Kibaka angushiwa kichapo na kuvuliwa nguo zote hadharani!!

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,464
2,000


KATIKA hali ya kushangaza mwishoni mwa wiki hii kibaka mmoja mbaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alinusurika kufa mikononi mwa wananchi wenye hasira kali huko Port Elizabeth nchini SOUTH AFRICA,

Mwanadishi wetu aliyeko nchini humo anatuarifu kuwa chanzo kikubwa na tukio ni kibaka huyo alipokuwa katika jitihada zake za kumpora mali ya mtu ambaye alipiga kelele za kuashiria kuporwa mali yake hiyo. Ndipo raia walipokusanyika na kuanza kumuangushia kichapo kibaka huyo kwa kumpiga kwa kutumia silaha mbali mbali yakiwemo na mawe na vitu vyenye ncha kali.

Hata hivyo Polisi walikuwa karibu kunusuru maisha ya kijana huyo ambaye alikuwa tayari ameshajeruhiwa vya kutosha pamoja na kuvuliwa NGUO zake zote na kubaki kama alivyozaliwa.

Kijana huyo kwa sasa yupo ndani akisubiri Kesi yake kutajwa, Wananchi katika eneo hilo la Port Elizabeth wamekuwa na mtindo wa kuuwa vibaka kwa staili ambayo mara nyingi imekuwa ikipigiwa makelele na vyombo vingi vya habari NCHINI humo!!
 
Top Bottom