuko mbele au tuko nyuma' mpenzi wake anajibu tuko mbele,sio nia yangu kuongelea wimbo huu lakini nauliza pia 'tunaenda mbele au nyuma' ?
Miaka ya hivi karibuni naona kile kipengele cha kuomba kibali polisi kimerudi kinyemela utasikia polisi wamezuia kundi flani kuandamana.Naomba wanasheria humu ndani watujulishe ni vipi tunaomba kibali au tunawajulisha polisi tukitaka kuandamana ?