Kibali biashara ya mkaa - DSM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibali biashara ya mkaa - DSM

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by C.K, Oct 19, 2011.

 1. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Salaam!

  Naomba anayejua kibali cha kuuza mkaa kinapatikanaje - wapi na kwa bei gani kwa muda gani (miezi 6 na mwaka). Pls help me with relevant info.

  Asante!
   
 2. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Uko mkoa gani? Kila mkoa na kanuni zake. Mfano dar usajili unapatikana halmashauri unayotaka kufanyia biashara yako. Pwani usajili unapatikana halmashauri pia lakini lazima uwe na mukhtasari wa kijiji unachovuna mkaa, moro sasa hivi wamezuia vibali na usajili.
  Vibali vya pwani ni 4200 ya maliasili kwa gunia na 1000 ya halmashauri kwa gunia, hivyo basi kila gunia litakugharimu 5200, hiyo ni baada ya kuwa na usajili ambao ni 205,000 kwa mwaka.

  Kwa dar ni hiyo hiyo 205,000 kwa mwaka, lakini sijui kama kuna vibali vya mkaa hapa kwakuwa sidhani kama kuna sehem wanaruhusu kuchoma mkaa.

  Morogoro ni 6000 kwa gunia, ambayo 4000 maliasili na 2000 halmashauri.

  Unazo taarifa za usafiri? (Kila gunia litakugharimu 6000) kama unavyo vibali mwenyewe. Ila hiyo isikusumbue, tafuta fuso au canter yenye vibali we unalipa unaweka kishoka mkapa unafika, dereva atahusika kila sehemu ya maliasili na ukaguzi. Ila hakikisha tu ni vya kweli. Usije kulaza mzigo barabarani kwa kupitisha mzigo na vibali feki.
   
 3. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45

  Shukrani kwa taarifa hizo tosherevu!
   
 4. samito

  samito JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mkuu ebu naomba maujuzi nikitaka kuuzia mkaa dar, je niende kijiji gani ambako nitanunua jumla jumla? em nipe strategy labda hii bizness itanitoa
   
 5. T

  Tabalo JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2015
  Joined: Feb 10, 2013
  Messages: 235
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  vp kwa mkoa mwanza gharama za kuchoma mkaa zinakuwaje?
  msaada tafadhali
   
Loading...