Kibaki Afuta Adhabu Ya Kunyongwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibaki Afuta Adhabu Ya Kunyongwa.

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Junius, Aug 3, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Rais Mwai Emilio Kibaki wa Kenya ametoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 4000 waliohukumiwa kunyongwa na badala yake watatumikiwa kifungo cha maisha.
  Msamaha huo unawahusu wafungwa wote waliohukumiwa kifo ambao wanasubiri hukumu hiyo katika gereza kuu la Kamiti lillopo katika viunga la jiji la Nairobi.
  Taarifa hiyo ya rais Kibaki iliyosomwa na makamo wa rais wa Kenya Bw. Kalonzo Musyoka ilisema kuwa msamaha huo hauna maana kuwa nchi ya Kenya imepiga marufuku adhabu ya kifo na amesisitiza kuwa mahakama bado zinaweza kuendelea kutoa adhabu hiyo.
  "wafungwa wanaosubiri kunyongwa hawafanyi kazi yoyote gerezani, wamekaa tu, wanakula na wanalala hivyo wanakuwa mzigo kwa serikali na inawathiri kisaikolojia kukaa tu wakisubiri siku gani watanyongwa" ilisema taarifa ya rais Kibaki.
  Wafungwa hao ambao wengine wana miaka zaidi ya 22 gerezani wakisubiri hukumu hiyo sasa watatumikia vifungo vya maisha.
  Kenya haijatekeleza adhabu ya kifo kwa zaidi ya miongo miwili sasa na rais Kibaki amewataka wataalamu wa sheria kuweka majadiliano ya kitaifa kutafuta namna ya kupiga vita adhabu ya kifo ambayo bado ipo katka sheria za Kenya licha ya msamaha huo wa rais.
  Hatua hiyo inakuja siku chache tu baada ya wafungwa wanaosubiri kunyongwa katika gereza moja nchini Kenya kufanya fujo na vituko katika chumba cha gereza wakishinikiza kutekelezwa adhabu zao badala ya kuachwa wakiteseka.
  Nchi za karibuni kabisa kufuta adhabu hiyo ya kifo katka sheria zake barani Afrika ni Rwanda na Togo.

  source:voa
   
Loading...