wehoodie
JF-Expert Member
- Nov 20, 2011
- 1,021
- 992
Wakuu
Naomba msaada wa kimaelekezo namna ya kupata International Driving Permit (IDP) kutoka hawajamaa wa AAT ambao naamini ndio issuing authority Tanzania. Zaidi ningependa kupata mtu aliepata anipe uzoefu wake, je yawezekana kuipata bila muhitaji kufika physically kwa hawajamaa naaminisha kwa kutumia mtu n.k.
Hivi kwa nini Taasisi kama hizi hawana hata website?
Note. Muhitaji wa IDP anayo leseni yakwaida (zile mpya) inayotolewa na TRA.
Shukrani!

Leseni ya kimataifa
UTARATIBU WA KUPATA &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; INTERNATIONAL DRIVING PERMIT
HAPA NCHINI.
- Mwombaji anatakiwa kuwa na leseni ya Udereva ya daraja lolote lile iliyo hai ya hapa Nchini.
- Anatakiwa kuipeleka leseni yake ofisi ya Mamlaka ya Leseni (T) TRA kwa ajili ya ukaguzi,
- Baada ya Ukaguzi, Mamlaka ya Leseni (T) TRA itatoa barua rasmi kwenda kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani(T) kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo.
- Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itakagua leseni hiyo pamoja na cheti cha Umahiri (Certificate of Competence) kuthibitisha uhalali wa leseni na cheti hicho cha umahiri.
- Baada ya kuthibitisha uhalali wa leseni hiyo, Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (T) itatoa barua rasmi kwenda Oisi ya Automobile Association Tanzania ambayo ndiyo asasi pekee hapa nchini yenye Mamlaka ya kutoa leseni za Kimataifa.